Pikipiki zapigwa marufuku Bujumbura

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
Pikipiki hutegemewa sana kwa uchukuzi Burundi.

Burundi imepiga marufuku pikipiki kuingia katikati mwa mji mkuu Bujumbura katika juhudi za kujaribu kupunguza mashambulio.

Pikipiki hutumiwa sana kusafirisha watu na mizigo Bujumbura lakini sasa zimekuwa zikitumiwa kutekeleza mashambulio, meya wa Bujumbura Freddy Mbonimpa anasema.

Mtu mmoja aliuawa Jumatatu wiki hii watu waliokuwa wameabiri pikipiki waliporusha guruneti tatu.

Usalama umeimarishwa mjini humo tangu kutoka kwa mashambulio hayo na polisi wanapekua watu na magari, shirika la habari la AFP linasema.

“Polisi wamegundua kwamba wahalifu hubeba guruneti wakitumia mabegu au vikapu,” Bw Mbonimpa anasema.

Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Prime Ndikumagenge anasema marufuku hiyo itaathiri sana watu wanaosafiri kutoka eneo moja hadi jingine mjini.

Huwezi kutoka kusini mwa mji hadi kaskazini bila kupitia katikati mwa mji, anasema.

Machafuko yalizuka nchini Burundi Aprili mwaka jana Rais Pierre Nkurunziza, ambaye amekuwa uongozini tangu 2005, alipotangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu.

Watu 400 wamefariki na wengine 240,000 kutorokea nchi jirani tangu wakati huo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Hahahah daah waendesha boda boda ndo basi tena,itabd serikali iwape ruzuku waweze Kuishi sasa
 
huyo Mayor hana lolote! hayo yote ni kupoteza lengo tu... cha muhimu ni Nkurunziza kuachia ngazi na kupisha "MHUTU" mwingine aongoze, lol! juzi mayor huyo huyo ametangaza kutaifisha nyumba za waliokimbia nchi na kuzigeuza office za polisi (ambao ndio wao waliowakimbiza na wengine kuuwawa) nchi ikiongozwa na wasanii wasio tumia akili yani tabu tupu... kwenye budget yao ya huu mwaka eti kuna pesa zimetengwa za kutengeneza ndege ya kumsafirisha Raisi wakati ndege yenyewe ishauzwa mwaka jana! hata kama ingekuwepo, ni ya kumpeleka wapi huyo Raisi wakati hata Bujumbura kwenyewe anaogopa kufika? Burundi NOMA!
 
Pikipiki hutegemewa sana kwa uchukuzi Burundi.

Burundi imepiga marufuku pikipiki kuingia katikati mwa mji mkuu Bujumbura katika juhudi za kujaribu kupunguza mashambulio.

Pikipiki hutumiwa sana kusafirisha watu na mizigo Bujumbura lakini sasa zimekuwa zikitumiwa kutekeleza mashambulio, meya wa Bujumbura Freddy Mbonimpa anasema.

Mtu mmoja aliuawa Jumatatu wiki hii watu waliokuwa wameabiri pikipiki waliporusha guruneti tatu.

Usalama umeimarishwa mjini humo tangu kutoka kwa mashambulio hayo na polisi wanapekua watu na magari, shirika la habari la AFP linasema.

“Polisi wamegundua kwamba wahalifu hubeba guruneti wakitumia mabegu au vikapu,” Bw Mbonimpa anasema.

Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Prime Ndikumagenge anasema marufuku hiyo itaathiri sana watu wanaosafiri kutoka eneo moja hadi jingine mjini.

Huwezi kutoka kusini mwa mji hadi kaskazini bila kupitia katikati mwa mji, anasema.

Machafuko yalizuka nchini Burundi Aprili mwaka jana Rais Pierre Nkurunziza, ambaye amekuwa uongozini tangu 2005, alipotangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu.

Watu 400 wamefariki na wengine 240,000 kutorokea nchi jirani tangu wakati huo.

Chanzo: BBC Swahili
CbYWlIIWEAAi6yQ.jpg
 
Hilo sio jibu lake ila watafute njia zilizo sahihi kumaliza tatizo .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom