vimon
Senior Member
- Apr 3, 2008
- 183
- 195
Pinda amekamilisha mkutano na waandishi wa habari hivi punde na meseji ya kubwa kwa madaktari ni kuwaambia kuwa serikali haiwezekani kushinikizwa na madaktari na kuwafukuza mawaziri Mponda na Nkya. Hivyo, kama wanataka kugoma, wagome tu.
Legal and Human Rights Centre
Mkutano wa Wanaharakati na Waandishi wa Habari: Sehemu ya tamko: "...kama kweli Rais Jakaya Kikwete ana nia ya dhati ya kutetea maisha ya Watanzania, tangu Jumamosi hadi leo angelikuwa amekwishachukua hatua ili kuzuia maafa yatakayotokea ikiwemo vifo zaidi vya Watanzania kutokana na mgomo mwingine wa Madaktari. Wananchi tunamtaka Rais atekeleze madai ya madaktari mara... moja, yakiwemo yafuatayo:
1. Waziri wa Afya na Naibu wake, ambao wameshindwa kujiuzulu hadi sasa wawajibishwe na Rais aliyewaweka madarakani ili wapishe mchakato wa kutatua mgogoro walioshindwa kuudhibiti, uweze kutatuliwa;
2. Huduma ya afya na mazingira ya kazi yaboreshwe haraka iwezekanavyo, kwani hali hiyo ndiyo inawafedhehesha madaktari katika kutumia taaluma walizo nazo;
3. Iwapo serikali haitatimiza hayo, italazimisha umma wa Watanzania kuchukua hatua dhidi ya wote wanaohusika kwa njia ya nguvu za umma, kuanzia Tarehe 07/03/2012;
4. Tunawasihi Watanzania wote wanaojali utu wao na utu wa Watanzania wenzao wawe tayari kuinuka kuchukua hatua itakayoifanya serikali kutimiza wajibu wake katika kuzuia watu zaidi kupoteza maisha. Ni sisi Watanzania wenye uchungu na nchi yetu na maisha yetu. Imesainiwa leo, Tarehe 06/03/2012"
Maswali ya kujiuliza je hawa viongozi wetu wanataka tufe,wakina mama wajawazito nani atawafanyia operesheni na watoto wasio na hatia nani atawahudumia. Tetesi madaktari wamekasirishwa na kauli ya pinda na wameapa kumwonyesha kuwa wao si watu wakupiga siasa.
Angalizo kama unaumwa na huna pesa za kwenda India,jitaidi uende hospitali leo hii. Ukipata Tangazo hili mwarifu na mwenzako.