Pinda afichua tuhuma nzito kigogo wizara ya afya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda afichua tuhuma nzito kigogo wizara ya afya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Feb 11, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Awali, Pinda alitangaza kuwasimamisha kazi Nyoni na Dk. Mtasiwa na kusema amefikia hatua hiyo kutokana na kupokea malalamiko mengi dhidi yao.

  Alisema zipo tuhuma mbalimbali dhidi yao zikiwemo sare za wauguzi na vifaa vya kupima Ukimwi vilivyonunuliwa vikiwa ni feki na kwamba mwenye mradi ni mmoja wa vigogo wizarani.
  “Vifaa hivyo vya kupimia Ukimwi havikuwa katika ubora na vilikuwa vinaonekana ni feki na mradi huo tumeambiwa ni wa wizara na hata tenda ya usafi katika Hospitali ya Muhimbili tumejulishwa ni mradi wa mtu wizarani,” alisema Pinda.

  Pinda alisema kutokana na malalamiko hayo, ameona ni lazima pawepo na tatizo na kuamua kuwasimamisha ili kupisha vyombo vya dola kuchunguza.

  IPPMedia
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Bungeni Dodoma
  Mjini Dodoma, Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyokuwa ikishughulikia mgomo huo, imekabidhi ripoti yake kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda na inadaiwa kuelezwa kuwa baadhi ya watendaji hao walishinikiza kampuni za kufanya usafi, MNH na kupitishwa kwa sare ya madereva wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI).

  "Wale madaktari tumekaa nao kila mmoja wetu (wabunge), alikuwa akibubujikwa machozi ukisikiliza shida zao... huyu (jina tunalo) anadaiwa licha ya Bodi ya Zabuni kupitisha sare kwa madereva wa MOI, alikwenda akashinikiza wapitishe kitambaa walichokataa," alidokeza mmoja wajumbe wa kamati hiyo.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hivi mlipopitisha Azimio la Zanzibar hawakujua kwamba haya mambo yapo na yanatokea kila wizara. Hata kama mradi ni wa waziri,mkewe au mtoto wake, mhusika hajafanya kosa maana sheria inawaruhusu na hii haiwezi kuwa sababu ya kumfukuza kazi..Viongozi wote serikalini wana miradi yao ndani ya wizara, Halmashauri na serikali za mitaa wanazoziendesha na hakuna msafi hata mmoja...
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuna jambo hapa linatakiwa kufanyiwa kazi. Kwa kawaida nchi nyingi hasa zinazokazia nidhamu ya watumishi serikalini hairuhusiwi mtumishi wa serikali kujihusisha katika tenda zinazohusiana na huduma ndani ya umma. Na kama kabla ya kuwa mtumishi au akiwa mtumishi wa umma anaanzisha miradi yake, inabidi aajiri watu wengine watakaoendesha lakini kwa masharti ya shughuli hizo kutofungamano ndani ya eneo la huduma yake au taasisi anayoongoza pamoja na serikali.
   
 5. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Hapa ni kinyume.............unashiriki asilimia 100 na ikiwezekana hata mali za umma uanzitumia kwenye shughulizako hizi binafsi kuahakikisha kuwa unapata faida kubwa
   
 6. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sioni kama kuna kilichoaharibika, ila hawa viongozi wamzetuzunguka nyuma.

  tahadhari ya jambo hilo limewekwa wazi kisheria, na sababu za kutangaza tenda serikalini ni kwa ajili ya kuepuka matatizo kama hayo, sasa nani wa kulaumiwa kama si vyuombo vya utendaji serikalini ambavyo kazi na wajibu wao ni pamoja na uchunguzi wa utendaji, uwajibikana na nidhamu ya viongozi? Usalama wa taifa wapi? Takukuru wapi?
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
  haya mambo ya kampuni za usafi na uniform ni mambo madogo sana!! Hawa ni majambazi wa hat ari!
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Umeona eeh? hakisemwi ambacho kina manufaa kwa Watanzania na kina athari kubwa kwao!
   
 9. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Arobaini zao zimekaribia kama sio kufika. Nani angehisi watu kama Mama Nyoni au Jairo wangepata aibu ya mwaka na CV zao kuwa na mauaridi yanukiayo ya experince????
   
