Pinda ahitimisha mjadala wa hotuba ya rais bungeni

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,598
3,671
anahitimisha mjadala wa hotuba ya rais kwa kufanya comparison ya kile kilichokuwapo kabla ya uhuru akilinganisha na leo, nachoona mimi anapwaya kujaribu kulinganisha maendeleo ya watu ya miaka ya 1960 ambapo idadi kupwa ya watu waliopo sasa wana wastani wa miaka 25 hadi 30, kimsingi hajaeleweka anatumia nguvu kubwa sana kujieleza:msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela:
 
Sio kweli, sio kweli na sio kweli hata kidogo kuwa asilimia 80 ya Watanzania wakaao mjini wanapata huduma ya uhakika ya maji safi. Pinda kadanganya hivyo wakati akihitimisha hotuba ya rais bungeni jioni hii.
 
Ni kweli hotuba ya pm ilikuwa nzuri na yenye mvuto kusikiliza ila ameweka kichefuchefu alipo anza kufanya comparison kati ya maendeleo yaliyo fanywa na wakoloni na yaliyopatikana na baada ya miaka hamsini ya uhuru, shule, wanafunzi huduma za afya, barabara nk.ni lazima pm ajue wakoloni wakuja Tanzania kuleta maendeleo ila kunyonya nakuondoka hivyo walivyo acha kwao ni sawa.sasa baada uhuru wenye nchi ndo sasa walitakiwa kufanya kazi kwa bidii kujiletea maendeleo yao wenyewe jambo ambalo serikali ya awamu ya kwanza ilitekeleza kwa dhati sana. Pm katika hotuba yake alitakiwa kufanya comparison ya maendeleo kati ya nchi zilizopata uhuru pamoja na Tanzania ndio aseme kwamba serikali imefanya kazi kubwa au haijafanya kazi yoyote. pia akumbuke serikali inayo lalamikwa ni hii ya jk. awamu ya kwanza ilifanya vizuri sana mbali na kuwa na changa moto nyingi. awamu ya kwanza ililenga katika kujenga misingi ya kuzalisha mali ndo maana kulikuwa na viwanda vingi.sasa hivi wanachakachua tu. Pm alitakiwa aseme dhahili serikari yake imefanya nini na wanatarajia kufanyia nini watanzania maskini.Tuangalie nchi za Asia ambazo zimepiga maendeleo wakati zilikuwa maskini kama sisi.
Wana Jf ejadilini.
 
Zama za bunge la kutia muhuri kila kitu kutoka serikalini bila akili ya kuhoji zimerudi! Oh spika sitta uko wapi?
 
hizo takwimu ni wataalam wamempa au ni hisia zake?hana washauri wazuri huyo mzee,wadarisalama sijui wamelichukuliaje hilo tamko,anyway alakini kule wanakoishi wao hayo matatizo ya mgao wa maji na umeme ni sawa na hip hop yakichina ,hautokaa uisikie kamwe.
 
Waziri Mkuu Mhe Pinda leo ametoa hotuba ya kuahirisha bunge mjini Dodoma. Katika hotuba yake ameelezea mafanikio makubwa ya serikali ya awmu ya 4 inayoongozwa na Dk Kikwete. Natumai Great thinkers mlikuwa mnaifuatilia hotuba hiyo neno kwa neno.
Umeguswa wapi na nini kimekugusa ktk hotuba yake?
 
maji tunaoga ya chumvi, tunakunywa ya chumvi hayo maji niliyaona mara ya mwisho bombani kwangu miezi sita sasa imepita. dawasco walikuja eti wanadai bili yao nikawaambia wang'oe bomba lao tuu maana naona halina dili.PINDA KACHEMKA TENA!!!!!!
 
Kulinganisha miaka ya ukoloni na miaka ya uhuru siyo kitu rahisi kama wengine wanavyotaka tuamini; maana walipokuja wakoloni apakuwepo nchi inaitwa Tanganyika, isipokuwa viinchi vidogo vidogo vilivyoundwa na makabila yaliyokuwepo. Aidha hapakuwepo mawasiliano ya aina yeyote, iwe barabara, reli, ndege n.k. Hapakuwepo kilimo cha mazao ya biashara. Hapakuwepo mashule,hata ya kufundisha watu kusoma na kuandika n.k. Kwa maneno mengine wakoloni walianzia kwenye sufuli, hivyo ni vigumu kuwalinganisha na wale wanaoanzia kwenye "plus"
 
Dar es Salaam kwenyewe asilimia ya wapatao maji ya DAWASA haisogei 80, sembuse vijijini?
 

