Pigo la kwanza kwa Simbachawene

YEHODAYA una personal grudges na Waziri wa mambo ya ndani?
Simbachawene mwenyewe ndie kaanza kujichemsha alisema atatumia wataalamu wa polisi zaidi kwenye utendaji

ghafla huyo kajiibukia kivyake na kuanza kuponda imani za watu mbele ya waandishi wa habari na kuita makanisa ya watu vibanda imani!!!! nyumba ya mtu ya kulala unaweza iita kibanda? sembuse nyumba ya kuabuadia mtu? unaidharau kiasi hicho na kuiita kibanda? huna adabu hata kidogo kisa ohhh mimi waziri.!!!! anyway uwaziri kauanzia mguu wa kushoto badala ya wa kulia

Jr
 
YEHODAYA una personal grudges na Waziri wa mambo ya ndani?

Jr
NDIO KWA KUTUKANA WATU WA MUNGU MAKANISA YAO KUITA VIBANDA IMANI SIJAPENDA tena MBELE YA PRESS CONFERENCE

WAO KWAO WANAONA NI MAKANISA,MA CATHEDRAL YEYE NANI KUITA VIBANDA IMANI? ANATAKIWA AOMBE MSAMAHA TENA KWENYE PRESS KAMA ALIVYOTAMKA NI DHARAU YA HALI YA JUU KWA IMANI ZA WATU
 
Kwa hili nasimama na Simbachawene. Vile ni vibanda imani au ukipenda vibanda imani umiza... Kanisa la kweli ni Kristo na wewe mwenyewe..!!! Mafuta ya upako ni biashara na utapeli na kichocheo cha madhabahu za giza
NDIO KWA KUTUKANA WATU WA MUNGU MAKANISA YAO KUITA VIBANDA IMANI SIJAPENDA tena MBELE YA PRESS CONFERENCE

WAO KWAO WANAONA NI MAKANISA,MA CATHEDRAL YEYE NANI KUITA VIBANDA IMANI? ANATAKIWA AOMBE MSAMAHA TENA KWENYE PRESS KAMA ALIVYOTAMKA NI DHARAU YA HALI YA JUU KWA IMANI ZA WATU

Jr
 
Tatizo papara viongozi wengi wa Serikali wanakuwa wepesi kutoa matamko haraka haraka bila kufanya uchunguzi wa kina kwanza

Nilimshangaa Simbachawene nikasema huyu naye vipi si atulie kwanza na mkuu wa mkoa naye nikamshangaa

Matukio yakitokea ukisema tunaendelea na uchunguzi tutatoa taarifa kamili tukishakamilisha Kuna shida gani?
Mambo makubwa yakitokea viongozi wajifunze kutulia kwanza sio unatoka Kama alivyotoka Simbachawene na huyo mkuu wa mkoa na kuanza kukebehi imani za watu

Imani ya mtu ni kitu nyeti kiongozi wa Serikali anatakiwa kuwa makini nacho
Imani za.kitapeli zinaruhusiwa?
 
NDIO KWA KUTUKANA WATU WA MUNGU MAKANISA YAO KUITA VIBANDA IMANI SIJAPENDA tena MBELE YA PRESS CONFERENCE

WAO KWAO WANAONA NI MAKANISA,MA CATHEDRAL YEYE NANI KUITA VIBANDA IMANI? ANATAKIWA AOMBE MSAMAHA TENA KWENYE PRESS KAMA ALIVYOTAMKA NI DHARAU YA HALI YA JUU KWA IMANI ZA WATU
Dogo kanisa siyo matofali au mabati, kanisa ni imani katika kristo, ni sawa kuyaita mabanda umiza
 
.
KWA IMANI YAKO UKO SAHIHI NA MIMI KWA IMANI YANGU NAONA IMANI YA KWAKO NI YA KISHETANI YANGU NAIONA YA MUNGU
Screenshot_20200204-134540.jpeg

