Pikipiki kupakia bati na vitu vya aina hiyo si kuvunja sheria?

Asamwa

JF-Expert Member
Apr 13, 2012
3,677
2,438
Kuna hii tabia ya wenye pikipiki hasa boda boda kupakia mizigo mirefu ambayo inachomoza pande zote, kwa mfano mbao, bati, nondo n.k.

Hii ni hatari sana kwa watembea kwa miguu na hata vyombo vingine vya usafiri.

Nimeshashuhudia zaidi ya mara mbili pikipiki iliyopakia mizigo ya aina hiyo ikipita eneo ambalo wako askari wa usalama barabarani lakini hawakuchukua hatua yo yote.

Ina maana kuwa sheria inaruhusu upakiaji wa namna hii?
 
Ninachofahamu kwenye gari hautakiwi kupakia mzigo kuzidi bodi yako hasa magari ya uchukuzi mfano carry, canter ama fuso. (Alinifundisha dereva wangu) Sijajua uko upande wa pikipiki
 
Back
Top Bottom