.
Yeleuuuwi uwor'e meso phoe?
Eler'i tsikyeri kufoi, CRDB, NMB, NBC, BOA, CITY NK mabenki wa woose waichur'ie eler'i ipho makapatinyi wake. Suka ndaayo undekur'ikaho tsapho iwinyi.
.
 
TUNATAKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA TUME HURU
YA UCHAGUZI BUNGENI SASA HIVI!!!


Enyi Ndugu Waheshimiwa viongozi wetu

akina Kikwete, Dr Slaa, Prof Lipumba, Mbowe, Julius Mtatiro, Zitto Kabwe, Mbatia, Dr Mvungi, Prof Baregu, Prof Mukandala, Dr Bana, Dr Azaveli, Mama Nkya, Ndg Mgaya, Makwaia wa Kuhenga, Jenerali Ulimwengu, Reginald Mengi, Pius Msekwa, Fredrick Sumaye Fredrick Msuya, John Malecela, Mama Anna Makinda, Sheik Issa Bin Simba, Mhe Iddi Simba, Maaskofu na Wachungaji wote nchini, Denis Mwamnyange, Said Mwema, The Othma's, Tundu Lissu, Sitta, Mwakyembe, Mzee Mkapa, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Sinde Warioba, Mzee Butiku, Prof Sarungi, Selasini, Ole Sendeka, Tido Mhando, Mama Maria Nyerere, Mama Karume, Selelii, Prof Bangu, Dr Matumaini, Bashe, Celina Kombani, Kafulila, Hamad Rashid, Regia, Lukuvi, Mama Maghimbi,Mama Anna Abdala, Pombe Magufuli, Mstaarabu wa Siasa Tanzania - Dr Mohammed Shein, Salmin Amour, Godbless Lema, Mzee Mwanakijiji, Maxence Melo, Candid Scope, Fareed, Mwakalebela, Mnyika, Halima Mdee, viongozi wote wa serikali za wanafunzi vyuoni ... na wengine wengi wengi wengi tu, sisi kama vijana wa nchi hii sasa hivi tunawaulizeni nyote kwa pamoja kwamba ...

... suala letu la michakato wa kujiandikia KATIBA MPYA na kuunda Tume Huru ya Uchaguzi ZINAANZA LINI BUNGENI???
 
Hotuba yake ilikuwa inajibu maswali ambayo alikuwa nayo kichwani au ameyasikia mitaani. Kuelezea maendeleo kwa kulinganisha alichofanya mkoloni na kilichofanywa na serikali hasa ya awamu ya nne ni aina ya ufedhuli.

Pinda amejikita tu juu ya ongezeko la vitu lakini si ubora wa huduma. Ongezeko la vitu imeendana na ongezeko la watu vile vile. wananchi wa sasa wamejitahidi kuleta maendeleo kuliko ambavyo serikali imefanya kwa upande wake. Shule za kata alizozungumzia zimejengwa na wananchi kuliko ambavyo serikali inataka tuamini.

Pinda anafikiri wananchi hatujui kuwa uchumi wa nchi hii unadumaa kwa sababu kuna kundi dogo limehodhi uchumi wa nchi na ndio wanaotuamulia hata viongozi wa kutuongoza. amesahau kuwa kuna siku aliwahi kusema bungeni kuwa mafisadi waliokwapua fedha za EPA hawakamatiki kirahisi kwa sababu wanaweza kuyumbisha uchumi wa nchi.
 
Hivi we Biendangwero umezaliwa lini? Unajua kua kabla ya mkoloni wazee wetu walikuwa wan ujuzi wa kufua chuma. Na awamu ya kwanzandiyo iliyoondoa ukabila. Miaka 50 ya uhuru tunge paswa kuwa kama Malesha au Singapo. Usiongee kama umechakachuliwa, kuwa kama kijana wa leo. Ee Mungu tusaidie wa TZ tuamke. Hao kina Januari, Baba zao wanatafuta pa kujifichia.
 
Back
Top Bottom