Pima uzazi kabla ya ndoa, kuna mateso ukigundua sio mzima viungo vya uzazi

Hii mada kwangu imekuja kipindi muafaka naomba unishauri katika changamoto niliyokumbana nayo.

Ni hivi nina mchumba wangu ambaye nimeshatoa mahari tangu January na tarehe ya ndoa ikapangwa Ila bahati mbaya kabla ya tarehe nikapata Safari ya dharura kwa miezi 4 hivyo ikabidi nihairishe ndoa mpaka nitakaporudi.

Niliporudi mwezi huu wa tano nikataka niendelee na michakato ya ndoa Ila Sasa majuzi huyo mchumba wangu nilipompigia simu aliniambia yupo hospital anapata matibabu,sikujua shida yake but alinijibu kiuno Ila kwa mujibu wake Dr alimuuliza kuhusu umri akamjibu 30yrs ndoa akamjibu ameolewa,watoto akamjibu hana.Dr akamshauri wapime hormone na ultra sound.Ila Sasa ukweli ni kwamba huyu mwanamke anaishi kwao yaan kwa wazazi namimi sijawahi kudai kuhusu watoto kwa maana nilitaka wa ndani ya ndoa.
Kesho yake akapewa majibu kuwa hormones ziko sawa Ila mayai hayakomai ndo maana hana mtoto,hivyo anatakiwa kufanyiwa operation ndipo ataweza kuzaa na akampangia na tarehe kabisa.

Mchumba aliponipa mrejesho huu nilimuuliza maswali mengi sana mojawapo ni kitu gani kilimfanya aone awezi kuzaa wakati Mimi sijawahi ata kumuuliza?Pili kwanini akubali kufanya operation wakati atujui Kama anayo shida kwani Mimi mchumba wake sijawah kupanga kutafuta watoto tukakosa?
Akasema yeye anaenda kufanya operation hiyo tarehe,na haya yote wazazi wake hawajui wananipigia tu kupitia kwa mshenga kwamba michakato ikoje binafsi nilitaka kusitisha mpka nipate muafaka wa Hilo kwani Nina hofu anajijua au Kuna kitu anajijua .
Nipe maoni yako nifanyaje
Tafuteni kwanza mtoto ndo mfunge ndoa.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Iliniuma sana ,Shangazi angu aliolewa 2016 na jamaa mmoja hivi wa pwani ,nilikuwa najua fika shangazi hana kizazi , nilijaribu kufanya mbinu zote nimsanue jamaa lakini ilishindikana wakafunga ndoa mwezi wa 11 mwaka 2016 ,mpaka Leo hakuna mtoto kabisa maana shangazi alikuwa bingwa sana wa kutoa mimba.

Shangaz alivokuwa anakuja na jamaa kijijini alikuwa hamwachii upepo hata kidogo mtu uongee nae kabisa
Mkuu ulikuwa unataka umchomee shangaz..
 
Back
Top Bottom