Jr
 
Kuna kitu kimemuingia huyu mama, siku ya kwanza alionekana ktk video akikemea aina ya mahubiri ya nabii. Tena alishangazwa atawezaje kutatua matatizo ya watu wengi vile kwa wakati mmoja!!, akaenda mbali zaidi kwa kusema Alichokiona pale ni biashara, kila kitu kinauzwa tena kwa bei ya juu. Maji ya 700, yanauzwa 1000. Mama ghafla kabadili msimamo wake.
Aliongea na Jiwe na kupata amri kutoka juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kapokewa ofisini na vifo mfululizo. Ukiachana na vifo vya majanga asilia ya mvua nk. Kuna haya yaliyotokana na mwenendo wa matendo ya kibinadamu

Kabla hata hatujamaliza wiki ya kwanza ya mwezi wa pili tayari tumeshapoteza Watanzania wenzetu wasiopungua 40 kwenye matukio mawili tu. La mkanyagano Moshi kwenye kongamano la kidini.. Na vijana wetu 10 wa JKT waliopoteza maisha kambini Msata..

Hili la JKT taarifa rasmi bado lakini la Moshi tayari matamko yenye kukanganya yameshatolewa na viongozi mbali mbali. Wa kwanza kutoa Tamko na ambaye ni mhusika mkuu ni Waziri wa mambo ya ndani. Na alitoa angalizo zuri kuhusu sasa kuvifuatilia hivi vibanda na mabanda ya imani na shughuli zake. Amepongezwa na wengi

Kwa mstuko wa wengi jana kwenye shughuli za kuaga marehemu waliopoteza maisha yao kwenye kongamano la kukanyaga mafuta mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alisema hakuna haja ya kuzuia shughuli kama hizo na waliosababisha mkanyagano ni vijana vibaka waliotoka nje wakitakaa kuingia ndani

Mkuu wa mkoa kajuaje kuwa walikuwa vibaka na si watu wengine wowote?
Mkuu wa mkoa hakuzungumzia kuhusu hali ya ulinzi na usalama wa eneo husika
Mkuu wa mkoa hakuzungumzia muda ulioongezeka nje ya muda wa kibali
Mkuu wa mkoa hakuzungumzia kuhusu uzembe na uwajibikaji wa pamoja kwenye swala zima.
Sana sana amemkata kalima Waziri mwenye dhamana na sasa hawezi tena kuendelea kuchukua hatua alizotaka kuchukua.
Kwa hali ilivyo hakuna atakayewajibika wala kuwajibishwa....

Je, Mwamposa ni mkubwa kuliko mamlaka? Badala ya viongozi kuungana kukemea haya yanayotendwa na hawa viongozi wa dini janja janja ndio kwanza wanahamasishwa...

Jr
DPP kaona Mwamposya hana kesi ya kujibu.

Mama Mghwira yuko sahihi na ni mkweli!
 
Kama wewe ungefanyaje na uchaguzi huo naunajua huyu nabii fake na wengineo wanawafuasi wengi
 
Taarifa ya kwanza kimsingi ilipikwa kwa sababu ya kukwepa rawama kwa vyombo vya usalama. Na hiyo ndiyo ilitumika na mkuu wa mkoa na waziri.

Tukiachana na imani, whether unaiamini au huiamini lakini maadamu kibali cha mkutano kilitoka, then jeshi halikuwajibika kulinda usalama kwenye mkusanyiko ule ambao unasemekana ulikuwa na watu zaidi ya elfu kumi.

Taarifa za watu waliokuwepo zinaeleza kuwa, mafuta yaliwekwa mageti matatu, na watu walielekezwa kupita katika mageti hayo.

Kinachowashangaza ni kwa namna gani geti moja kulitokea vurugu ilihali mageti mawili watu walipita kwa ustaarabu. Ndipo dhana kwamba huwenda kuna vijana vibaka walitokea nje kutaka kuingia ndani inapata nguvu, hii ni kwa mujibu wa mashuhuda.

Yote kwa yote, Rais ametumia busara kubwa kuelekeza kuwa mapungufu yashughulikiwe. Lakini pia Waziri awaombe radhi watanzania kwa kuita vibanda imani kwa sababu hata Martin Luther alipojitenga na RC alitukanwa matusi kama haya. Leo ni giant

Tujifunze kuheshimu kile watu wengine wanaamini na huo ndiyo uvumilivu wa kidini na kiimani
 
Vibanda imani

Jr
 
Back
Top Bottom