Tetesi: Pikipiki alizotoa waziri mkuu Arusha ulikuwa ni mradi wa mtu kuwakopesha vijana

Bakeza

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
348
192
KUMBE WAZIRI MKUU AMEINGIZWA KWENYE MRADI WA KITAPELI ARUSHA.

Siri imefichuka kuhusiana na pikipiki 200 zilizogawia kwa vijana wa Arusha, mwishoni mwa wiki iliyopita WAZIRI MKUU Majaliwa K Majaliwa alizindua pikipiki 200 waliokopeshwa vijana wa Arusha,

Jana nilikutana na mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa pikipiki mjini Arusha ambaye kwa maelezo yake aliniambia anafahamu kuhusu huo Mradi na kwa mara kadhaa walikutana na mkuu wa mkoa wa Arusha ndg Mrisho Gambo kukubaliana ili pikipiki zake ziingizwe kwenye Mradi huo, kwa maelezo yake kuna mambo walishindwa kukubaliana na RC Gambo nadhani ndo ikawa sababu ya yeye kutoshwa,

Sasa kwa msiyojua huo mradi haukuwa msaada kama ulivyokuwa ikitangazwa bali ni biashara tena ya kinyonyaji embu fuatilia masharti ya mkopo wa pikipiki hizi,

Kila aliyekopeshwa pikipiki alitakiwa adhaminiwe na mtu mwenye hati ya nyumba au mali isiyohamishika, hapa mkopeshaji anapata hakika ya kupata marejesho ya mkopo wake.

Kila mkopaji wa pikipiki alitakiwa arejeshe kiasi cha Tsh 8000 kwa siku ndani ya mwaka mzima yaani kwa siku 365

Sasa wewe chukua 8000×365=2920,000

Kwa maana hiyo kila mtu atakuwa ameuziwa pikipiki tsh 2,920,000/=

Bei ya Pikipiki ya aina zilizokopeshwa dukani ni tsh 2000,000/=

Kwa maana hiyo tsh 920,000/= anayopata mkopeshaji ni riba ya mkopo wake huo,

Hii inamaana kwamba amepata fursa ya kuuza pikipiki 200 kwa mwaka kiasi ambacho siyo rahisi kwa kipindi kama hichi kukifikia mauzo ya kiwango hicho, lakini pia anapata riba ya mtaji wake ya kiasi cha tsh 920,000/= kwa pikipiki moja,

Hii inamaana kuwa Ukiacha faida ya kawaida tu ya kuuza pikipiki moja tsh 2000,0000/= mkopeshaji anapata cha ziada yaani riba ya tsh 920,000×200=184,000,000.

Mwisho wa siku huyo anayesema amewasaidia vijana kujikwamua kiuchumi atakuwa ametengeneza tsh milioni 184 kwa mwaka.

Ukiacha bishara ya madini ya Tanzanite hapa Arusha sijui kama kuna biashara nyingine inalipa kama hii, sasa sijui Waziri mkuu ameingizwa kwenye dili hili kwa kujua au kwa kutojua sijui, ila mimi tu niwatakie wakopaji kila la Kheri katika kurejesha fedha kwa waliowasaidia kwa wakati wasije kufilisiwa waliyowadhamini.
 
Kwenye hotuba yao walisema wanawasaidia vijana na kuwaepusha na unyonyaji unaofanywa na wamiliki wa pikipiki ambao huwapa baada ya kuwanyonya sasa mimi nilifikiri waliwapa bure ila warudishe kiwango cha kununulia pikipiki
 
Nipishe mbali sheitwani chama kongwe, nimekuchoka na hila zako mpaka unamzidi maarifa sheitwani!!!
 
Utapeli uko wapi? Unadhani kama kila mmoja angeamua kujichanga ili aje kununua pikipiki yake angefanikiwa? mtaji angeutoa wapi? Kama muuzaji/mkopeshaji angeuza kwa cash unadhani angezungusha mara ngapi? kwa nini na yeye asipate faida?
Riba ya 46% ni zaidi ya mabenki yanayotoza kati 15% na 23%, huu ni utapeli na wizi kwa wanyonge.
 
KUMBE WAZIRI MKUU AMEINGIZWA KWENYE MRADI WA KITAPELI ARUSHA.

Siri imefichuka kuhusiana na pikipiki 200 zilizogawia kwa vijana wa Arusha, mwishoni mwa wiki iliyopita WAZIRI MKUU Majaliwa K Majaliwa alizindua pikipiki 200 waliokopeshwa vijana wa Arusha,

Jana nilikutana na mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa pikipiki mjini Arusha ambaye kwa maelezo yake aliniambia anafahamu kuhusu huo Mradi na kwa mara kadhaa walikutana na mkuu wa mkoa wa Arusha ndg Mrisho Gambo kukubaliana ili pikipiki zake ziingizwe kwenye Mradi huo, kwa maelezo yake kuna mambo walishindwa kukubaliana na RC Gambo nadhani ndo ikawa sababu ya yeye kutoshwa,

Sasa kwa msiyojua huo mradi haukuwa msaada kama ulivyokuwa ikitangazwa bali ni biashara tena ya kinyonyaji embu fuatilia masharti ya mkopo wa pikipiki hizi,

Kila aliyekopeshwa pikipiki alitakiwa adhaminiwe na mtu mwenye hati ya nyumba au mali isiyohamishika, hapa mkopeshaji anapata hakika ya kupata marejesho ya mkopo wake.

Kila mkopaji wa pikipiki alitakiwa arejeshe kiasi cha Tsh 8000 kwa siku ndani ya mwaka mzima yaani kwa siku 365

Sasa wewe chukua 8000×365=2920,000

Kwa maana hiyo kila mtu atakuwa ameuziwa pikipiki tsh 2,920,000/=

Bei ya Pikipiki ya aina zilizokopeshwa dukani ni tsh 2000,000/=

Kwa maana hiyo tsh 920,000/= anayopata mkopeshaji ni riba ya mkopo wake huo,

Hii inamaana kwamba amepata fursa ya kuuza pikipiki 200 kwa mwaka kiasi ambacho siyo rahisi kwa kipindi kama hichi kukifikia mauzo ya kiwango hicho, lakini pia anapata riba ya mtaji wake ya kiasi cha tsh 920,000/= kwa pikipiki moja,

Hii inamaana kuwa Ukiacha faida ya kawaida tu ya kuuza pikipiki moja tsh 2000,0000/= mkopeshaji anapata cha ziada yaani riba ya tsh 920,000×200=184,000,000.

Mwisho wa siku huyo anayesema amewasaidia vijana kujikwamua kiuchumi atakuwa ametengeneza tsh milioni 184 kwa mwaka.

Ukiacha bishara ya madini ya Tanzanite hapa Arusha sijui kama kuna biashara nyingine inalipa kama hii, sasa sijui Waziri mkuu ameingizwa kwenye dili hili kwa kujua au kwa kutojua sijui, ila mimi tu niwatakie wakopaji kila la Kheri katika kurejesha fedha kwa waliowasaidia kwa wakati wasije kufilisiwa waliyowadhamini.
Kwa hiyo waliokopeshwa sio vijana ni vikongwe wa miaka 90 kwenda mbele?
 
Kwani kuna MTU alishikiwa bunduki akakope?
Utapata wapi mtu akupe pikipiki mpya ufanyie kazi umpe elfu nane tu kwa siku,baada ya mwaka inakua yako
Mie naona chadema mmeumizwa sana na hizo pikipiki,inabidi kuwapiku akina Gambo nyie toeni pikipiki 1,000 na msidai marejesho
Hakuna aliyeumia ila nawaonea huruma sana wakopaji kwa uzoefu wangu wa mikopo only 25% ya wakopaji huweza kurudisha wengine huishia kufilisiwa na mifano ipo mingi.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom