Pika mchanyato wa ndizi bukoba na viazi namna hii

Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,421
1,387
Mahitaji:

  • Ndizi za kupika(ndizi bukoba) kubwa 5.Menya,kata katikati ukipenda
  • Viazi ulaya 4 vikubwa.kata katikati kwa urefu
  • Nyama kilo 1.chemsha adi iive
  • Nyanya 4 kubwa.sugua au saga
  • Nyanya ya kopo kijiko 1 cha chai
  • Vitunguu 2 vikubwa
  • Carry powder kijiko 1 cha chai
  • Karoti 2 kubwa.kata duara
  • Royco mchuzi mix,kijiko 1 cha chai
  • Mafuta ya kupikia,kiasi upendacho
  • Chumvi

Njia

1.Katika sufuria weka mafuta,vitunguu ,na carry powder.Kaanga pamoja adi vitunguu viive,Ongeza nyanya ya tunda na nyanya ya kopo, kaanga adi nyanya iive.


  • Vitunguu viive lakini visiwe na rangi ya brauni iliyokooza
  • Ili kujua nyanya imeiva ,nyanya na mafuta vitatengana ndani ya sufuria.Nyanya isipoiva matokeo ya pishi hili hayatakua mazuri kama itakiwavyo.
2.Ongeza Ndizi na viazi,kaanga kwa pamoja kwa muda adi uone nyanya inashikana na viazi na ndizi.Ongeza nyama(bila mchuzi) endelea kukaanga kwa pamoja kwa dakika moja au zaidi.Ongeza mchuzi wa nyama adi ufunike mchanganyiko wa ndizi na yazidi kwa kwa inchi moja.Funika na acha vichemke kwa moto mdogo.

  • mchanyato wa ndizi.jpg
    Kama mchuzi wa nyama ni kidogo,basi changanya na maji
  • Pika chakula hiki kwa moto mdogo (simmer).Moto ukiwa mkali,mchuzi utakauka kabla ya ndizi na viazi kuiva na utalazimika kuogeza maji na utakua umeharibu pishi hili.

3.Vinapoelekea kuiva,ongeza royco,chumvi na Karoti.Tingisha au zungusha sufuria ili kuchanganya ,Acha vichemke adi viive.Chakula tayari kwa kula.

Chakula hiki kikiiva kinatakiwa kubaki na mchuzi ambao ni rojo.Hivyo zingatia sana kipimo cha maji na mchuzi wa nyama unachoweka.Na hakikisha hukaushi mchuzi wote unapopika.

ENJOY MLO WAKO
 
Chakula chako kizuri ila kwenye ingredients ulivyoweka Royco, Mchuzi Mix na Nyanya ya Kopo umenitoa hamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom