Pikipiki ilivyookoa roho yangu,ningeuawa kikatili,Part -5.

Truth guy.

JF-Expert Member
Oct 30, 2013
396
195
Kitendo cha yule mwanamke kunyakua rasket yangu ambamo ndani yake kulikuwemo na laptop, pamoja na camera ya kisasa aina ya Minolta,kilinifanya nipagawe kabisa,hata hivyo nikajikaza kiume na kumvaa yule bazazi wa kike ili kuokoa vitu vyangu vya thamani.

Sekunde ile ile nilirusha teke kali lililotua tumboni mwa yule bazazi, aliguna kwa maumivu na kabla hajatulia vyema, nilimtandika ngumi nzito ya mdomoni, damu zikaruka na jino lake moja kudondoka chini ilhali bazazi naye akipiga mweleka chini, kelele za vurugu chumbani mule ziliwafanya wapangaji wote kuanza kuingia chumbani kwangu

Wakati hali hiyo ikitokea nilikuwa tayari mkononi mwangu nimebeba rasket,nilianza kutoka mbio mule chumbani kuelekea nje,mlangoni nikastaajabu kupishana na lile kundi la watu lililokuwa linakuja gest likiwa na mrembo yule niliyekuwa nimetoka kulala naye masaa machache yaliyopita,kundi lile pamoja na wapangaji wenzangu,wote pamoja walikuwa wakiingia chumbani,ehee huyu hapa ndiye mwenyewe,mrembo yule alipayuka,nami kwa uoga nikapiga kelele.
 
Mkuu story yako ni nzuri,ila nakushauri uiweke kwa ujumla tupate uhondo kamili,maana inaonekana ni story fupi,tunaweza kuilewa vizuri tu kwa pamoja.
 
mkuu story yako ni nzuri,ila nakushauri uiweke kwa ujumla tupate uhondo kamili,maana inaonekana ni story fupi,tunaweza kuilewa vizuri tu kwa pamoja.

asante kwa ushauri,kwa kuwa bado nipo pori,ngoja nirudi town nitaiunganisha yote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom