Pikipiki ilivyookoa roho yangu, ningeuawa kikatili...

Truth guy.

JF-Expert Member
Oct 30, 2013
396
195
lugha aliyokuwa akiongea yule mrembo,sikuweza kuielewa ila nilihisi anaongea kitutsi,alipomaliza kuongea,aliniambia kuwa yeye hajui popote kunakopatikana silaha,alinidadisi mi ni nani hasa? mwishoni alijiridhisha kuwa lazima nitakuwa askari mpelelezi,ktk chunguzi nyingi nilizowahi kufanya,nikiri tu kuwa huu ulikuwa uchunguzi wa kizembe sana,na sijui kwa nini nilijisahau kiasi hiki,usiku ule niliachana na yule mrembo nikamlipa haki yake naye kuondoka,ilikuwa yapata majira ya saa 5 usiku wakati roho yangu ilipogoma kabisa kulala kwenye ile gest,niliamka na mara nikawa nasikia sauti moyoni mwangu ikiniamuru niondoke pale kwani si sehemu salama kwangu,hali ya ule mji mdogo ilikuwa tulivu sana,nilijiuliza niende wapi usiku ule? wakati nikiwa ktk hali hiyo ya sintofahamu,ghafla nilisikia kelele nje ya gest na sauti ya mwanamke akilia,JE NINI KITAENDELEA? USIKOSE KUSOMA PART-3 YA STORY HII YA KWELI YA KUSISIMUA,WENGINE ITAWALIZA.
 
Kwanini unalazimisha kuiwekea parts stori fupi kama hii, kwanza haina hata mzuka bora ungeimalza tu.
 
Wala usilete part 3, idelete huko huko kichwani. Huwezi kutuzeveza watu wazima eboo!
 
Wee dogo mburula kweli,part 1 haijulikani ipo wapi,part yenyewe umeiweka kwenye thread mpya.
Naona haina haja ya kuendelea na vipandevipande vya ki whatsapp.
 
Jamani mi nitaimaliza yote hata kama hamtaki,wapo watakaoisoma yote,nyie kama hamtaki mkiona heading yake acheni kusoma,hata ikisomwa na mmoja tu inatosha,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe,bila kujali how shall my scriptures be jugded,naandika mfupi maana natumia simu,jf tupo wengi mno si wote wenye mtazamo kama wenu,mwingine kanituhumu pengine nakunywa pombe aina ya viroba,ktk maisha yangu sijawahi kunywa pombe kabisa,kazi za kijasusi ni ngumu sana wakati mwingine inakulazimu kufanya jambo lisilo la kawaida,ili upate unachohitaji,yes nilizini na yule binti lakini nilitumia kinga vizuri,so mwenye kusoma asome,anayeacha aache,hata hivyo humu kuna thread nyingi,si lazima kusoma thread yangu,nadhani nimeeleweka,kuniandikia uzi wa kunituhumu ni kunipoteza muda tu.siku njema!
 
Sasa umewezaje kujibu tuhuma ambazo zinakupotezea muda?
Kuandika kupitia simu mii naona hoja hii wala haina mashiko,ingekuwa unatuma sms sawa gharama itakosti/simu nyngne huwa zinatabia ya kuwa limit ya sms zaid ya hapo inageuka kuwa MMS,
lkn huku ukiwa net wala hivyo vikomo hakuna,matokeo yake wee unasingizia simu.
Mkuu jitahidi kuendana na washusha Hadithi,Simulizi,riwaya n.k wa humu jf.naona wee upo ki fb zaidi.
Fanyia kazi ushauri wala hutakumbana na dhahama zilizokukuta hpo juu.
Hakuna aliekamilika ila ukionekana unaenda ndivyo sivyo lazima uambiwe.

Unatuletea visimulizi vya kitoto,halafu unategemea ss tukae kimya?Never happen.
Hata kama ulitaka kutupa elimu!ujumbe flani,siungewapa hata wapita njia huko mtaani.
Acha kutoa povu Guy
 
Last edited by a moderator:
Kelele za watu nje ya gest usiku ule na sauti ya mwanamke akilia vilinifanya nitaharuki sana,nikasikia sauti ya kiume ikimfokea yule mwanamke aliyekuwa akilia,"umeshatembea naye mara ngapi?"ilifoka sauti ile ikimhoji yule mwanamke,nilianza kutetemeka nisijue la kufanya,wapangaji wenzangu kwenye ile gest walianza kuamka ili kujua kinachoendelea,nami nilipata ujasiri nikaungana nao,kupitia mlango wa uani nilichungulia lile kundi la watu lililokuwa linakuja pale gest,sikuamini nilichokiona,nilimuona yule mrembo wa kitutsi akiwa na lile kundi,na ndiye alikuwa akipigwa na kulia,wanaume wawili wa miraba minne mmoja akiwa na panga mkononi walikuwa wakija kwa kasi kwenye ile gest,nilijua tu anayetafutwa ni mimi hakuna mwingine,pikipiki yangu aina ya Honda CD 175 niliyoinunua kampala ambayo ndo usafiri niupendao sana nilikuwa nimeipaki mule gest,sikutaka kupoteza muda niliingia chumbani nikachukua rasket yangu,ilhali wapangaji wenzangu wakistaajabu,SOMA PART -3. UJUE KILICHOENDELEA.
 
Nilipoingia chumbani ili kuchukua rasket yangu ili nitoweke eneo lile hatari,mwili wangu uliishiwa nguvu baada ya kumkuta mule chumbani mmoja wa wapangaji wenzangu niliyeingia naye kulala muda mmoja, alikuwa ni mwanamke ambaye kabla hatujalala nilimsikia akijitambulisha kwa jamaa mmoja kuwa yeye ni mfanyabiashara wa mahindi anayepeleka Bujumbura.

Mwanamke yule alikuwa uchi wa mnyama,alikuwa na makalio makubwa,na matiti ya kuvutia,hakuwa mrembo kivile,ila alikuwa sexual flirtive,siyo siri nilichoka,mkononi mwake alikuwa kabeba chu.pi yake,aliponiona alinikaribisha kwa ukarimu,jamani ni vigumu kuamini nayowaambia,hakukuwa na namna nilijua nipo hatarini na ilinipasa kufanya jambo ili kujiokoa,sikumjali yule mwanamke,niliifata ile rasket yangu iliyokuwa mezani,looh kumbe nilichelewa,mwanamke yule alikuwa tayari kainyakua ipo mikononi mwake,sikutaka kujiuliza swali lolote,kila kitu kilikuwa dhahiri kuwa,natakiwa kudhurika na watu nisiowajua.

SUBIRI PART-5,NI KWELI KABISA IMENITOKEA.
 
Nilipiga kelele kwa nguvu na kuwasihi wapangaji wenzangu waniokoe kwani nilikuwa nauawa sasa, mwanaume mmoja kati ya wale wawili wa miraba minne alinipiga mtama nikadondoka chini na mwingine mwenye panga aliliinua juu ili anikate.

kwa kasi ya ajabu mpangaji mwenzangu mmoja alimrukia teke yule jamaa na kumpiga mkononi hadi panga likamponyoka,nilijiburuza pale chini ili kuifuata pikipiki yangu iliyokuwa pale uani,kabla hata sijaidandia ghafla nilisikia mlio wa risasi "paaa"wakati nikijiuliza nini kinaendelea?

risasi nyingine tena ikaunguruma,kutahamaki maskini ya Mungu yule mpangaji aliyeniokoa nisikatwe panga alikuwa katandikwa risasi mbili ambazo hata hivyo hazikuweza kumdhuru maana ziliishia kwenye koti kubwa la baridi alilokuwa kavaa zikalichanachana lote sehemu za mkono wa kulia maana lilisambaa kama matawi na hivyo kumnusuru,milio ile ya risasi iliamsha taharuki kubwa ktk mji mdogo ule,kila mmoja kwenye gest ile alikimbia akitafuta mahali salama pa kujificha,mi nilikimbilia chooni na kujifungia......
 
Nikiwa ndani ya kile choo nilisikia kelele nyingi zikitokea nje ya ile gest,lile genge la wale watu hatari lililokuwa limenifuata pale gest.

Nililichungulia kupitia tundu dogo la funguo la ule mlango wa choo,nikawaona wale watu wanahaha kunitafuta kila upande mule ndani,sikujua muhudumu alikuwa kajificha wapi, mara tena nikasikia zile kelele kutoka nje zikija uelekeo wa gest niliyokuwemo.

Lile kundi la watu hatari lilikimbia nje baada ya kusikia kelele zile,papo hapa nilipata mwanya wa kutoka mafichoni, nikaiendea pikipiki yangu haraka, niliwasha injini, wakati nataka kuondoka tu, katika hali isiyokuwa ya kawaida nilishtuka kuona yule mtu mwenye miraba minne akiwa pamoja na yule mwanamke niliyekuwa nimemkuta chumbani kwangu akiwa uchi wa mnyama.

Bazazi yule aliinua panga ili kunikata kichwani,na kwa kuwa pikipiki ilikuwa tayari kwenye moto,nilishika clutch na kuweka moto mkubwa,nilipoachia ghafla pikipiki ilipaa na kumfanya yule muuaji kunikosa na lile panga kichwani na hivyo kujikuta akimkata vibaya........
 
mkuu kisa kinaelekea kunoga,nakushauri usiitoe tena mpaka utakapokua tayari kutoa story kamili.
 
Panga lile lilimkata vibaya yule mwanamke begani,damu iliruka, tayari nilikuwa nje ya ile gest baada ya kutoka kwa spid isiyo ya kawaida,nilipishana na lile kundi la watu waliokuwa wakija pale gest,mmoja wao nilimuona akiwa kwenye pikipiki aina ya baja 250,kundi lile liliponiona lilipiga kelele,"anatorokahuyo mmekuwa wazembe nyie keshatuharibia biashara mbwa huyo",nilisikia zile kelele ilhali nikizidi kukimbia hovyo bila ya kujua hata naelekea wapi,sekunde chache baadae nilitokeza kwenye barabara ya lami,kupitia 'site mirror' niliona mwanga mkali wa taa ya pikipiki ukija kwa kasi ya ajabu,sikutaka kuwa na hofu yoyote,sekunde kama tano tu pikipiki ile tayari ilinipita,sikuamini nilichokiona,ilikuwa ni ile pikipiki baja250 iliyokuwa nje ya gest pamoja na lile kundi la wauaji,nilipunguza mwendo ghafla,nayo ikasimama mita chache kutoka nilipo,niligeuka haraka na kushika njia nyingine ya vumbi na wao bila kuchelewa waligeuka na kuanza kunikimbiza,hapo sasa nilijua tayari nakufa,siku zangu zimeisha hapa duniani...
 
duh.!!,bonge la bongo "muvi".haya part 2 lini?.

MKUU HIYO NI PART 8,PEKUA ZOTE KUANZIA PART 1,zote nimezipost zimo.kila siku nawapostia ikifika sehemu ya 15,nitaistop ili nije niwaletee full story,ni ya kweli kabisa.
 
Niliongeza spidi pikipiki ikazidi kukimbia lakini sikuweza kuwaacha wale watu,na nilikuwa naenda sehemu nisiyoijua,nilipoingiza gia namba 5 hapo niliona maajabu ambayo sikutarajia kabisa,pikipiki yangu ni Honda Benly CD 175 Japan originated.

Ni watu wachache sana wenye hizi pikipiki hata Dar niliiona moja tu sidhani kama zipo nyingi, huwa zikiwa spidi zinakata mlio na unasikia upepo tu, sasa ndo ilifikia stage hiyo,wauaji wakiwa na Baja 250 walianza kuchemka kunipata

Niliona kwenye site mirror nikizidi kuwaacha,sikuamini kwa kweli,Honda Benly CD 175,inawezaje kuiacha Baja cc 250? wataalamu wa vyombo vya moto mnijuze,hapo ndo nawapigia saluti wajapan,km kama 12 baadae niliiona Baja ikiwa kwa mbali sana nilianza kuiacha barabara ya vumbi na mbele niliona njia panda mbili za barabara ya lami,sikujua nifuate ipi niache ipi,sikuwa na muda wa kupoteza kufikiri niliamua kukata kulia na kuendelea kukimbia zaidi dakika 2 tu nilikuwa katikati ya msitu mnene wa kutisha mwili ulisisimka kwa hofu nikawa naomba Mungu......
 
Back
Top Bottom