 10. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nyoni alikua anajitapa sana kuwa, hakuna wa kumtoa hapo wizarani, labda yeye mwenyewe ndo aamue. Huyu mama alikua na kiburi sana, yeye pamoja na Deo Mtasiwa. Mtasiwa alikua ananata sana, ingawa alikuwa afupi kama mbilikimo lakini alikuwa anajiona kama mungu. Shame on them!
   
 11. c

  chakechake Member

  #11
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JF kama kawaida haipewi credit

  Wenye JF kama kawaida hawalalamiki na watu wakiweka threads za kuwa suta hawa waandishi wa habari na uozo wa vyombo vya habari Tanzania zinahamishwa.
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu uko sahihi kabisa. Kuna madudu yanafanyika huko serikalini wee acha tu. wacha wawachunguze tuona watakuja na issue gani kisha watupe solution. Sheria ya manunuzi inawataka wajumbe wa kamati ya utathimini wa tenda pamoja na wajumbe wa bodi ya uzabuni kujaza kajitu kanakoitwa convenant ukissma kwamba huna uhusiano na kampuni ambazo.zomeleta zabuni. Lakini sheria haisemi juu ya Afsa Masuuli yeye anadeclare wapi conflict of interest.

  Hilo la kushinikiza mtu apewe tenda kama halikufanywa kwa maandishi inakuwa ni vigumu mno kumtia hatiani Afsa Masuuli. Utaishia kuwatia hatiani wajumbe wa kamati ya utathmini na wajumbe wa bodi.
   
 13. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kwani ripoti za Ngereja,jailo,Meli ya MV surrender ziliishia wapi ukiishaona kitu kimeundiwa tume ujue ndio mchezo umeisha hapo........nimeshangaa kikao cha bunge hiki hawajagusia hata ile taarifa ya kina jairo,luhanjo n,k yaani hizi tume mie naona ni kupoteza muda tu sababu matokeo ya tume hayachukuliwi umuhimu hasa mapendekezo....hapa bora wabebe upinzani tu au la tupate mtu makini ambaye awe na udikteta fulani hv
   
 14. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Hapo hakuna tuhuma wala nini sema wanaondoa masalia ya Ndugu Luhanjo pale ikulu, Mtasikia mengi mwaka huu
   
 15. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  NEtwork error
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hongera utawala wa kikwete kuwatimua watuhumiwa
   
 17. b

  blacktanzanite Member

  #17
  Feb 12, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wana JF tunatakiwa kueleza madhambi makuu ambayo yamefikisha hapa mzozo wa madaktari wetu.maswala mengine kuna vyombo vya dola feki ndivyo ambavyo vinatakiwa kutupiwa lawama kwa kuwalinda hao majambazi(vigogo).ukweli ni sekta zote zimeoza serikali inaendeshwa kiundugunazation na zaidi kurithishana ...baba mwanzilishi wa nyumba kumi na mtoto kawkewa uwazili au ubunge hiii ya wapi?mtoto wa nyoka ni joka tuuuu.makampuni yanayofanya kazi na serikali ni ya watumishi wenyewe kwa vivuli vya watu wengine.ukitaka wewe utapata vikwazo 1000 au kukataliwa kwa kazi uzifanyazo ili ukwame...
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  mkuu sijasikia vizuri hebu rudia tena. Mkuu watuhumiwa huwa wanasimamishwa, tuhuma zinachunguzwa na zikithibitishwa wanatimuliwa au kufikishwa mahakamani.
   
 19. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #19
  Feb 12, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  yahee umeamua kuwageuzia kibao wenye JF!

  lakini kweli kuna hali ya kuwa JF wako too cosy na mainstream media
   
 20. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #20
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180

  kwa kuanza ......

  we need to oVERHAULL TISS........

  mfano kuna mengi madudu ambayo hawayaripoti hadi watu wapige kelee au wagome....e.g barabara za magufuli n.k....

  we also need TISS ambayo inatambua kuwa uchumi mzuri, bei ya nishati na upatikanaji wake.....uhakika wa chakula.....n.k. kitu ni sehemu ya agenda zake......

  cha ajabu TISS ya hapa hushinda kuchunguiza nani kahamia CDM!...na kuzuia maandamano.....
   
Loading...