laurent Msembeyu
Senior Member
- Oct 5, 2015
- 121
- 101
Police walinunua au walipewa msaada wa pikipiki 500 nchi nzima kwa ajili ya shughuri za ki- polisi, pikipiki hizo alikabidhiwa aliyekuwa IGP Bwana Said Mwema ili zigawanywe inchi nzima zisaidie shughuri za police. Pikipiki hizo ambazo zimetengenezwa china mda huu napoandika bandiko hili haziko barabarani, zimeisha chakaa,ni lightoff, zimekuwa screpa ndani ya miaka mitatu tu tangu zitolewe, zilizopo barabarani hazizidi 20 inchi nzima.
Hapa nilipo mkoani Mtwara tumefanya survey, Manisapaa ya Mtwara/Mikindani pikipiki zote zimekufa i.e indicator zote zimepululuka, mabampa ya pembeni yameanguka, Site mirror zote zimetolewa, taa za mbele (headlight) zimepasuka, tyre zimekwisha. Hivyo hivyo Wilaya ya Masasi, Newala , Nanyumbu, pia tumesurvey mkoa wa Lindi ni hivyo hivyo.
Nini chakujifunza kutokana na kadhia hii:-

- Kama pikipiki zile zilitolewa kama msaada, basi msaada huo ulikuwa na agenda iliyojificha kwa sababu there is no free lunch under the sun, ndani ya msaada huo kuna watanzania wameumia au wachina wameshinda tenda na kutoa huduma mbovu mfano barabara, bidhaa fake n.k
- Kama pikipiki hizo zilinunuliwa basi procument officer wa jeshi la polisi (au wizara ya mambo ya ndani ) alipewa mlungula na kukubali kuingiza pikipiki zisizokuwa na kiwango, huu ni muendelezo tu wa utumishi serikalini ambao siku za hivi karibuni umekosa kabisa weledi.
- Pia tunajifunza kwamba hakuna kitu toka china kihusucho mambo ya usafiri kitafaa katika shuguri za kipolisi, sekta hiyo ina shughuri nyingi ngumu na nzito kwa hiyo inahitaji vifaa imara na vya kudumu, jeshi lifikirie upya kuagiza vitendea kazi vyake toka China, Kama ni pikipiki jeshi liagize pikipiki toka JAPAN , HONDA XL 125 and above ndizo zitafaa kwa shuguri za kipolisi. Heri kuagiza pikipiki chache zidumu kuliko kuagiza nyingi kwa ajiri ya uraisi wa bei halafu zikae miezi 6 tu.