Pikipiki zisizotumia Petroli

Obhusegwe

JF-Expert Member
Dec 28, 2008
231
28
Hello wakubwa,

Jana nikiwa nimekaa sehemu nikisubiri shoeshiner amalize kuning'arishia viatu, nilimwona jamaa akisepa mitaani na kapikipiki fulani hivi lakini kalikuwa hakatoi mlio wowote, nikashangaaa. Nilivyowaulizia watu waliokuwa wamekaa karibu karibu (akiwemo na shoe shiner) wakasema ni pikipiki inatumia betri, yaani unachaji then unatambaa barabarani, hakuna kuingia petrol station wala nini!! Waliendelea kusema kuwa huyo jamaa mwenye piki*2 hiyo anakaa mbagalla, na anatumia kwa siku tatu to and fro ndo anachaji betri kwny umeme! Nasikia ni tech ya MCHINA

Sasa sijui ni kweli au la, jamani naomba mtu mwenye uhakika anihabarishe nijue zinapatikana wapi nijichukulie moja make nimechoshwa na hizi habari za petroli!!

Plz mwenye data za uhakika amwage hapa nahisi kuna watu wengi tunaweza kufaidika na hii teknolojia.

Thanks, nasubiri michango yenu.
 
Hiyo ni kweli.Wachina karibu miaka 5 sasa hawatumii pikipiki za petrol.Ni pikipiki za umeme tu.Na ukionekana una ya petrol unakamatwa.Wanapunguza uchafuzi wa mazingira.
 
wow, sounds cool, sasa hapa bongo kuna duka wameshaanza kuziuza?
 
NI kweli jamani,hizo pikipiki ni tamu we acha,mimi nina mwaka sasa nimeshaachana na mipikipiki ya umeme kwani ni ghatari tupu,hizi pikipiki zina uwezo wa kwenda hadi 100km kabla hazijaisha umeme na nyingi speed yake ni 40km/hr.Ila kwa sasa kuna pikipiki mpya zimeingia kwa kichina wanaiita DianMo(kwa kidhungu zijui ni Electric Motor au nini,sina uhakika).HIzi zinaweza kukimbia kama Motorbike ila tu hazina uwezo wa kwenda umbali mrefu,kwa sasa nyingi zina uwezo wa kwenda 60km kabla hazijaisha umeme.
Kazi kwenu wadau.
Hiyo hapo chini ni mfano wa pikipiki ambayo nimekuwa nikiitumia zaidi ya mwaka bila kwenda kwa fundi,kumbuka bure iinaponza hivyo pikipiki ya 1000yuan sio sawa na ile ya 3000yuan ingawa nje zitaonekana sawasawa.
 
Attachments

  • DSC00412.JPG
    DSC00412.JPG
    112.6 KB · Views: 446
  • DSC00414.JPG
    DSC00414.JPG
    91.4 KB · Views: 381
  • DSC00415.JPG
    DSC00415.JPG
    102.6 KB · Views: 319
mkuu kilongwe 1000 yuan au 3000 yuan ni sawa na shilingi ngapi za kikwetu?Hapo umeniacha kidogo
 
3,000.00 CNY = 577,516.40 TZS
China Yuan Renminbi Tanzania Shillings

ingia web hii XE - Full Universal Currency Converter waweza kujua rate mbalimbali za kubadilisha fedha kwenda kwa Shilingi

Thanks mkuu kwa fununu hiyo, binafsi ningependa kuwa nayo ila mpaka sasa sijaona aliyenambia kama zinapatikana hapa dar, au mpaka uagize huko china, na je zinasajiliwa na kullipa road licence? make nahisi hazina cc, sasa wataziclassify vipi?
 
NI kweli jamani,hizo pikipiki ni tamu we acha,mimi nina mwaka sasa nimeshaachana na mipikipiki ya umeme kwani ni ghatari tupu,hizi pikipiki zina uwezo wa kwenda hadi 100km kabla hazijaisha umeme na nyingi speed yake ni 40km/hr.Ila kwa sasa kuna pikipiki mpya zimeingia kwa kichina wanaiita DianMo(kwa kidhungu zijui ni Electric Motor au nini,sina uhakika).HIzi zinaweza kukimbia kama Motorbike ila tu hazina uwezo wa kwenda umbali mrefu,kwa sasa nyingi zina uwezo wa kwenda 60km kabla hazijaisha umeme.
Kazi kwenu wadau.
Hiyo hapo chini ni mfano wa pikipiki ambayo nimekuwa nikiitumia zaidi ya mwaka bila kwenda kwa fundi,kumbuka bure iinaponza hivyo pikipiki ya 1000yuan sio sawa na ile ya 3000yuan ingawa nje zitaonekana sawasawa.

Mkuu uliipata wapi? Ulinunua hapa au ulitumiwa na mjomba-ako kutoka china?
 
Lakini baisikeli ni injini kiuno. spidi yake haizidi hizi pikipiki ya umeme na kama kiuno kikichoka sijuhi utachaji wapi.
 
Back
Top Bottom