Pilau


J

Jocasta

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Messages
215
Likes
146
Points
60
J

Jocasta

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2014
215 146 60
Wanajukwaa naomba mwenye uelewa juu ya mapishi ya pilau anielekeze pls
 
Northman

Northman

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2016
Messages
710
Likes
935
Points
180
Northman

Northman

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2016
710 935 180
Mimi sijui wanavyopika lakini huwa wanaweka mchele then sijui kinachoendelea, lakini badae inatokea pilau.
 
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
12,291
Likes
25,749
Points
280
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
12,291 25,749 280
Wanajukwaa naomba mwenye uelewa juu ya mapishi ya pilau anielekeze pls
Kuna aina nyingi za upishi wa pilau,kama wasemavyo;mchele mmoja mapishi mengi..lakini muhimu liwe pilau,na mpaka liwe pilau kuna viungo ambavyo ni lazima uwe navyo ili litokee pilau ina maana ukikosa hivyo viungo muhimu basi halitakuwa pilau tena,.
Kuna wanao weka nyanya kwenye pilau lakini hii si lazima sana,ni katika kuongeza tuu ladha lakini haiwezi kubadili chakula chako kisiwe pilau..anyway upishi wa pilau uko hivi;hivi ni viungo vya pilau
●kitunguu saumu,kitunguu maji
●pilipili manga,abdalasini,hiriki,karafuu,pilipili mtama,tangawizi,binzari kidogo
●pilau masala
●karoti na njegele kama utapenda,sio lazima sana
●nyama yoyote ya ng'ombe,kuku,mbuzi n.k
●mchele kiasi kutokana na walaji wako
●viazi mviringo/viazi ulaya
Baada ya kuwa na viungo vyako hivyo vyote hatua inayofuata ni kupika..kwanza utachemsha nyama yako mpaka iive vizuri utaiwekea viungo kidogo kama tangawizi,chumvi,pilipili manga pamoja na soya sauce kidogo kuipa ladha nyama yako..
●nyama ikishaiva utaiweka pembeni pamoja na supu yake ambayo utaitumia kuweka kwenye kupika pilau
●menya viungo vyako kitunguu saumu kitunguu maji pamoja na viazi vichache,osha viazi vitoe kwenye maji weka pembeni,twanga abdalasini,pilipili manga pamoja na hiriki ukimaliza vitoe halafu utwangwe kitunguu saumu pamoja na tangawizi
●osha mchele wako vizuri usiuloweke sana mchele pilau litalegea,osha utoe kwenye maji ukauke/ujichuje maji Ili wakati wa kupika lichambuke vizuuurii
●bandika maji jikoni kwenye sufuria pana yaache yachemke,usipike pilau kwenye sufuria ndogo kwasababu lina vitu vingi litashindwa kuiva vzr kwa nafasi
●maji ya kichemka yaipue,.hapa sasa tutapika kisasa tofauti na upishi wa kizamani wa kuchemsha viungo sisi tutapika kwa kukaanga viungo pamoja na mchele

Hatua ya 1
●bandika sufuria kavu jikoni,likipata moto kidogo weka mafuta ya wastani/kiasi hakikisha yamepata moto,halafu weka vitunguu maji anza kuvikaanga taratibu hadi vibadilike rangi viwe vya brown (usiviunguze pilau litakuwa jeusi na chungu)halafu weka kitunguu saumu kaanga kwa pamoja mpaka viwe brown kabisaa
●weka vile viungo vingine pamoja na viazi kisha kaanga kwa pamoja,baada ya hapo weka pilau masala usiweke nyingi saana weka kiasi utapata rangi nzurii ya pilau kumbuka vile viungo vingine tulishaviweka kwahiyo pilau masala isiwe nyingi sana,kaanga mchanganyiko huu vizuri kisha weka nyama bila supu yake,iweke yenyewe ikaange pamoja na viungo vyote mpaka vichanganyike vzr
●baada ya hapo utaweka mchele wako kwenye sufuria utaukaanga pamoja na mchannyiko uliokuwepo halafu utaweka chumvi,kaanga mchanganyiko huu kwa dk kama 3-4 halafu weka supu ya nyama changanya ongeza na yale maji ya moto kisha acha mchanganyiko wako uive taratibu ukiwa umefunika sufuria lako

Hatua ya 2
●maji yakikauka geuza pilau lako kidogo halafu punguza moto chini acha moto kidogo sana,halafu acha kwa dk 5 palia na moto wa wastani kwa juu,.pilau haligeuzwi geuzwi sana kwasababu unaweza vuruga viazi vyako na lisipendeze tena
●ukipalia kwa moto wa juu kwa dakika 5-6 funua ugeuze tena baada ya hapo ongeza moto juu kidogo na uache chakula chako kwa dk 20, kama moto ni mchache utafanya dk 30....Baada ya hapo pilau letu litakuwa tayari na mashAllah litakuwa taaam saana😋😋😊

Hatua ya 3/mwisho
●toa ukoko wa juu ligeuze pilau lako,pakua na tayari kwa kula
●unaweza kula kwa salad/kachumbari au mbogamboga za majani bila kusahau juice fresh ya matunda au smoothie yoyote ile.

Mpaka wakati mwingine,.tchaoooo!!!!!
 

Forum statistics

Threads 1,250,894
Members 481,523
Posts 29,749,882