Pinda aanza kupindisha madaraka yake

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Pinda aanza kupindisha madaraka yake

Katika kile kinachoelezwa kama kufuata nyayo za mtangulizi wake Bwana Lowassa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameanza kutumia fedha za serikali kujijenga uhalali katika chama. Waziri Mkuu tayari ameshaanza kuwapa hisani za aina mbalimbali viongozi mbalimbali wa CCM. Kadhalika, ameshaanza kutumia kofia yake kufanya kazi za CCM ili kujiweka karibu zaidi na viongozi wa hivi karibuni. Tukio la hivi karibuni la Bwana Pinda kutumia msafara wa kiserikali kwenda Iringa mara baada ya Mei Mosi kufungua tawi la CCM limeelezwa na baadhi ya wadadisi wa mambo kuwa sehemu ya mkakati huo. Hata hivyo, tayari viongozi kadhaa wa upinzani mkoani Iringa wameanza kulaumu kitendo hicho kuwa kinakidhana na Sheria ya Maadili ya Watumishi wa Umma. “Waziri Mkuu kama kiongozi wa umma anapaswa kufanya kazi zake bila kubagua watu kiitikadi, kitendo cha Bwana Pinda kutumia magari ya serikali, mafuta ya serikali na watendaji wa serikali kwenda kujenga chama chake. Na kuwabagua wanavyuo wenye itikadi tofauti katika hotuba yake hakipaswi kupita bila kukemewa”, alisema Mhadhiri mmoja wa chuo cha Tumaini ambaye hakupenda kutwajwa jina lake. Aidha, wanafunzi mbalimbali wa chuo hicho, wamesema kabla ya waziri mkuu kuja, wapo watu wanoasadikiwa kuwa wanausalama walifika katika chuo hicho na kufanya mahojiano na baadhi ya wanafunzi wanaoelekea kuwa mstari wa mbele kuunga mkono upinzani. Haijajulikana mara moja nini ilikuwa ajenda ya mazungumzo hayo. Hata hivyo, baadae ndipo baadhi viongozi wa wanafunzi walipopitisha karatasi zilizotaka wote wenye kutaka kazi serikali baada ya kuhitimu waorodheshe majina yao kwa ajili waziri mkuu kuyaona na hatimaye kupatiwa ajira. “Nimeshangaa wenzangu kuniambia kwamba jina langu limesemwa kati ya majina ya wananchama wa CCM 700 waliopokea kadi kwenye uzinduzi wa tawi pale Kihesa”, alisema mwanafunzi mmoja. Katika tukio hilo, waziri mkuu alitoa kadi kwa wanavyuo 700 hata hivyo ni wachache ndio waliojitokeza na kadi zilichukuliwa kwa niaba na wanachuo waliokuwepo siku hiyo. Kwa mujibu wa watu walio karibu na Waziri Mkuu Pinda, hii ni hatua ya awali katika mkakati kabambe wa kuweka mizizi ndani ya chama. Hata hivyo, wengine wameshaanza kulaumu kwamba hii ni hatua ya mwanzo ya Pinda kupindisha madaraka yake.

Chanzo: Paparazi Muwazi, Safarini Mbeya na Iringa
 
Katika nchi za watu wafuatiliaji wa mambo Pinda should be in big trouble.I doubt that will happen in Tanzania.
 
unakumbuka Denzel katika "Training Day"? "even King Kong got no shyt on me"... he is above the law.. at least visaluti na ving'ora vinamfanya ajihisi hivyo.
 
Pinda aanza kupindisha madaraka yake

Katika kile kinachoelezwa kama kufuata nyayo za mtangulizi wake Bwana Lowassa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameanza kutumia fedha za serikali kujijenga uhalali katika chama. Waziri Mkuu tayari ameshaanza kuwapa hisani za aina mbalimbali viongozi mbalimbali wa CCM. Kadhalika, ameshaanza kutumia kofia yake kufanya kazi za CCM ili kujiweka karibu zaidi na viongozi wa hivi karibuni. Tukio la hivi karibuni la Bwana Pinda kutumia msafara wa kiserikali kwenda Iringa mara baada ya Mei Mosi kufungua tawi la CCM limeelezwa na baadhi ya wadadisi wa mambo kuwa sehemu ya mkakati huo. Hata hivyo, tayari viongozi kadhaa wa upinzani mkoani Iringa wameanza kulaumu kitendo hicho kuwa kinakidhana na Sheria ya Maadili ya Watumishi wa Umma. “Waziri Mkuu kama kiongozi wa umma anapaswa kufanya kazi zake bila kubagua watu kiitikadi, kitendo cha Bwana Pinda kutumia magari ya serikali, mafuta ya serikali na watendaji wa serikali kwenda kujenga chama chake. Na kuwabagua wanavyuo wenye itikadi tofauti katika hotuba yake hakipaswi kupita bila kukemewa”, alisema Mhadhiri mmoja wa chuo cha Tumaini ambaye hakupenda kutwajwa jina lake. Aidha, wanafunzi mbalimbali wa chuo hicho, wamesema kabla ya waziri mkuu kuja, wapo watu wanoasadikiwa kuwa wanausalama walifika katika chuo hicho na kufanya mahojiano na baadhi ya wanafunzi wanaoelekea kuwa mstari wa mbele kuunga mkono upinzani. Haijajulikana mara moja nini ilikuwa ajenda ya mazungumzo hayo. Hata hivyo, baadae ndipo baadhi viongozi wa wanafunzi walipopitisha karatasi zilizotaka wote wenye kutaka kazi serikali baada ya kuhitimu waorodheshe majina yao kwa ajili waziri mkuu kuyaona na hatimaye kupatiwa ajira. “Nimeshangaa wenzangu kuniambia kwamba jina langu limesemwa kati ya majina ya wananchama wa CCM 700 waliopokea kadi kwenye uzinduzi wa tawi pale Kihesa”, alisema mwanafunzi mmoja. Katika tukio hilo, waziri mkuu alitoa kadi kwa wanavyuo 700 hata hivyo ni wachache ndio waliojitokeza na kadi zilichukuliwa kwa niaba na wanachuo waliokuwepo siku hiyo. Kwa mujibu wa watu walio karibu na Waziri Mkuu Pinda, hii ni hatua ya awali katika mkakati kabambe wa kuweka mizizi ndani ya chama. Hata hivyo, wengine wameshaanza kulaumu kwamba hii ni hatua ya mwanzo ya Pinda kupindisha madaraka yake.

Chanzo: Paparazi Muwazi, Safarini Mbeya na Iringa

safari njema.
 
propaganda

Mtu wa Pwani ipi ni propaganda ndugu .Fafanua .Ipi ni propaganda ya kusema wanafunzi 700 wajiunga CCM kumbe ni wachache tu ama kusema ukwlei wa tukio ? Ipi ni propaganda na hata kuvunja sheria kumwandikisha mwanafunzi jina na yeye akiwa hajui ila anaambiw ajina lime enda kwa Waziri mkuu ili wapate kazi ?

Hivi si kweli kwamba CCM they have been doing this for ages ? Kuingia kwa mashushu kuhoji watu siwezi kukataa maana ndiyo njia za CCM hizo.Watishieni wakome ili tupate response nzuri .Watisheni wasije wakaja juu against Waziri mkuu wakati wakiwa anahutubia .Hii ni kawaida kwa CCM.

Muulize yule mtoto mdogo Ukerewe aliye muuliza maswali Lowasa kilimpata nini .Muulize yuke mzee wa Mbeya aliyehoji matumizi ya pesa za sekondary kakutwa na kitu gani .
 
Tuwe waangalifu kwenye malalamiko.

Once a person falls under the protection of the PSU, it is a 24 hr job. whether he goes to play soccer, swim, harusini, kwa mademu blah blah the govt will provide him/her with all necessary protection including vingora, magari, walinzi.

Now, kwenye nchi zilizoendelea sana kuna portion flani ya cost ya mtu mwenyewe kulipa back kama anakwenda kwenye mambo ya politics ie Pinda peke yake inabidi alipe gharama za usafiri kwenda kwenye huo mkutano kwa cost za bongo taxi umbali huo ni kama buku tano tu. Gharama za walinzi, magari hizo ni za state.
 
Mkuu Pinda.........mbona unaniangusha aisee!!

......Hivi hawa wanafunzi kweli walidhani kazi serikalini zinapatikana kwa kuandikisha majina na kupelekwa kwa waziri Mkuu........hawa ndio wanafunzi wa chuo kikuu!!!.....dahh hii kali!
 
moelex23,

Mkuu unaweza kutupa mfano ktk hili maanake sidhani kama campain za chama zinahusiana na serikali kuu hata kama Clinton ama Obama ni ma seneta..naweza kuwa wrong lakini itakuwa vizuri kama utaweza kunipa mfano unaolingana na kesi kama hii.
Swala la ufunguzi wa tawi la chama ni nje kabisa ya madaraka aliyopewa kama waziri mkuu..Je kweli anaweza kwenda Ukerewe kufungua tawi la Chadema akiwa kama waziri mkuu? na gharama zikalipwa na serikali!
 
Mifano iko mingi sana mkuu.

Kama PM wa Canada Stephen Harper akienda kwenye mikutano ya chama chake Province yoyote, serikali inabeba gharama zote za kumsafirisha na kumprotect. Yeye watamcharge cost yake ya first class ticket price kwenye ndege basi, lakini gharama zingine nchi inabeba.

