Pinda abanwa na wananchi; akwepa maswali yao! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda abanwa na wananchi; akwepa maswali yao!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by vudee, Sep 18, 2011.

 1. v

  vudee New Member

  #1
  Sep 18, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pinda avuna aibu Musoma  • Ni baada ya kuahidi afya bure, wananchi wamzodoa waziwaz
  • Akiri kuwa Chadema ni chama kikubwa, asisitiza amani na utulivu
  • Nyerere amfunika, avuruga U-CCM kwenye ziara ya kiserikali

  Na Edward Kinabo, Musoma


  ZIARA ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, iliyoanza jana mjini Musoma mkoani Mara, ilipata msukosuko wa aina yake, kutokana na wananchi waliojitokeza kumsikiliza kuikatisha hotuba yake zaidi ya mara tatu, wakimpinga waziwazi baada ya kuahidi kuwa Serikali inajipanga kutoa huduma za afya bure.

  Pinda alikumbana na msukosuko huo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mukendo, mkutano uliohudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo hilo, Vicent Nyerere (Chadema), Meya wa mji huu, Alex Kisurura (Chadema), na viongozi wa waandamizi wa kiserikali wa Musoma na mkoa wa Mara.

  Wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo walianza kupaza sauti za kumpinga waziwazi Kiongozi huyo huku baadhi yao wakizomea, pale alipoanza kuzungumzia uzinduzi wa Zahanati ya Kanisa la Africa Inland Church alioufanya jana mchana katika kata ya Bwire.

  Akiisifu Zahanati hiyo, Pinda alisema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wote wa afya nchini na kwamba inataka kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za afya bure.

  Kauli hiyo ilizusha zogo kutoka kwa wananchi ambao walisikika wakiguna na kutoa kauli za kumkebehi.

  "aaah aaaah aaah, uongo uongo, hamuwezi, people ndio wanaweza, people ndio wanaweza" , ulisikika umati huo ukisema.

  People ndilo neno linalotumiwa na wananchi wengi wa Musoma kumaanisha "Chadema".

  Baada ya kupingwa na sauti hizo, Pinda alisema, "Pole pole jamani….looh, Pole pole jamani, mbona mnatupelekesha hivyo? Jamani eeeh, naomba niwaambie kuwa hata hivi sasa watoto na wazee wanatibiwa bure, na Watanzania wote wanaopelekwa nje kutibiwa magonjwa yasiyotibika hapa nchini, kama wanaokwenda China na India, wanagharamiwa na Serikali…kwa hiyo…".

  Hata hivyo, kabla hajaendelea zaidi na alichokuwa anasema, wananchi hao walimkatisha tena wakisema "hamna, hamna, wanaotibiwa nje ni mawaziri….oooh oooh, hamuwezi".

  Baada ya hali hiyo, Pinda alijikuta akiendelea kubishana na wananchi akisisitiza kuwa ni kweli wapo Watanzania wengi wa kawaida wanaotibiwa nje ya nchi bure kwa kugharamiwa na Serikali.

  "Wagonjwa wote wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi wanalipiwa na Serikali . Sehemu kubwa ya mzigo ule unabebwa na Serikali. Hiyo ndiyo pointi yangu …", alisema Pinda na wananchi wakaikatisha tena hotuba yake na kupaza sauti za kumpinga.

  "Naona kuna wanasiasa wengi sana hapa…", alisema Pinda na kubadilisha mada ya afya aliyokuwa akiizungumzia na kuhamia kwenye hoja ya kupanda kwa bei ya sukari ambapo alisema kuwa tayari ameshatoa maagizo kwa viongozi wa kiserikali kuhakikisha wanadhibiti tatizo hilo.

  Wakati akizungumzia hilo, baadhi ya wananchi walimkatisha tena wakimtaka ataje bei ya Sukari itakuwa ni shilingi ngapi, wakisema "tunataka bei...tunataka bei...tunataka bei".


  Licha ya kutakiwa kutaja bei, bado hakuitaja na badala yake alisisitiza kuwa amewaagiza viongozi wa serikali mkoa wa Mara kutazama kiasi cha sukari iliyopo kwenye maghala na kuhakikisha kuwa inauzwa kwa bei nafuu kwa wafanyabiashara wadogo kwani ana taarifa kuwa bei ya Sukari mkoani Mara imekuwa ikipanda kwa kasi kubwa kutokana na Sukari nyingi kuuzwa nchi jirani.

  Wananchi hao waliingilia tena hotuba ya Waziri Mkuu, wakimtaka awape nafasi ya kumuuliza maswali, lakini aliwaomba wamuache kwanza aendelee na ajenda yake akisema kuwa atawapa fursa hiyo mwishoni.

  "Jamani naomba basi mniache kidogo nimalizie ajenda yangu halafu hayo mambo mengine nitawapa nafasi baadaye", alisema Pinda.

  Hata hivyo katika hali iliyoonekana kuwashangaza wananchi wengi, Pinda alihitimisha hotuba hiyo bila kuwapa wananchi muda wa kuuliza maswali na badala yake alisema " Jamani tutafuta muda mwingine tuje tuzungumze kwa kirefu, ahsanteni sana", kisha aliingia kwenye gari na msafara ukaanza kuondoka.

  Mkuu wa wilaya ya Musoma mjini, Godfrey Ngatumi naye alikumbana na msukosuko wa wananchi wa Musoma pale alipotoa fursa kwa viongozi wa kiserikali kusalimia wananchi katika mkutano huo wa hadhara, ikiwa ni pamoja na kumpa nafasi Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine (CCM) na Waziri wa Kazi, Gaudensia Kabaka, lakini bila kumpa Nyerere nafasi ya kusalimia wananchi wake.

  Kutokana na hali hiyo, wananchi walipaza sauti wakitaka mbunge wao apewe nafasi ya kusalimia, hali iliyomlazimu Pinda kuingilia kati akiuliza "kuna nini", ndipo mkuu huyo wa wilaya akalazimika kumpa nafasi hiyo.

  Nyerere aliwasalimia wananchi hao kwa salamu ya Chadema ya Peoples Power, ambayo iliitikiwa kwa nguvu na umati wote wa wananchi huku wakimshangilia kwa nguvu.

  Na baada ya kumalizika kwa mkutano huo, umati wa wananchi uliimba "peoples power… peoples power" na kulizonga gari la Nyerere, wakimshangilia kwa nguvu na kumsindikiza, huku magari ya kiserikali yakiondoka kwa kasi uwanjani hapo.
  Ziara hiyo ilianza rasmi jana asubuhi kwa Pinda kutembelea Shule ya Msingi Mwisenge aliyosoma Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambapo aliahidi Serikali itafanya jitihada za kuhamasisha wadau wote kuiboresha shule hiyo ili kumuenzi Baba wa Taifa hasa katika kipindi hiki ambapo taifa linakwenda kuadhimisha miaka 50 ya uhuru.

  Akiwa shuleni hapo Pinda alipata nafasi ya kumsalimia Mzee James Irenge, mwenye umri wa miaka 121 ambaye aliwahi kumfundisha Hayati Mwalimu Nyerere katika shule hiyo ya Mwisenge kuanzia 1934 hadi mwaka 1936.

  "Nimefurahi kukutana na Mzee aliyemfundisha Mwalimu, nimeongea naye ameniambia ana tatizo la njaa, nikamwambia Mzee wewe sio wa kupata njaa….sasa tutakaa tutaangalia namna ya kumsaidia".

  Kabla ya kuwasili Pinda shuleni hapo, Nyerere alipinga Katibu wa CCM Mkoa wa Mara kupangwa kuketi meza kuu jirani na Waziri Mkuu, akisema ziara hiyo si ziara ya kichama bali ni ziara ya kiserikali na kuagiza kuwa nafasi hiyo aketi meya.

  Kutokana hali hiyo, maafisa usalama walimuhamisha katibu huyo wa CCM kutoka kwenye nafasi hiyo, na baadaye meya aliketi hapo.

  Ziara ya Pinda ambayo itachukua siku saba katika mkoa wa Mara itaendelea tena leo wilayani Butiama.
   
 2. s

  samoramsouth Senior Member

  #2
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante kwa habari. Peopleeeeeeeeees
   
 3. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndiyo tatizo la wanasiasa wa bongo, badala aeleze kinaga ubaga utatuzi wa matatizo ya wananchi yeye anasingizia wanasiasa wenzake ina maana matatizo yanachagua itikadi za vyama? Unajua mfano pointi ya kumuambia mtu wa Musoma (au mkoa mwingine haswa vijijini) eti kuna watanzania wanapelekwa kutibiwa nje hawezi kukuelewa, yeye alitakiwa asome mazingira na kuwaelewesha wananchi kwa lugha rahisi, kwani inawezekana hapo Musoma kuna wananchi wengi walishakufa au bado wanaugua halafu hawana hela za matibabu sasa unaposema kutibiwa bure nje ya nchi mwananchi wa kawaida atakuelewaje?
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Yeah Na Bado...
   
 5. R

  RMA JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natamani iwapo watanzania wote wangekuwa na mwamko na mang'amuzi kama ya watu wa Mara. Lakini kwa sababu ya kukosa uelewa, watanzania wengi wanaendelea kila siku kudanganywa na wanasiasa uchwara wa CCM!
   
 6. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CCM bado wanataka Watanzania wacheze ngoma yao wakati haiwezekani.
   
 7. Blandes

  Blandes JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2011
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mungu wangu washushie watu wa mikoa yote wawe kama vita murah,yaan nch ii itanyooka tu
   
 8. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Mtu mwongo anaogopa sana maswali kwani huwa wanaugonjwa wa kusahau sana.Pinda ni msanii sana kuliko kingwendu.kwani anaongoza kwenye viini macho vya ccm au chama cha mazingaombwe.
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Ngoma inogile...........
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  wengine wanakufa kwakushindwa kwenda hata mwimbili tu na sio nje naona kadanganya sana sasa kakosa cha kudanganya
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Na hili ndilo linalodhihirisha anguko la ccm
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wangeuonyesha mwamko huu wakati wa Mwalimu ningewasifu. Mwalimu aliiacha Mara hoi bin taaban si kwa miundombinu, elimu, uchumi,.... Watu wa Mara wakawa wanaishia darasa la nne na la saba tu kisha wanakimbilia jeshini.
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapo ndipo unaona uhuni wa viongozi magamba na serikali yake.

  Bila hata aibu mkuu wa wilaya ya musoma anamtambulisha mbunge wa tarime na kumuacha mbunge wa musoma? hata hivyo pongezi za pekee ziwaendee wananchi wa musoma ambao hawakukubali kuona mbunge wao akidharauliwa mbele yao.

  Uhuni mwingine wa magamba wanamuweka meza kuu mwenyekiti wa chama chao na kumuacha meya wa manispaa! kweli gamba kuu alisema magamba wanafanya siasa uchwara ndio hizi zilizotokea musoma.

  Watu wangu wa nyumbani mmefanya vizuri kumuonjesha joto Pinda ili siku nyingine akija musoma ajipange vizuri, asije kupiga porojo.
   
 14. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  laiti habari hii ingewafikia watu wote wa igunga basi tulikuwa tunachukua jimbo kiulainiii
   
 15. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapo ndiyo kazi inapokuwa kubwa kwani hawawezi kuwaita viongozi wa eneo lingine kusalimia watu na kuwatosa mayor na mbunge wa eneo husika hiyo ndio peoples power
   
 16. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Waalimu waliomfundisha mwl. Nyerere hawapaswi kulia njaa, ila wengine hata wakifa hakuna tabu. Huu ni upuuzi mtupu.
   
 17. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nawapongeza wananchi wa Musoma kwa mwamko huo. Thats the way how its supposed to be all over Tanzania!
   
 18. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,412
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  imetokea pia jana kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru mji mdogo kahama diwani wa chadema ilifukuzwa kwenye jukwaa kubwa baadae wakashauriana wakatangaza kumrudisha huwezi amini aliposalimia umati ulilipuka kwa nderemo na vifijo . alama za nyakati ni kitendawili kigumu sana kwa ccm
   
 19. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Muziki utakuwa mtamu pale watakapoona wamechelewa sana, mara itakuwa cha mtoto.
   
 20. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Hivi Igunga wamesoma habari hii... ! mungu niweke hai nipate kuona anguko la CCM!!
   
Loading...