Pima DNA kwa njia ya asili yenye ukweli kwa zaidi ya 90%

mjusilizard

JF-Expert Member
Nov 7, 2019
923
1,586
HUU NDIYO UKWELI WA DNA YA KIUTAMADUNI

Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm ) linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.

Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha yaendelee.

Wamesema kwamba hata iweje Mtoto wako wa damu yako kabisa akizaliwa ni lazima tu alama zilizopo katika Mikono yake zitafanana na Wewe na wala haziongopi. Na ndipo hawa akina Babu na Bibi wakaenda mbele na kusema kuwa hiyo mbinu ndiyo iliweza kuwafanya wao huko nyuma wasiwe wasaliti na wawe wakweli kwani katika Makabila mengi hiyo mbinu ilishasambazwa na iliendelea kutumika.

Na ili kulithibitisha hili ndiyo maana Bibi yoyote au Babu akipelekewa Mjukuu akimbeba tu kisirisiri atawahi kuuangalia mkono wa Mjukuu wake na hasa vidole vyake kisha atajua kuwa Mtoto wao kazalisha au kazalishiwa na wenzake.

MWISHO
Andiko langu hili kamwe halina kusudio la kuharibu Mahusiano yoyote yale bali naomba tulitumie tu kama sehemu ya kujipatia maarifa ambayo nina amini wengi wetu ( Vijana na Mabinti ) wa leo tulikuwa hatuna na kama itatokea umekuta umezalishiwa ( umebambikiwa ) basi ninachokuomba tu samehe, piga moyo konde na songa mbele na ule msemo wa Wahenga kuwa siku zote Kitanda hakizai haramu.

Kwa Dada zangu Wapendwa najua huu uzi utawaudhi na kuwauma ila tuvumiliane tu na pengine huu uzi unaweza ukawa msaada mkubwa sana Kwenu hasa katika kuwafanya mbadilike na muache kuwabambikia Wanaume zenu Watoto ambao siyo wao kwani hata Takwimu za mara ya mwisho za Mkemia Mkuu wa Serikali zinasema kuwa 49% ya Wanaume wa Kitanzania wanalea Watoto wasio wao
( wamebambikiwa ) hivyo mtusamehe na mtuonee huruma sisi Wanaume.
 
Napenda utamaduni wa kwetu. Ukishamlipia mwanamke mahari, watotot wote atakaowazaa ni wako.
Hata kama wanafanana na jirani zako.
Unaambiwa kibarua akifanyakazi kwa shamba la jirani ,mazao ni ya nani
Ndo maana kesi za ukatili wa watoto haziishi. Eti mtoto kapoteza shilingi mia, anakatwa mkono.
 
Mtoto anazaliwa kwa kushirikiana baba na mama, endapo akafanana na mama yake inakuwaje? Inakuwaje kwa watu wa imani tunaosema ulimwenguni kote tumetokana na baba na mama moja, mikono si ingefanana sababu kila mtoto angefanana na baba yake, babu hivyo hivyo na kuendelea. Ndio maana siku hizi kuna DNA nayo mnafanana kwa percent kadhaa tu. Achana na magumu ya mababu mengi yasikuwa na ushahidi.
 
Unajua hata maana ya DNA?!!
HUU NDIYO UKWELI WA DNA YA KIUTAMADUNI

Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm ) linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.

Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha yaendelee.

Wamesema kwamba hata iweje Mtoto wako wa damu yako kabisa akizaliwa ni lazima tu alama zilizopo katika Mikono yake zitafanana na Wewe na wala haziongopi. Na ndipo hawa akina Babu na Bibi wakaenda mbele na kusema kuwa hiyo mbinu ndiyo iliweza kuwafanya wao huko nyuma wasiwe wasaliti na wawe wakweli kwani katika Makabila mengi hiyo mbinu ilishasambazwa na iliendelea kutumika.

Na ili kulithibitisha hili ndiyo maana Bibi yoyote au Babu akipelekewa Mjukuu akimbeba tu kisirisiri atawahi kuuangalia mkono wa Mjukuu wake na hasa vidole vyake kisha atajua kuwa Mtoto wao kazalisha au kazalishiwa na wenzake.

MWISHO
Andiko langu hili kamwe halina kusudio la kuharibu Mahusiano yoyote yale bali naomba tulitumie tu kama sehemu ya kujipatia maarifa ambayo nina amini wengi wetu ( Vijana na Mabinti ) wa leo tulikuwa hatuna na kama itatokea umekuta umezalishiwa ( umebambikiwa ) basi ninachokuomba tu samehe, piga moyo konde na songa mbele na ule msemo wa Wahenga kuwa siku zote Kitanda hakizai haramu.

Kwa Dada zangu Wapendwa najua huu uzi utawaudhi na kuwauma ila tuvumiliane tu na pengine huu uzi unaweza ukawa msaada mkubwa sana Kwenu hasa katika kuwafanya mbadilike na muache kuwabambikia Wanaume zenu Watoto ambao siyo wao kwani hata Takwimu za mara ya mwisho za Mkemia Mkuu wa Serikali zinasema kuwa 49% ya Wanaume wa Kitanzania wanalea Watoto wasio wao
( wamebambikiwa ) hivyo mtusamehe na mtuonee huruma sisi Wanaume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom