Pima hoja za Mnyika na Nape juu ya shutuma za mauwaji ya wana-CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pima hoja za Mnyika na Nape juu ya shutuma za mauwaji ya wana-CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, May 10, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilielezea
  kile ilichoeleza kuwa ni kutishwa na wimbi la mauaji yanayotishia
  amani ya nchi kikidai kuwa jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika
  wilaya ya Igunga peke yake.

  Madai hayo ya CHADEMA, pamoja na wanachama wengine na mashabiki wao,
  yalitolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ambaye alidai
  kuwa mauaji hayo yana mkono wa serikali ya CCM, ambayo kwa madai yao
  imeona wazi kuwa upepo wa kisiasa umekiendea vibaya na sasa kinataka
  kujiimarisha katika utawala kwa kuua watu wanaoipinga.

  Akifungua kikao cha Baraza Kuu la chama hicho jijini Dar es Salaam
  Aprili 29 mwaku huu mwenyekiti huyo alifafanua kuwa mbali na kuuawa
  kwa watu wanne kwa pamoja na juzi kifo cha mwenyekiti wao wa tawi huko
  Arumeru mkoani Arusha, jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika
  wilaya ya Igunga peke yake tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa
  jimbo hilo mwaka jana.

  Mbowe katika maelezo yake alijaribu katika maeneo kadhaa kuihusisha
  CCM na au serikali yake katika matukio kadhaa yaliyowakabili baadhi ya
  wanachama na viongozi wa Chadema katika maeneo mbalimbali nchini
  likiwemo lile la Mbunge Highness Kiwia ambaye Suala lake bado Lipo
  mikononi mwa vyombo Vya dola likishughulikiwa.

  Katika sehemu kubwa ya maelezo ya Ndg. Mbowe amejitahidi kuonesha kuwa
  mauaji yote yaliyoikabili na yatakayokuwa yakiikabili Chadema kupitia
  wafuasi wake yanafanyika kisiasa, Jambo ambalo ni la uzushi, kwani
  Halina ushahidi wa kisheria hata kimazingira, wa Moja kwa Moja
  unaoondosha ujinai au makosa hayo, na kuwa ni makosa yanayolenga
  muktadha wa kisiasa.

  Huku akitaka kuuaminisha umma kuwa huo ndio ukweli, Ndg. Mbowe
  amesisitiza kuwa hilo lime kuwa likitekelezwa na CCM kwa lengo la
  kuwatisha wananchi kujiunga na chama hicho hoja ambayo haina msingi
  wowote wa kiutafiti.

  Hivyo CCM kwa kutambua kuwa Suala la mauaji linabeba Kosa la jinai, na
  kwa kuwa Ndg. Mbowe ameshutumu Moja kwa Moja CCM na serikali yake
  kuihusisha na mauaji hayo, ni vema sasa nasi tukatoa msimamo wetu
  dhidi ya tuhuma, hiyo.

  Kwanza, si busara hata kidogo kuihusisha CCM katika matukio hayo,
  kwani uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola umeshindwa mpaka sasa
  kuhusisha matukio hayo na siasa, badala ya kuyahusisha na makosa ya
  jinai ambayo hufanywa na watu kwa malengo tofauti na yale ambayo Ndg.
  Mbowe anataka kuwaaminisha watu.

  Pili, CCM haijawai, haiwezi, na haitakuja fanya jambo lolote lenye
  lengo la kuvuruga Amani na Usalama wenye utulivu ndani ya taifa letu,
  hivyo uzushi na usingiziaji uliofanywa na Mtu Kama Ndg. Mbowe, si vema
  kuuacha kimya, badala yake nimetumia wasaa Huu muhimu Kujibu, na kutoa
  ufafanuzi ili Kuupa umma wa watanzania habari sahihi.

  Ni aibu kwa Chama kama Chadema kujitahidi kwa nguvu zote kujaribu
  kuficha ukweli wa mauaji yanayotoa roho za watanzania wenzetu kwa
  kuyapa sura ya kisiasa. Hizi ni juhudi za makusudi za kutaka kuficha
  ukweli wa kinachotokea.

  Ni aibu kwa chama kama Chadema kujaribu kutumia mauaji mabaya kama
  haya kutafuta mtaji wa kisiasa. Huku ni kuonyesha jinsi gani
  wamefilisika kisiasa mpaka wanafikia mahali pa kuamini kuwa wanaweza
  kutumia chochote kama mtaji wa kisiasa, vikiwemo vifo vya watanzania
  wenzetu. Huku si kufilisika tu ila kwakweli ni unyama unaotakiwa
  kulaaniwa na kila muungwana.

  Mwisho.

  Imetolewa na:
  Nape Moses Nnauye
  Chama Cha Mapinduzi
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM

  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

  Taarifa hii ya CCM inadhihirisha masuala kadhaa ya msingi;

  mosi, kwamba chama legelege huzaa serikali legelege. Ulegelege wa serikali katika kushughulikia masuala ya mauji ya raia ni matokeo ya CCM kushindwa kuonyesha kwa vitendo inavyothamini utu na uhai wa binadamu. CCM isingekuwa legelege ingeiwezesha serikali inayoongozwa na wanachama wake kufanya uchunguzi wa vifo vyenye utata (inquest) kupitia mahakama maalum (coronary court).

  Pili, kwamba CCM imekosa uhalali wa kimaadili wa kukumea vitendo hivyo na kuchukua hatua zinazostahili kwa kuwa wanazungumza maneno matupu ya amani na utulivu huku viongozi na wanachama wake wanafanya matendo ya vurugu na umwahaji damu. Nape anasema hakuna ushahidi wa kimazingira, wakati anajua kwamba mpaka sasa kuna majalada yamefunguliwa dhidi ya viongozi wa CCM Kiteto, Busanda, Biharamulo kwa vitendo vya umwagaji damu kwenye kampeni za chaguzi ndogo. CCM inajua pia kifo cha kiongozi wa CHADEMA Arumeru mpaka sasa kuna viongozi wake wamekamatwa na kuhojiwa na polisi. CCM inajua kuwa makada wake wametajwa kwa majina kwenye tukio la kukatwa mapanga kwa wabunge wa CHADEMA Mwanza tukio ambalo mashahidi wameeleza kuwa hata Askari polisi wameshuhudia na kuachia litokee.

  Na CCM inajua kilichomo mpaka sasa kwenye jalada la uchunguzi la mauji ya Mbwana Masudi kule Igunga. Orodha ni ndefu ya watu na matukio, hivyo taarifa ya CCM ya kutoa kanusho la ujumla ni ishara ya kufisha ukweli na kugeuza mjadala suala ambalo halitafanikiwa, tamko hili la Nape ni kama Al Sahaf kule Iraq, CCM ikae vikao vyake vya kikatiba itoe maamuzi ya chama hicho kuhusu suala hili la umwagaji damu na mauaji ambayo yanatuhumiwa kufanywa na viongozi wa chama hicho pamoja na vyombo vya dola sio kwa wanaCHADEMA tu bali hata kwa wananchi wa kawaida. Inapaswa kuwa kutoka kauli ya amiri jeshi mkuu na kiongozi wa serikali Rais Jakaya Kikwete. Tunachohitaji kusikia ni hatua kuchukuliwa kwa wahusika kama kweli hawajatumwa na CCM na serikali na sio propaganda.

  Tatu, imekuwa ni kawaida ya CCM kuanza kwa kuukana ukweli unapotolewa lakini hatimaye hukiri sehemu ya ukweli huo kama zilivyokuwa kauli za CCM mara baada ya kutolewa hadharani kwa Orodha ya Mafisadi. Walianza kwa kanusho lakini hatimaye wakakubali kuna ufisadi ila wakadai mafisadi ni baadhi ya wanachama na sio chama, lakini mpaka leo wameshindwa kujivua gamba kama walivyodai. Hata hili, wameanza kwa kukukana baadaye wanatesema ni la wanachama wachache waliotenda jinai bila kutumwa na chama, lakini ukweli utabaki kwamba haiwezekani matendo yote haya yakajirudiarudia bila vyombo vya ulinzi na usalama kufahamu. Na tunazo taarifa juu ya mikakati ya CCM ya vurugu na vikundi wanavyotumia kufanya uharamia, na yapo majalada ambayo yamefunguliwa polisi. CCM inahitaji ushahidi gani zaidi toka kwa CHADEMA na umma?

  John Mnyika
   
 2. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kujibizana na nape au ccm kwa wakati huu ni kupoteza rasilimali mda na nguvu.tuwasubiri 2015
   
 3. Eliza wa Tegeta

  Eliza wa Tegeta JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vuvuzela Nape anatakiwa ajifunze !!!!
  Sio kila kitu anatolea tamko kama kurugenzi ya mawasiliano ya kukanusha ya ikulu
   
 4. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,316
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  Hapa sasa ndo tunapata uhakika kwanini watu wa Ubungo walimchagua Mnyika na kumwacha huyu Nape, soma maandishi yao then utaona nani kichwa hapo!
   
 5. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  mouddymtoi ni ndefu sana ntaipitia taratibu ila kifupi tu huwezi kuwalinganisha Nape na Mnyika kwani sera za vyama vyao zinatofautiana sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Tumeumbwa tofauti jama, Mnyika ni kichwa kweli!
   
 7. M

  MAKAWANI Senior Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tutawahukumu kwa matendo yao na si maneno yao!
   
 8. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kumlinganisha Mnyika na Nape ni sawa na kulinganisha mlima Kilimanjaro na kichuguu. Uliangalia maelezo ya Mnyika ni mafupi, ya kueleweka na yenye mantiki wakati maelezo ya Nape ni marefu tu lakini hayaeleweki wala hayana mantiki.
   
 9. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Hivi nani alisoma na Nape o level alipata div gani na A level alipata nini? Manaake msije mkawa mnaelezea mambo magumu!
   
 10. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #10
  May 10, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Inawezekana alisoma shule nzuri na kafaulu vizuri lakini kwa kuwa ameamua kujitoa fahamu na kumeza utambi mchafu lazima atoe uchafu, maneno marahisi ya kumuelezea Nape unaweza kuyasoma kwenye michango ya wadau wengi jinsi wanavyomuelezea. Kuna mchangiaji mmoja aliwahi kusema kuwa "Kinachoingia kwenye uchafu ni uchafu"
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,478
  Trophy Points: 280
  Unalinganisha Petrol na mafuta ya taa mkuu.
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  May 10, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Hoja zote mbili yaani ya Nape na ya Myika zina mashiko....... Ya Nape, si vema kuwaaminisha watu hata mwana CDM akiiba na kuuwawa na rai wema basi ameuwawa na CCM kwakuwa ni mwana CDM Ya Mnyika, ni kweli CCM imeshindwa wajibu wake kama mtawala
   
 13. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama Nape uwezo wako wa kuelezea mambo ndiyo huu basi ujue kuwa unathibitisha kile ambacho unadhani unakikana. Kwa kifupi ninapenda nichambue maelezo ya Nape kama nnilivyonukuu kama ifuatavyo:

   
 14. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli Nape ni senior state Vuvuzela kama mwana Jf mmoja aliyesema kwenye post moja humu jamvini,haiwekekani kama kuna watu hadi wamefunguliwa majalada na ni wana ccm,bado yeye anakanusha,sitashangaa siku akila kipigo toka kwa ... then akakana sijapigwa huku akiwa na manundu kibao!
  Asubuhi njema wanabodi
   
 15. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  mbona nape hajaweka wazi ukwel upi cdm wanaufcha? Ni nafas ipi wanataka kuitumia kama mtaj wa kisiasa? Au ndo habari za kishirikina za baba kumuua mwanae apate mali? Kama ukwel anao si autoe tuufaham.
   
 16. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  We Ndg. ni wa siku nyingi sana humu JF tangu 2009, sasa kama michango yote tangu wakati huo ndiyo hii basi huna mchango muhimu humu JF hivi mauaji yote yaliyo fanyika yanaendana na Uharifu? kumbuka Igunga wakala wa CDM alitekwa na kuokotwa baada ya siku kadhaa akiwa mfu, Mwenyekiti wa CDM huko Arumeru amachinjwa, Kibaha mtu aliyekuwa CCM baada ya kujiunga na CUF akauawa pia ukumbuke na wale vijana 4 wa Arumeru hawa nawafanisha na tukio la Igunga sasa swali la kujiuliza mbona CCM hawauawi?
   
 17. u

  uwemba1 JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 755
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
  U r wrong kwanza kuongea ni tendo,
  Pili, Nassary anahukumiwa Kwa maneno yake si matendo
  So maneno na matendo daima ni ndugu
   
 18. P

  Paul S.S Verified User

  #18
  May 10, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  kibogo najua unapenda kusikia tu mtu akiipamba CDM au akiiponda CCM basi........kuna wengine hatuangalii mambo haya kwa jicho la upofu wa mahaba ya vyama., inawezekana hayo mauji yapo kweli lakini si sahihi pia kusema kila mauji yaliotajwa ya mwana CDM ni mbinu ya CCM kuwatisha eti wananchi wasiingie upinzani........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,834
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Naona Nape Mwenyewe Hajui AU anaficha Ukweli!! Najua kuna Vijana wapo Trained kwa kazi Hizi!! Wala Hawapo kwenye green Guard!! Ila ni Vijana wa kiuni ambao wanapatikana maeneo ya Ubungo Maziwa Wakijifanya kufanya Kazi nyingine Huku kwenye Chaguzi wakienda Kutimiza Azma Zao!!
   
 20. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watakuwa wameuwa wangapi?
   
Loading...