Pinda - a clueless PM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda - a clueless PM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ZeMarcopolo, Jun 3, 2009.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Pinda: Wawekezaji kwenye kilimo watapewa ardhi

  Na Joseph Mwendapole
  3rd June 2009


  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema serikali itawapa ardhi wawekezaji wa kigeni wanaotaka kuwekeza kwenye kilimo nchini bila kujali kelele za wananchi.

  Vile vile, amesema ingawa yeye ni Waziri Mkuu, lakini baba yake ambaye ni mkulima, bado ni fukara hali inayomfanya ajisikie kuwa ana deni la kuinua sekta ya kilimo nchini.

  Aliyasema hayo juzi jioni wakati akizungumza kwenye chakula cha jioni kilichoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafasi (TPSF), kwa ajili ya kubadilishana mawazo na wafanyabiashara wa ndani.

  Wafanyabiashara hao ni wale wanaohudhuria mkutano wa siku mbili ulioanza jana jijini Dar es Salaam unaoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.

  Pinda alisema Tanzania ina ardhi nzuri na yenye rutuba kwa ajili ya kilimo ambayo haitumiki kwa uzalishaji lakini wanapopewa wawekezaji kuitumia wananchi huanza kulalamika.

  Alisema Tanzania inakadiriwa kuwa na hekari zaidi ya milioni 40 ambazo zinafaa kwa kilimo lakini mpaka sasa watu wamebaki kuitizama bila kuifanyia chochote.

  Aliongeza kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyofanya miujiza katika mapinduzi ya kilimo na mifugo na kwamba kilichofanyika ni kuwa makini na kufanya tafiti za kina katika kuendeleza sekta hizo.

  Aliongeza kuwa serikali sasa lazima ifanye jambo la kusogeza mbele sekta ya kilimo na kwamba isipoweza kufanya hivyo sasa ni dhahiri haitakuja kuweza tena.

  Mkurugenzi wa TPSF, Dk. Evans Rweikiza na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Ester Mkwizu, walisema sekta hiyo imekuwa ikikua siku hadi siku na waliomba ushirikiano wa serikali katika kukamilisha mipango yake.


  Source:NIPASHE
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mzee wa Noblesse Oblige,

  Hizi reporting ndizo Mzee Dilunga anaziita "incredible" kwa sababu article nzima haina direct quote hata moja.

  Essentially tunachosoma hapa ni interpretation ya mwandishi kuhusu alichosema Pinda, hatujawekewa maneno aliyosema Pinda ambayo yanaweza kuwa tofauti sana na kilichoripotiwa hapa.
   
 3. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Haha ahahahahahahahhahahahahaa aa

  Blue Ray, hebu imagine that.

  Can you believe kuna maelfu ya Watanzania wenzetu leo watasoma hiyo ripoti ya NIPASHE bila ku question veracity ya huyo mwandishi. Yani hawatajua ya Mwandishi yapi, ya Pinda yapi.

  Kweli unaandika habari Pinda kasema watatoa ardhi "bila kujali wananchi." Na wakuu wanaamini!
   
  Last edited: Jun 3, 2009
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Jaribu kuwa muungwana kidogo..^^^
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kwa nini serikali isiwape motisha Watz wazawa ili wafungue mashamba makubwa kilimo cha kisasa cha umwagiliaji??

  kwa nini iwe lazima hoja wa wageni?
   
 6. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Wazee wa Jamvini

  Imeshapindishwa mara mbili...'Clueless'-'Wawekezaji wapewe Ardhi'

  Amesema Tanzania kuna rutuba nzuri ya Ardhi...
  Amesema Asilimia 40 haitumiki...
  Ameongeza kwa kuashiria na kuipa changamoto Serikali wafanye sasa, kwani -kwa mtazamo wake- Hiki kitakuwa na gharama kubwa na Serikali kushindwa.Au?

  Sasa Ze-Marcopolo Unadiriki kudai kuwa Waziri mkuu yuko Clueless?

  Kwanini umwingie huyu Waziri Mkuu kibinafsi?
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Nilichojaribu kufanya ni kusummarize ujumbe uliotolewa na gazeti kwa maneno machache.
   
 8. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wrong answer!!
  Why would you do that? Kuna threads watu wanafanya copy paste hapa JF unafikiri hawana uwezo wa kusummarise? Its because they dont want to misinform the public!!

  Unapotoa habari ambayo umeiconclude kwamba PM is clueless we need to know exact words used and not interpretation by your own understandigs!! Ze marco kwa hili naona haujatenda haki kabisa!
   
 9. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Why is Pinda "clueless"?
   
 10. A

  August_Shao Senior Member

  #10
  Jun 4, 2009
  Joined: Nov 23, 2007
  Messages: 158
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
 11. M

  Msuruhishi Member

  #11
  Jun 4, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Kimsingi watu hawalalamiki kuhusu wawekezaji kuja nchini na kuwekeza kwenye kilimo. Watanzania wasingependa kuona kilichotokea kwenye uwekezaji katika sekta ya madini kikijirudia. Ardhi yote ni rasilmali ya watanzania. Yeyote mwenye uwezo wa kuwekeza katika ardhi hiyo, iwe kwa kuchimba madini au kwa kuendesha kilimo, lazima maslahi ya watanzania yazingatiwe. Hivyo basi, Serikali haina budi kuweka utaratibu utakaokubaliwa na wananchi ili nao wafaidike na uwekezaji huo.

  Tunapinga vikali na tutaendelea kupinga, wawekezaji kutoka nje kupewa ardhi, ati kwa kuwa haina watu wanaoitumia; kwani Watanzania wanaendelea kuzaliana. Yeyote anayetaka kuwekeza kwenye ardhi aelekezwe kuiomba kutoka kwenye kijiji husika na kuwe na mikataba kuhakikisha kuwa kuna mgao wenye uwiano unaoeleweka kati ya mwekezaji na serikali ya kijiji.

  Lakini kwa kuwa ni rahisi serikali za vijiji na za halmashauri za wilaya kurubuniwa na wawekezaji kama ilivyotokea Kisarawe, Mkuranga na kwingineko, Kituo cha Uwekezaji (TIC) kuwa na kitengo maalum cha kusimamia na kuongoza utaratibu wote na kuuratibu. La sivyo tutaishia na mikataba kama ya Karl Peters na machifu wa zamani.

  Nasisitiza, wageni hao wakipewa lease ya ardhii na Serikali Kuu, wataishia kulipa ada ndogo tu ya ardhi na hivyo wananchi hawatafaidika; hata kama nchi itajitosheleza kwa njia nyingine!
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kiongozi anayeamini kuwa ana mamlaka ya kuamia matumizi ya ardhi hata kama wananchi hawakubaliani nayo ni cluesless. Has no clue what trouble he is putting his political carrier into.
  Kiongozi anayejisikia shujaa kutetea watu wa nchi nyingine huku akiwakandia wananchi wake is clueless. Has no clue that foreigners will only praise and smile to local leaders to get what the want.
  Kiongozi anayewalaumu wananchi kwa kutotumia ardhi is clueless. Has no clue that the message sent is that the government has failed to facilitate the use of land.
  I dont see how Zemarcopolo is unfair! Zemarcopolo didnt fabricate the story, its in the news and no statement from Pinda to denounce it.
   
 13. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Ze Marcopolo, you have NOT pointed out the "cluelessness "of Mr Pinda the PM.If any thing to go by, it is your heading that has no direction as to the story you are purporting to host.
  The "cluelessness" can just be in your infertile imagination.
   
 14. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  huyu jamaa anasifiwa ya kuwa mwanasheria mzuri but i cant agree nor deny because he is not that vocal as other members of the party. but what i can tell is that he is not a long term thinker nor wiser for that matter if he came up with that pumba. first before i go any further what do people understand about the Zimbabwe problem, its to do with land that Mugabe allowed the west to invest on it for the benefit off Zimbabwe na maslahi yake mwenyewe kidogo. and once you give these people land its going to be difficult to get it back so are we ready to loose our land for good.

  on the good side yes they will make a good use of it but not for you and me but for themselves and their supermarkets. and getting it back could cause a lot of trouble to ourselves. like i always say viongozi inabidi waulewe umma kama ulivyo na sivyo wanavyofikiria wao watu walivyo au watakua hivyo siku zote. in twenty years time more tanzanians will be educated more will ask questions and more will understand what is patriotism and what it means to be a tanznanian and start to think like tanznanians as whole, care for the intrest of their land. then when this time comes its going to be a problem getting our land back why? a white man has demonstrated this through the suez canal crisis and recently Zimbabwe because he doesnt invest there he takes more of the produce back home., therefore he makes a vital part of his system and he's not going to let it go without putting up a fight. Just investigate more on The Tanznania- Canada wheat project in Bosatu Plains then you'll see what percentage of the wheat goes to canada and what percent we get look at the prices they've set then you'll understand the investment is not for me and you its for their supermarkets at a cheaper price.

  MUngu Ibariki Tanznania
   
  Last edited: Jun 4, 2009
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kinachoshangaza ni pale wanapotokea watu wakaamua habari fulani ni za uongo na fulani ni sahihi, just depending on who is the subject of discussion!
   
 16. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  like i said watu wengi wajua kulalamika na kujua wanataka nini lakini hawajui watapata vipi realistically

  Mungu Ibariki Tanznania
   
 17. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Naona tusichanganye watu kutaka standards za juu katika uandishi na "watu kusema habari fulani za uongo na fulani za kweli". Bottom line ni kwamba ukimaliza kusoma hiyo article unabaki hujui Pinda mwenyewe alisema nini na mwandishi katafsiri vipi maneno ya Pinda, hujui asilimia ngapi ya riporti hii ni distortion ya muandishi na ngapi ni maneno ya Pinda.

  Pinda watu wamemlambast tangu siku ya kwanza anaapishwa kwamba ni box tupu, bila hata kumpa grace period, lakini kwa mujibu wa story hiyo hapo juu, hata kama Pinda kweli kasema utumbo hatuwezi kujua, kwa sababu mwandishi kafanya utumbo mkubwa zaidi kwa kutorekodi verbatim utumbo wa Pinda na kutuletea tuone wenyewe.

  Kuhusu Pinda kukanusha mtu anaweza kusema inawezekana anawaona ma tabloid na anachagua kuchukua the high road na kunyamaza kimya.

  Katika Tanzania ya leo ya ufisadi na rushwa, uzembe na upuuzi wa kila aina unaofanana na huo, kama tunataka kuwa discipline hawa viongozi kitu cha kwanza tunachohitaji sis ni discipline.huwezi kumshambulia Pinda kuwa ni clueless kwa kutumia article iliyo clueless kuhusu kanuni za uandishi wa habari, wewe ndiye utaonekana clueless.

  Mwishowe tutawashika mafisadi redhanded hivi hivi watatufunga magoli kwa technicalities tu.
   
 18. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Apparently, ili article iwe na ujumbe unaoeleweka ni LAZIMA iwe na direct quotes!
   
 19. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Si kwamba ujumbe haueleweki. Ujumbe hauaminiki.

  Huwezi kudai Pinda ni clueless kasema watakodi ardhi ya nchi "bila kujali kelele za wananchi." Hiyo ni tafsiri yako wewe na mwandishi wako wewe. Weka maneno yake nione mwenyewe alichotamka yeye Pinda neno kwa neno.

  Vinginevyo mmetunga.
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  vinginevyo wametunga...
   
Loading...