Piki piki za kichina - ni ipi bora zaidi?

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
1,037
2,000
Kwa wana JF
mimi nimekuwa naendesha pikipiki ya San LG kwa muda mrefu tu huku kijijini (kwa shughuli zangu) na haijanisumbua kiasi cha kunikatisha tamaa.

Kwa sasa naona kuna ujio wa majina meeengi ya Pikipiki.....Kuna rafiki yangu anahitaji kununua Pikipiki kwa ajili ya shuhuli zake na ameniuliza nipendekeze piki piki ipi kati ya haya majina mengi ya kichina ambayo ni nzuri zaidi kwa sasa(Imara, yenye spare na inayopendeza)

Kuna mtu mmoja ameniambia anunue aina ya Boxer (150cc) Kuna anayeifaham?

Nitashukuru kwa mawazo yenu...
 
pingu mkoka

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
434
225
Kwa wana JF
mimi nimekuwa naendesha pikipiki ya Sun LG kwa muda mrefu tu huku kijijini (kwa shughuli zangu) na haijanisumbua kiasi cha kunikatisha tamaa.

Kwa sasa naona kuna ujio wa majina meeengi ya Pikipiki.....Kuna rafiki yangu anahitaji kununua Pikipiki kwa ajili ya shuhuli zake na ameniuliza nipendekeze piki piki ipi kati ya haya majina mengi ya kichina ambayo ni nzuri zaidi kwa sasa(Imara, yenye spare na inayopendeza)

Kuna mtu mmoja ameniambia anunue aina ya Boxer (150cc) Kuna anayeifaham?

Nitashukuru kwa mawazo yenu...
Boxe ndo yenyewe.
 
Dec 19, 2013
74
0
Tofautisha kati ya sunlg na sanlg ni vi2 viwili tofauti na boxer ni pikiphki ya india sio china. Mm pikipiki nazielewa sana nakushauri nunua sanlg ni pikipiki inayostahimili mazingira magumu
 
Nascoba

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
310
250
boxer ina speed mpaka 140,lakina haiwezi kuhimili mikiki mikiki hasa ya vijijini,pia spea zake bei juu,nunue sanlg au T.BETTER.
 
Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
1,037
2,000
oops sorry
Niliyo nayo ni San LG

Kama boxer ni ya India nafikiri itakuwa nzuri kwani ni maarufu kwa uimara na matumzi mazuri ya mafuta ila kwa mazingiraya kijijini ndio sijui......
T.BETTER hiyo siifaham...ila nitaifuatilia na kama nitapata mawazo ya wanachama nitaipa pia kipaumbele...
Asante Ezekiely
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom