Pinda afika Kiteto kuona ujenzi wa jengo la bil 4.5 uliokwama.

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Waziri Mkuu mstaafu, na mlezi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Manyara, Mhe Mizengo Pinda, amefika Kiteto na kushuhudia ujenzi wa jengo la halmashauri ya Wilaya hiyo ambao umesimama kwa kukosa fedha.

Akisoma taarifa Afisa utunishi kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona, alitaja thamani ya jengo hilo kuwa ni Tsh 4,502,411,452.

Alisema jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2016 na kutegemewa kukamilika mwaka 2018.

Kiasi cha fedha kilichopokelewa na halm kwaajili ya ujenzi ni Tsh 1,950,000,000 na ambacho bado ni 2,552,411,452.

Kambona alisema uongozi wa Wilaya umekuwa na jitihada kubwa kuwasikiana na TAMISEMI na kumwomba Mhe Pinda, mlezi wa Mkoa wa Manyara kulisemea kwa ukaribu suala hili ili fedha hizo zipatikane kukamilisha jengo hilo.

Kukamilika kwa ujenzi huu kutasaidia watumishi kupata mazingira bora ya kufanya kazi, hivyo kuongeza morali na ufanisi zaidi wa kufanya kazi katika kuhudumia jamii.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbunge alitosha kufatilia fedha za ujenzi tamisemi.Huyo mstaafu apumzike ale pension na akalime.
Huo ni aina mpya ya ufujaji wa fedha za walipa kodi.Hizo nafasi za ulezi ni upigaji na mwendelezo wa mlolongo wa matumizi yasiyo ya lazima
 
Mkuu kila Wizara ameipa Bilion 1 ijenge jengo lake huko Dodoma alafu Jeno la Halmashauri linaghalimu Bilion 4 ambazo ata Hospital anayojenga Dodoma bado bajeti haifiki Bilion 4! Kuna kazi
 
Back
Top Bottom