PiKi na FoodSasa wafanye yafuatayo

C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,070
3,718
Kumekuwa na kuibuka kwa applications ambazo zinamfanya mtu kuweza kuagiza chakula online na kuletewa kwa delivery, ambazo ni piki na foodsasa, app hizi zinasaidia sana kwenye shughuli za kuagiza vyakula kutoka kwenye restaurants mbalimbali nchini

Hivyo basi ninashauri piki na foodsasa wafanye yafuatayo ambayo kila mmoja akiweza kufanya yafuatayo watafanikiwa sana

Kwanza waunganishe kampuni zao na kuja na startup moja iitwayo FoodPiki then wafanye yafuatayo

1) Wafungue ofisi EU, lengo la kufungua ofisi EU kwa maana ulaya ni kuwa "close to the money" ni rahisi kwa mwekezaji kuwekeza katika kampuni yenye ofisi ulaya na marekani hata kama operation ni Africa based ila wawe na operation system Berlin (Ujerumani)

2) Operation mind iwe ni Sadc region kwa maana nchi kusini mwa jangwa la sahara wasibase tu kwa Tanzania wakibase kwa Sadc region itasaidia kuvutia wawekezaji kuweka pesa zao pale

3) Watafute hela wa outcourse German companies hasa za Berlin pale katika kutengeneza app yao maana kwa sasa hizi app ni utumbo mtupu so ni bora watengeneze kwa wataalamu wa app ambao ni wa ujerumani ambao wanaweza kutengeneza delivery apps

4) Waandae mpango kazi wa ku rise seed investment ambao wanaweza kuanza kuandika kuomba Zaidi ya $1.2 na kuendelea

Wakifanya haya yote wategemee nini

Wategemee kununuliwa na kampuni kubwa kabisa ya delivery hero kampuni ya ujerumani ambao wao ndio kampuni inayomiliki apps za ku deliver chakula duniani wakimiliki kampuni ikiwemo kampuni ya foodpanda iliyonunuliwa kwa$ 3.5 Billions, delivery hero pia wamenunua kampuni za middle east, south America, asia za ku deliver chakula

Delivery hero wanataka kuja kwa soko la Africa lakini hakuna kampuni Giant ya Delivery App

So nimeona Foodsasa na Piki wakaamua kila mmoja wakaunganisha nguvu na kuanzisha startup moja ya food delivery kwa kuunganisha resources wakaiita FoodPiki

Maeneo ambayo watalenga ni pamoja na Tanzania, Uganda, Kenya, Zanzibar, Malawi, Zambia, Namibia, Angola, Congo brazaville, South Africa na Mauritius bado hakuna soko la uhakika la food delivery japokuwa demand ipo juu sana

Hivyo fanyeni yafuatayo na msishangae mkanunuliwa na delivery hero kwa Zaidi ya 100+ million
 
Kuna ombwe kubwa sana ya online food delivery kwa soko la SADC ilhali kuna thousands of restaurants within this region lakini pia urbanization ya Africa sadc countries inareflect kuwa hii product ina demad kubwa sana
 
Kuna ombwe kubwa sana ya online food delivery kwa soko la SADC ilhali kuna thousands of restaurants within this region lakini pia urbanization ya Africa sadc countries inareflect kuwa hii product ina demad kubwa sana
Upo vizuri katika hii Industry.
 
Back
Top Bottom