Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Pinda aanza kupindisha madaraka yake
Katika kile kinachoelezwa kama kufuata nyayo za mtangulizi wake Bwana Lowassa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameanza kutumia fedha za serikali kujijenga uhalali katika chama. Waziri Mkuu tayari ameshaanza kuwapa hisani za aina mbalimbali viongozi mbalimbali wa CCM. Kadhalika, ameshaanza kutumia kofia yake kufanya kazi za CCM ili kujiweka karibu zaidi na viongozi wa hivi karibuni. Tukio la hivi karibuni la Bwana Pinda kutumia msafara wa kiserikali kwenda Iringa mara baada ya Mei Mosi kufungua tawi la CCM limeelezwa na baadhi ya wadadisi wa mambo kuwa sehemu ya mkakati huo. Hata hivyo, tayari viongozi kadhaa wa upinzani mkoani Iringa wameanza kulaumu kitendo hicho kuwa kinakidhana na Sheria ya Maadili ya Watumishi wa Umma. Waziri Mkuu kama kiongozi wa umma anapaswa kufanya kazi zake bila kubagua watu kiitikadi, kitendo cha Bwana Pinda kutumia magari ya serikali, mafuta ya serikali na watendaji wa serikali kwenda kujenga chama chake. Na kuwabagua wanavyuo wenye itikadi tofauti katika hotuba yake hakipaswi kupita bila kukemewa, alisema Mhadhiri mmoja wa chuo cha Tumaini ambaye hakupenda kutwajwa jina lake. Aidha, wanafunzi mbalimbali wa chuo hicho, wamesema kabla ya waziri mkuu kuja, wapo watu wanoasadikiwa kuwa wanausalama walifika katika chuo hicho na kufanya mahojiano na baadhi ya wanafunzi wanaoelekea kuwa mstari wa mbele kuunga mkono upinzani. Haijajulikana mara moja nini ilikuwa ajenda ya mazungumzo hayo. Hata hivyo, baadae ndipo baadhi viongozi wa wanafunzi walipopitisha karatasi zilizotaka wote wenye kutaka kazi serikali baada ya kuhitimu waorodheshe majina yao kwa ajili waziri mkuu kuyaona na hatimaye kupatiwa ajira. Nimeshangaa wenzangu kuniambia kwamba jina langu limesemwa kati ya majina ya wananchama wa CCM 700 waliopokea kadi kwenye uzinduzi wa tawi pale Kihesa, alisema mwanafunzi mmoja. Katika tukio hilo, waziri mkuu alitoa kadi kwa wanavyuo 700 hata hivyo ni wachache ndio waliojitokeza na kadi zilichukuliwa kwa niaba na wanachuo waliokuwepo siku hiyo. Kwa mujibu wa watu walio karibu na Waziri Mkuu Pinda, hii ni hatua ya awali katika mkakati kabambe wa kuweka mizizi ndani ya chama. Hata hivyo, wengine wameshaanza kulaumu kwamba hii ni hatua ya mwanzo ya Pinda kupindisha madaraka yake.
Chanzo: Paparazi Muwazi, Safarini Mbeya na Iringa