George Bush anavyoenda Crawford kupumzika au hata Maine kumwona Baba yake, bado Airforce One, Marine One zinaendelea kutumika kwake na familia nzima.

Ni protocol tu ndugu yangu.
 
Mkuu Pinda.........mbona unaniangusha aisee!!

......Hivi hawa wanafunzi kweli walidhani kazi serikalini zinapatikana kwa kuandikisha majina na kupelekwa kwa waziri Mkuu........hawa ndio wanafunzi wa chuo kikuu!!!.....dahh hii kali!
labda alikuwa nafanya personal research ya kuona wasomi wana mtizamo gani kuhusu kufanya kazi serikalini!!!. ha ha ha
 
mi naona mnahangaika bure tu, kiongozi si kuwa na sura ya ukali.
kiongozi ni wito...
kiongozi matendo...
kiongozi ujasiri...
huyo pinda jamani hana jipya oooh!
 
Nawashukuru sana wanaJF. Nilikuwa kijijini sana niliposikia habari hii ya Pinda. Nasikia kuna Tawi alilolifungua ambalo jengo lake limejengwa na mfanyabiashara mmoja wa Iringa (naomba nikosolewe maana radio ilikuwa haisikiki vizuri). Kama ni hivyo kweli, basi Pinda ameanza kupinda mapema, maana hao wanaoifadhili CCM wana malengo yao ya mbele ya kujinufaisha kupitia CCM. Pinda, kuwa makini vinginevyo watanzania watakata tamaa mapema kwako.
Kumbuka hadithi ya Vyura majini na jiw lillilotupwa. Lilipopiga maji, vyura wote walinyamaza, lakini baada ya muda chura mmoja alijitokeza na kutoa sauti kidogo; alipoona jiwe halikujitingisha, alitokea mwingine akafanya hivyohivyo. Baadae Vyura wote walitoka na kupiga kelele bila woga na hatimae wakalikalia lile jiwe na kupiga kelele wakiwa juu yake. Angalia, Pinda, usiwe kama hilo jiwe, maana mafisadi ndio kama hao vyura.
 
tatizo viongozi wetu hawajipi muda wa kutafakari mambo kabla ya kuamua wanakurupuka tu then wanaonekana wamechemka...Pole Pinda lakini ndio hivyo wapendwa disadvatage ya chama kushika dola wakati mwingine mambo huwa hivyo....
 
Huyu asipoangalia sio atapindisha bali atakata kona kabisa au asipopindisha anaweza akalielekeza gurudumu la maendeleo huko huko liliko elekea hapo ndio kindende ,maana kama kuna mti haya kama kuna mlima haya ila kama kuna bonde ndio hakuna msali mtume ni kupinduka na kupindukia ,tatizo ambalo wengi hatulijui hatuna taarifa akiendesha au akiendeshwa maana wakati mwengine hata abiria anatamani kuendesha gari na akipata dereva aliekuwa hajali anaweza kupewa gari kuendesha kama maneno yalimteka dereva ,si hasha mkasikia Pinda akisema alikuwa hajui chochote wakati anateuliwa alikuwa kijijini akilima mboga mboga mara akasikia akiambiwa kuna simu yake!!!
 
He is a leader provided for by the constitution.. and as long as it is with in reason he has a right to undertake in his party's functions na State imlinde na kumgahramia... That is the convention.. Acheni kulalamikia vitu visivyo na msingi.. Ingekuwa kanenda China kwenye shuhuli za chama then u can say that serikali isigharamie.. lakini he was already in the vicinity...
 
Sijaona baya la Mh Pinda kuhusu hili, hivi ulidhani Pinda arudi Dar na kuchukua gari lake binafsi arudi tena Iringa kufungua ofisi hizo kisa ni kuchanganya mambo. Tumuangalie Pinda kwa mambo mengine si hili. Kisha kuhusu ahadi ya ajira yawezekana si yeye aliyeagiza ni wapambe kutaka kuwapa hamasa vijana kumlaki Mzee positively. Mapema mno kumlaumu Pinda.
 
Inawezekana Masumbuka akasumbuka kweli. O lolo .Kisa ni jina au ..lololo. Sijui Pinda atapindisha au atapindua. Lolo lo.
 
Hotuba ya Mh. Pinda kulishukuru Bunge letu Tukufu kwa kumthibitisha kwenye nafasi hii aliyonayo sasa pamoja na mambo mengine aliwataja baadhi ya "Walimu" wake katika siasa na utumishi serikalini ambao ni Chenge, Lowassa, Mkapa,...Binafsi sitarajii utendaji wake uwe tofauti na hao. Tuna kazi kweli WaTz.
 
Back
Top Bottom