Pigo Kubwa Kwa Upinzani. Kabuye Ang'olewa Ubunge.

Jamani kwa kusema na EL ndio hawakuingia kwa rushwa nadhani aliteleza na alitaka huruma ya EL kwani alianza kwa kusema wabunge wote.. Huo si mchango, wangu kwa leo nasema taarifa zinasema kwamba, WABUNGE WA UPINZANI WANATAKA UCHAGUZI UFANYIKE SASA NA SI BAADAYE NA KWAMBA WATAHAKIKISHA KABUYE ANARUDI BUNGENI KWA NGUVU ZOTE. Tayari mfano umeonekana kule Chunya, wapinzani wamechukua kiti cha ubunge, na upepo ulivyo SISI EMU HAWATAKUBALI KUFANYA UCHAGUZI SASA

Sasa ule mkakati wa kusimamisha chaguzi mpaka daftari la wapiga kura liwe updated vipi tena basi?
 
Sasa ule mkakati wa kusimamisha chaguzi mpaka daftari la wapiga kura liwe updated vipi tena basi?

Masatu,

Unajua siasa ni ngumu sana na misimamo ni kitu adimu sana.

Lakini nilivyoelewa mimi Upinzani hawajagomea uchaguzi na badala yake wameenda mahakamani kutafuta haki zao. Ukienda mahakani inabidi uendelee na maandalizi mengine yote ili huko kukishindikana basi option ya pili ifanye kazi.

Wangelisema wamegoma mpaka tume ya uchaguzi iandikishe wapiga kura ningeelewa, lakini kwasasa wakiamua kuweka wagombea kwenye udiwani au ubunge ni sawa maana wanacheza karata zote.

Mkakati wa mahakamani unaendelea sambamba na maandalizi mengine.
 
Masatu hebu twambie nini kimekukuna?

Hawa jamaa walikuwa wanamuonea donge huyu mzee mimi nafikiri kambi ya upinzani inaweza kuhamia huko na kuwaibisha hawa hakina Mafisadi bila tabu yoyote maana hata Kabuye mwenyewe tu anaubavu wa kujieleza na kuwashinda hawa walioshindwa mtihani mdogo tu.

Ahh ndugu yangu we.. najivunia uhuru wa mahakama Tanzania
 
Akichangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa bungeni jana na Waziri wake, Dk Marry Nagu, mapema mwaka huu, Mzee Kabuye alingea kwa uchungu akisisitiza jinsi rushwa ilivyo kuwa waziwazi kwa watu kununua uongozi. Alimuweka Rais na WAZIRI MKUU baada ya kuona kama kalipua sana.. Lakini alikua ana maana kwamba viongozi wote wametumia rushwa. Hebu tujikumbushe alivyochangia na baadaye nitawaletea alivyochangia hoja ya Mudhihir ya kumsimamishs Zitto.

MHE. PHARES K. KABUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuongea machache. Kabla ya kuongea nina usemi aliousema Mkoloni mmoja Donald Cameroon tarehe 10/10/1926 wakati akizindua Baraza la Kwanza la Kutunga Sheria katika shule ya Aghakhan ambayo sasa hivi ni Tambaza. Alisema hivi nafungua baraza la kutunga sheria siyo kuwa mahali pa Serikali kushinikiza matakwa yake. Bali mahali pa uraia wawakilishi wa wananchi kutoa maoni yao na kusema wananchi wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisemi hivyo watu wasinielewe vibaya. Lakini inavyoonekana haijawa lakini nahofia kwamba Serikali yetu ina ikashinikiza matakwa yake katika Bunge hili kwa kutumia Chama. Sasa kama alivyosema naomba nitoe maoni pamoja na kusemea watu wa Biharamulo. Watu nitakaowasemea kwanza kwa kuwa ni Wizara ya Sheria ni Mahakama. Mahakama ya Wilaya ya Biharamulo, miaka yote ya uhuru haipo. Hakimu wa Wilaya anafanyia kazi kwenye gofu la wodi la wanawake katika Hospitali ya wakoloni iliyojengwa miaka zaidi ya 100. Shahidi ni Mheshimiwa Kimiti alipokuwa Mkuu wa Mkoa amekemea, amejitahidi lakini ameacha hivyo hivyo mpaka leo hakimu wa Wilaya anafanyiakazi kwenye iliyokuwa wodi ya wanawake. Bahati mbaya hata Jaji anapokuja anakaa pale pale kufanya mambo.

Hii mimi naona kama ni aibu, kwa nini tumejenga Bunge la namna hii zuri tusiende chini ya mti kukaa? Ni shauri ya maudhui. Kama tungekuwa chini ya miti ndiyo tunge-discuss lakini ndipo watu wangetuheshimu kwamba kweli hapa sheria itatungwa? Hivi kweli hakimu chini ya mti atatoa haki? Chini ya gofu la wodi ya wanawake. Naomba sana sina matatizo na Mheshimiwa, lakini naomba uniambie Mahakama ya Wilaya ya Biharamulo itajengwa lini ili watu watoke kwenye gofu la wodi ya wanawake? (Makofi)

Hakimu wa Wilaya hana nyumba anapanga. Kupanga kuna matatizo huyo anatoa haki hivi akipanga kwenye nyumba ambako wanapika gongo kesho yule mtu atashikwa na gongo atamhukumu si siku hiyo atamwambia toka na kwenye nyumba yangu? Ni matatizo tunawapa hawa. Miaka yote hiyo hivi kujenga mahakama na nyumba ya hakimu inachukua muda gani mbona mambo makubwa tumeyafanya lakini kwenye Mahakama za Wilaya. Sasa ukija kwenye Mahakama za Mwanzo, Biharamulo ina mahakimu wawili na kwa mwaka mzima Mheshimiwa Waziri, amekarabati jengo la Buselesele Wilaya ya Chato. Kweli wananchi tunawatakia wapewe haki kama watoa haki wenyewe hawakupewa haki, hiyo haki wataitoa kwa namna gani? (Makofi)

Yuko hakimu mmoja amehamishwa kutoka Muleba kuja Chato wao wanahesabiwa shilingi 150 kwa kilomita kwa mzigo wakati wakatumishi wengine kama wanajeshi wanapewa magari, wanapewa fedha za mizigo lakini huyu anahesabiwa shilingi 150 per kilometa per mzigo. Hawa ni watoa haki ambao tunastahili kuwaheshimu? Mtu anaweza hata akamhukumu Rais unamfanya hivyo? (Makofi)

Sasa nimesema machache, naomba niseme kubwa ambalo linanikera. Mwenzangu amelisema lakini nikiongezea si vibaya. Ndugu zangu rushwa. Rushwa ya siasa, zamani kuku walikuwa hawajisaidii wanapolala, wanachunga sana. Lakini siku moja ikatokea jogoo likajisaidia hapo hapo, makoo, vifaranga vikasema kumbe tunajisadia na hapa wanajisaidia, vikaanza kujisaidia pale. Sasa wewe jokoo mwanasiasa unapotoa rushwa unafikiria wengine wafanye nini, wewe si jogoo umeshajisaidia pale pale. Kama Mwenyezi Mungu angesema Wabunge walioingia kwa kutoa rushwa wafe naamini ningebaki Kabuye Haki ya Mungu. Wote mtakufa. Sidhani kama wapo wengine.

Labda kama Rais na Waziri Mkuu, lakini nina mashaka ni aibu na mnasema tuna heshima, heshima gani mataifa yanatuona tunatoa rushwa kununua uongozi. Leo hii tunayemuenzi Marehemu Nyerere akifufua mnakimbia nawaambieni. Mnamuenzi kwa maneno tu, rushwa imekithiri mnanunua uongozi mbaya sana. (Makofi)

Halafu wewe unanunua uongozi, mmoja nikamwambia mbona ndugu yangu anatoa rushwa akasema ninyi wanasiasa mambo yenu yanapopinda mnayanyoosha wakasema eeh, ninyi wanasiasa mambo yenu yanapopinda mnayanyoosha kwa takrima. Sisi tunaponyoosha ni rushwa ndugu zangu. Nchi hii tumeiweka pabaya mno. Chunga rushwa ni kansa, ni mdudu anayekula Tanzania na kesho na kesho kutwa Tanzania itatoweka. Kama hatuangalii rushwa ya uchaguzi mbaya sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine haki za binadamu zikoje kama kweli katika nchi inayosifiwa....

MHE. GOSBERT B. BLANDES: Mwongozo wa Spika.

MWENYEKITI: Mwongozo Mheshimiwa Blandes, kanuni.

MHE. GOSBERT B. BLANDES: Mheshimiwa Mwenyekiti, kanuni ya 50,000 kifungu cha kwanza kinasema ni marufuku kabisa kusema uongo Bungeni kwa sababu hiyo Mbunge yeyote anapokuwa akisema Bungeni atawajibika kuwa na hakika kwamba maelezo anayotoa ni sahihi na siyo mambo ya kubuni au ya kubahatisha tu. Spika au Mbunge yeyote anaweza kumdai Mbunge huyo atoe uthibitisho wa usemi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msemaji anaendelea kuzungumza Mheshimiwa Kabuye ametoa maneno ambayo ni mazito sana katika Bunge letu hili tukufu kwamba kuna watu wanaonunua uongozi isipokuwa yeye peke yake. Sasa nilikuwa namtaka Mheshimiwa Kabuye athibitishe usemi wake huo mzito. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kabuye kabla sijatoa mwongozo wangu.

MHE. PHARES K. KABUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo nililitegemea. Mimi ninao ushahidi ninaweza nikaleta watu wa Biharamulo waliopewa rushwa na wanaohakikisha kwamba mimi sikutoa hata pipi. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Blandes ameeleza vizuri kwa sababu usemi wako ni mzito kwamba wote humu ndani hata mimi Mwenyekiti, hatujaingia sawa sawa isipokuwa wewe peke yako. Sasa Waheshimiwa Wabunge, wanahisi hujawatendea haki. Muongozo wangu ni kwamba uliweke vizuri jambo hili kwa kulifuta.

MHE. PHARES K. KABUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kulazimishwa ninaomba kufuta usemi. (Makofi/Kicheko)

Tunakuja kwa mauaji ya holela nayo muwe tayari kutoa hoja zenu. Tunayo sifa yetu kwamba kweli tunaangalia haki za binadamu lakini ni katika nchi hii ambayo binadamu anauwawa na mwili wake unachomwa hadharani. Binadamu anadhalilishwa kwa tuhuma zizoweza zikathibitika lakini Serikali inasema ni wananchi wenye hasira.

Hawa wananchi wanakaa mbinguni? Mtu amechomewa hapo viongozi, Mwenyekiti wa Kitongoji yupo hata yule aliyesema ameibiwa hawezi akasaidia Serikali, tunatukanwa na watu wanaopita na matrela, wanakuta moshi, wanakuta mtu anawaka wanatuambia sisi tunapokuja kwenye Mabunge wanasema nini mmefika pabaya kabisa.

Mwingine alisema kwamba wazungu wanatuheshimiwa hawatusemi vibaya kwa kuwa tumewapa dhahabu wanachimba na kila kitu tumekuwa marafiki. Lakini vinginevyo hali yetu ni mbaya. Binadamu anauawawa na kuchomwa, wako wengi wameshachomwa na kuuwawa. Lakini Serikali haisemi. Ni watu wenye hasira, hivi sisi tukisema tuna hasira Rais atoke kwenye Ikulu, atatoka tumekasirika ataondoka, si tutakipata cha mtema kuni. Lakini watu wenye hasira wanaua watu na wanawachoma hawawezi kupatikana. Lazima pia tuliangalie pamoja na wimbi la ujambazi vijana wetu wanapofanyakazi lazima waangalie inaweza ikatokea kabisa kwa kusingizia ujambazi mtu akauawawa, tumeua jambazi. Lakini nakumbuka Mkoloni mahali ambapo uhai wa mtu umetoka lazima upelelezi upite kuhakikisha kwamba kweli hili ni jambazi na hili jambazi lilikuwa linapigana? Nakumbuka Mkoloni kama unapambana na adui ukimpiga mgongoni rasasi ni kesi alikuwa anakimbia, mpaka umpige kifua. Lakini sisi ambao tumejitawala ni watu wetu leo hii binadamu hana thamani. Unaweza ukakuta unachanja kuni kwenye msitu ukabambikiziwa huko huko wakatangaza wameua jambazi. Penyewe mkitaka ushahidi naweza nikaleta.

Ndugu zangu sheria lazima iangalie, sheria inalinda watu, watu wanauawawa hivyo na kuchomwa moto. Akina bibi wanaosingiziwa uchawi wanauwawa. Mkoa wa Shinyanga karibu kila mwaka bibi kama 500 wanaondoka lakini Serikali hii inayojidai inapenda watu iko hakuna linalofanyika. Je, hao waganga ambao ndiyo wanachonganisha watu..........

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo.

MHE. PHARES K. KABUYE: Sawa leo ni kazi yangu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli kwa ninayo heshima kubwa kwa mzee wangu Mheshimiwa Kabuye nimevumilia sana lugha yake aliyokuwa akiitumia katika mchango wake toka alipoanza na ninashukuru Mheshimiwa Blandes aliweza ku - intervene pale alipoweza kutoa hoja ya kufuta usemi wake. Lakini kila anapozidi kuendelea anazidi kutoa kauli ya kuudhi. Kwa hiyo, namuomba atumie maneno ambayo ni ya busara ambayo yanatakiwa kutumika katika Bunge hili tukufu. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kabuye ni kanuni ile ile ni mwendelezo pale pale, kutumia lugha ambazo ni za ujumla na zinazoudhi. Sasa mara ya kwanza nilikuvumilia kidogo kwa sababu umri kidogo nikaona labda leo umeamka tofauti kidogo. Uendelee kuchangia lakini kwa lugha inayokubalika lugha ya Kibunge, vinginevyo unilazimisha kukukalisha chini. Malizia dakika zako.

MHE. PHARES K. KABUYE: Katika kutetea watu, siyo kukalishwa tu, watu unaweza hata ukafukuzwa Ubunge.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kabuye, kaa chini. Tatizo unaendeleza mjadala na ubishi dhidi ya kiti kitu ambacho ni kuvunja kanuni zaidi. Ukishapewa mwongozo unafuata mwongozo unatumia haki yako ya kidemokrasia ndiyo maana Mwenyekiti, yuko hapa. vinginevyo ingekuwa ni nyumba ambayo haina Mwenyekiti hapa kila mtu anajisemea tu. (Makofi)

MHE. KABUZI F. RWILOMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo. Kanuni ile ile ya 51 ya kutosema uongo Bungeni. Mheshimiwa Kabuye amesema wakongo/wazee karibu 500 wanauwawa Shinyanga kila mwaka, nadhani kwa sisi tunayotoa maeneo hayo ni hali ya wasiwasi sana, naomba afute kauli hiyo. Kweli mauaji yapo lakini siyo kiasi kile. Labda athibitishe kama kuna vikongwe 500 wameshauwawa. (Makofi)

MHE. PHARES K. KABUYE: Naomba utaniongezea muda wangu unaopotea. Nilisema kwamba vikongwe karibu 500 kila mwaka wanakufa na kuna mahali niliposoma. Lakini hata hivyo kwa heshima ya Mwenyekiti na ndugu yangu jirani Rwilomba nafuta usemi. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo kwamba leo nimeamka vibaya ni uchungu na kama mzee kuna wakati unakaripia watoto mahali popote. Lakini pengine unaweza kwa uchungu ndiyo maana mtu anapofiwa hajui machozi yanatoka wapi. Kwa hiyo, ni uchungu na sijawahi kufanya hivyo. Unapoona mtu anakufa mimi nimewahi kuona mtu anakatwa kwenye sherehe, tunakula mama amekwenda kuchukua kingine anatoka nje na sahani ya vyakula anakatwa shoka na ilikuwa Bwanga. Kama hilo linaendelea na kweli watu inapaswa wote tusikitike ndiyo maana wakati mwingine unaweza ukasema kwa hasira na pengine ukavuka mipaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba sana tuangalie haki za watu na kama kitu wanakipenda tukiangalia kuna vijana wanahangaika kutafuta riziki kwa kutumia pikipiki, kwa kutumia baiskeli, lakini sheria inasema hivyo vifaa havistahili kufanyabiashara. Inawezekana wakati sheria inatungwa watu walikuwa hawajaingia kwenye ujasiriamali leo wanatafutia mahali ambapo hata angelikuwa na fedha ya kulipia gari, gari haliendi lazima atumie baiskeli na atumie pikipiki. Vijana wengi wameshapata hasara kwa sababu wamekula mikopo ya pikipiki leo hii wameambia pikipiki hazibebi, sijui hiyo mikopo watailipaje. Hapa Serikali yetu tukufu ilisema kwamba italiangalia hilo jambo, lakini naona muda unakwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna vyombo vya Serikali wakati mwingine vinanyanyasa watu. Nimeshuhudia kabisa mtu anayetuhumiwa uhalifu anashikwa mkanda ananing'inizwa kwetu tunaita Tanganyika Jeki. Mtanzania aliyepata uhuru karibu miaka 50 ananing'inizwa kwenye Tanzania Jeki hajabainika kwamba amekosa, ni mtuhumiwa tu, licha ya kupigwa. Nalo hilo watu watanikalisha chini lakini watu wanapigwa. Eti upelelezi, ili akiri makosa, wengine wanakiri baada ya kupigwa ili aweze kujiokoa. Nalo hilo lazima liangaliwe. (Makofi/Kicheko)

Lakini naomba kwa kuwa rushwa ilianzia kwetu wanasiasa nadhani imezagaa. Mimi nikipanda basi nalo muwe tayari kunikalisha, ukifika Kibaha basi limejaa, unavikuta vi-hiace wanapunguziwa watu kwenye hivyo vi-hiace ili iweze kupita kwenye mzani sawa sawa. Unajiuliza hawa watu wa mizani hili hawalioni nalo mtataka ushahidi. Pale kuna DC, kuna OCD, miaka yote wanapunguzia kwenye hiace hawa hawaoni? Ukienda Kahama karibu na mwenzangu yule anasema bibi vizee hawafi unapunguziwa kwenye Hiace unajiuliza hapa kuna DC, hapa kuna kila mtu vipi? Kwa hiyo hili mliangalie siyo mambo ya kuchezacheza. Kuna wakati hapa tutafukuzana kwa kusema kwa uchungu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. (Makofi)
 
Ahh ndugu yangu we.. najivunia uhuru wa mahakama Tanzania

Kwa taharifa ya Kabuye aliyoitoa Bungeni alisema hata pipi hakutoa! Sasa unauhakika gani kuwa Mahakama hajaingiliwa na Wakubwa?

Au sijaelewa uhuru unaozungumzia?

Ulishafika mahakama za tanzania? Je unajua kuwa Dito amepitia kwenye mahakama hizo hizo?
 
Kwa taharifa ya Kabuye aliyoitoa Bungeni alisema hata pipi hakutoa! Sasa unauhakika gani kuwa Mahakama hajaingiliwa na Wakubwa?

Au sijaelewa uhuru unaozungumzia?

Ulishafika mahakama za tanzania? Je unajua kuwa Dito amepitia kwenye mahakama hizo hizo?

Huyo ni msema pweke!
 
kama Edward hosea anasema maneno ya Rais ndio muongozo wa kazi yake,unategemea kwa majaji wa mahakama itakuwa vipi?same thing

Hapana unapotoka, bosi wa PCCB anariport kwa rais, na hiki cheo mpaka sasa hakiko kwenye katiba, na wadau walitaka iwe hivyo...

Jaji Mkuu anateuliwa na rais lakini anaapa kwa Jamhuri sio kwa Rais...

Acha kudanganya watu!!!
 
Kwa taharifa ya Kabuye aliyoitoa Bungeni alisema hata pipi hakutoa! Sasa unauhakika gani kuwa Mahakama hajaingiliwa na Wakubwa?

Au sijaelewa uhuru unaozungumzia?

Ulishafika mahakama za tanzania? Je unajua kuwa Dito amepitia kwenye mahakama hizo hizo?

Kakindomaster,

Hatuna ukweli wote juu ya hili na kuanza kuilaumu mahakama bila ushahidi wowote ni kosa kubwa sana.

Hata hilo unalolisema la Ditto, waliocheza mchezo mbaya ni serikali wala sio mahakama.

Kwa kiasi kikubwa mahakama na hasa mahakama kuu kwa TZ zina uhuru wa kutosha kuamua mambo yaliyo mengi kwa haki.

Huenda rushwa ni tatizo kwa mahakama kuliko vitisho vya serikali.

Sheria mara nyingi inawabana watu wema maana wanakuwa hawajajiandaa kudanganya. Huenda mheshimiwa naye kakumbwa na upande huo wa msumeno.
 
Baada ya Mudhihir kuwasilisha hoja ya kutaka Zitto afungiwe, miongoni mwa wachangiaji alikuwamo mzee Kabuye, habu tuone alivyochangia hoja hiyo:

MHE. PHARES K. KABUYE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi niseme machache. Mheshimiwa Spika, mimi nashindwa kusema kwamba kasema uongo na huo uongo kwamba ni mkubwa. Amehoji mkataba kusainiwa London na ni kweli na hakuna aliyekwishakwenda kuona kwamba yale yalikuwa safi au hapana. Yote aliyoyasema, nadhani wengine tumesema si kweli, hapa tumegawanyika. Kuna aliyesema ni kweli, lakini na sisi tukasema si kweli. Lakini, yeye alileta hoja, katoa taarifa kwamba nitakuja nitaleta hoja. Hoja ameileta, kama inaonekana ameshindwa, hivi shitaka linazua lingine pale pale? (Kicheko)

SPIKA: Mheshimiwa Kabuye, unaturudisha nyuma. Tunafuata Kanuni. Kesho na keshokutwa tutazungumza upungufu na jinsi ya kuboresha Kanuni zetu. Sasa hapo, unaweza kuyazungumza na tukarekebisha. Lakini, sasa hivi hizi ndio Kanuni tulizonazo hazijabadilishwa na ya 59(iii) inamruhusu Mbunge bila taarifa kusimama na kutoa hoja kwamba Mbunge mwenzie aadhibiwe kwa kiwango ambacho atakitaja kwa sababu alichokifanya au kukinena kabla huyo mhusika, Mbunge kimeathiri heshima ya Bunge. Sasa wewe jadili hilo.

MHE. PHARES K. KABUYE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwanza mtu, si mahakamani, lakini mtu anaweza akajiuliza Bunge ni Waziri? Waziri anaweza akasema nimevunjiwa heshima, akatoa hoja! Maana ya Bunge ni nini? Kamsema mtu na mtu huyo hajalalamika, sasa kavunjia Bunge heshima namna gani?
Mheshimiwa Spika, lakini naomba tu niseme kwamba uamuzi wa watu wengi unakuwa hivyo kwa sababu, utanisamehe, wakati najifunza Literature, nakumbuka mambo ya Socret, alisema (msinichukulie kwamba nawasema) "kwamba ninyi mwafanya hivyo mkifikiri kwamba mtakwepa kutoa hesabu ya maisha yenu, bali mimi nawaambia kwamba matokeo yatakuja kinyume chake, watu wengi watawataka kutoa hesabu ya maisha yenu nao watakuwa vijana zaidi kuliko mimi. Na ninyi mtawakasirikia sana"

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo uamuzi wa wengi…aliposema hiyo, wakampigia kura, alipojaribu kujieleza, hata kura zikapungua. Kwa hiyo, uamuzi wa namna hiyo, ninaomba kama ingekuwa Kamati ikakaa, ikachekecha, tungepewa kwamba kweli ukubwa wa uongo unalingana na huu au uongo haupo. Lakini, kwa sababu ni umati, uamuzi wa watu wengi, eeh, hapa ni mambo mengi. Kwa hiyo, mimi ninaomba mwisho kwamba angepewa fursa ya kutafuta hivyo vielelezo, inawezekana hakujua kwamba mambo yangelifika hapa. Nakushukuru sana!
 
Oh basi kweli wameamua kuuwa upinzani jamani. Jopo la wanasheria msaidieni huyu mzee aliyeweza kuingia bungeni bila hata punje ya rushwa.

Na kama ni kumzalilisha mtu inahusiana vipi na ubunge?
 
Kwa kiasi kikubwa mahakama na hasa mahakama kuu kwa TZ zina uhuru wa kutosha kuamua mambo yaliyo mengi kwa haki.

Waooo Mtanzania,

take time kuhudhuria kesi za mahakama za mwanzo hadi mikoa uone ukweli au uhakika wa statement yako, naweza kuamini mahakama kuu kwa sababu hata huko ni kesi chache za walalahoi zinafika..

Tatizo liko kwenye mahakama za chini ambazo nyingi haki hupunjwa hadharani..... statement yako iko very loaded mkuu.....
 
Waooo Mtanzania,

take time kuhudhuria kesi za mahakama za mwanzo hadi mikoa uone ukweli au uhakika wa statement yako, naweza kuamini mahakama kuu kwa sababu hata huko ni kesi chache za walalahoi zinafika..

Tatizo liko kwenye mahakama za chini ambazo nyingi haki hupunjwa hadharani..... statement yako iko very loaded mkuu.....

Mwafrika wa Kike,

Ndio maana nikaweka hasa mahakama kuu.

Hata mahakama za mwanzo tatizo kubwa ni uoga wa mahakimu pamoja na rushwa. Vitisho vya serikali nafikiri vinachukua nafasi ndogo.

Sheria zetu ndio mbaya na ndio zinawapa watawala nafasi kubwa ya kufanya watakalo na mahakama zipo kutekeleza hizo sheria.
 
Mwafrika wa Kike,

Ndio maana nikaweka hasa mahakama kuu.

Hata mahakama za mwanzo tatizo kubwa ni uoga wa mahakimu pamoja na rushwa. Vitisho vya serikali nafikiri vinachukua nafasi ndogo.

Sheria zetu ndio mbaya na ndio zinawapa watawala nafasi kubwa ya kufanya watakalo na mahakama zipo kutekeleza hizo sheria.

Mtanzania

Hapo nakubaliana na wewe kabisa kuhusu mahakama za mwanzo. Pia na kuhusu sheria zetu. Hila generally ukitoa mahakama kuu hali ya mahakama nyingine ni mbaya.

Sina uhakika huyu mzee kesi yake imesikilizwa wapi? Labda tutapata data kadri muda unavyoendelea.
 
Mtanzania

Hapo nakubaliana na wewe kabisa kuhusu mahakama za mwanzo. Pia na kuhusu sheria zetu. Hila generally ukitoa mahakama kuu hali ya mahakama nyingine ni mbaya.

Sina uhakika huyu mzee kesi yake imesikilizwa wapi? Labda tutapata data kadri muda unavyoendelea.

Kwa msingi huo hukumu ya mahakama kuu kutengua matokeo ya Biharamulo ni ya haki.....
 
Jamani kwa kusema na EL ndio hawakuingia kwa rushwa nadhani aliteleza na alitaka huruma ya EL kwani alianza kwa kusema wabunge wote.. Huo si mchango, wangu kwa leo nasema taarifa zinasema kwamba, WABUNGE WA UPINZANI WANATAKA UCHAGUZI UFANYIKE SASA NA SI BAADAYE NA KWAMBA WATAHAKIKISHA KABUYE ANARUDI BUNGENI KWA NGUVU ZOTE. Tayari mfano umeonekana kule Chunya, wapinzani wamechukua kiti cha ubunge, na upepo ulivyo SISI EMU HAWATAKUBALI KUFANYA UCHAGUZI SASA

Nani kachukua ubunge Chunya? Tuhabarishe tulioko mbali.
 
Back
Top Bottom