Pigo Kubwa Kwa Upinzani. Kabuye Ang'olewa Ubunge. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pigo Kubwa Kwa Upinzani. Kabuye Ang'olewa Ubunge.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Oct 12, 2007.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kwa taarifa zilizonifikia hivi punde ni kuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo mh.mzee Phares Kabuye , ameng'olewa kwenye kiti chake cha ubunge asubuhi hii ya leo.

  Mahakama kuu kanda ya Kagera imetoa uamuzi kuwa ameshindwa kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na mgombea wa ccm na hivyo kutangaza kuwa amekosa sifa za kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo.

  Kwa taarifa zaidi ni kuwa anaendelea na utaratibu wa kukata rufaa na sijui hali itakuwaje ila nitaendelea kuwahabarisha zaidi hapo baadae.

  Hili ni pigo kubwa kwa upinzani kwani huyu mzee aliweza kumkaba kwelikweli Karamagi wakati anatetea ufisadi wake wa kusaini mkataba nje ya nchi.

  Je?huu ni mwanzo wa kuwapunguza wabunge wa upinzani?
  Je?wananchi watachukua uamuzi gani kwani huyu mzee aliendesha kampeni zake kwa kutumia baiskeli halafu anashitakiwa kwa rushwa.
   
 2. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kosa la pili ni kuwa alimdhalilisha mtu wakati wa kampeni ,sasa hapo ndio wajuvi wa mambo mtueleze aliweza je kudhalilisha wakati akiomba kupewa kura?
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  MK,

  Badala ya kuwafuta ubunge walioupata kwa kura za wizi na kuhonga, wanawafuta ubunge watu ambao wameupata kwa sera
  maana hawakuwa na vyombo vya dola nyuma yao vya kuwasaidia.

  Ninachombea mimi ni kwa huyu mheshimiwa kutokukosa sifa ya kugombea tena maana kwa mazingira ya sasa uchaguzi ukirudiwa nina uhakika anaweza kushinda tena.
   
 4. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  tena atashinda kwa kishindo
   
 5. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2007
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Inauma sana hii. Nadhani inafaa wapinzani wakaungana kumsaidia kugharamia rufaa, maana nijuavyo kuna uwezekano alikuwa anajitetea mwenyewe. Huyu mzee ni mwalimu mstaafu na ana msimamo sana na mambo ya msingi. Alifanya kampeni huko Biharamulo akiwa hana hela, hata usafiri alitumia baiskeli. Naamini hata wananchi walimchagua kwa kumpenda kwa dhati, ni mtu mwenye kujitoa. Inawezekana ametungiwa hiyo kesi, mawakili wakacheza na vipengele vya sheria, ikawa kama anavyotuhabarisha MK. Na chama anachotoka ni maskini wa kutupwa katika rasilmali zote tunazojua (fedha, watu, mali n.k). Nadhani asaidiwe huyu mzee, itakuwa ni kuwasaidia wananchi wa Biharamulo kama huyu mzee atabaki bungeni.
   
 6. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ni kuwa aliambiwa aqmemdhalilisha mgombea wa ccm ,

  Nimepewa taarifa kuwa wapinzani wanakutana na pia mawake wako mbioni kuweka court injuction ili kuzuia utekelezaji wa hukumu hiyo.

  Najaribu kuwasiliana na wakili aliyekuwa upande wa utetezi ila ananiambia yupo bize hivyo nimeamua kumpa nafasi ya kukata rufaa kwanza na kuwza kuzuia utekelezaji wa hiyo hukumu.
   
 7. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  naomba Tundu Lissu afikishiwe suala hili,aangalie je nis heria zipi zimetumika,zitto kama uko online naomba utusaidie kwa hili
   
 8. B

  BroJay4 JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2007
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapa inabidi tupigane kiume,huyu mzee alitoa issue moja bungeni hadi leo hii sitamsahau,hapana,inabidi haki itendeke.
   
 9. ram

  ram JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,210
  Likes Received: 909
  Trophy Points: 280
  Siamini! Hapa nimekuwa mdogo kama piliton,hata cha kusema sina lakini Mungu yupo atampigania tu
   
 10. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2007
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 35
  Hili ndio tatizo la mafisadi hawapendi kushindwa, mzee Kabuye kwa kweli kung'olewa ni mbaya sana. Hapa rufaa ni ya muhimu sana kwa kambi ya upinzani
   
 11. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  mwanakijiji fanya mawasiliano na Shemeleza pharles Kabuye wikiendi hii ili umuhoji katika KLh news,aeleze jinsi hawa mafisadi wanavyotaka kumuaibisha
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Na kuna yeyote anaweza kunifafanulia mgawanyo wa madaraka na majukumu ktk nguzo za serikali??? isije ikawa mpaka majaji wanapewa maelekezo kutoka juu.

  Labda pia wale majaji wapya walioteuliwa ni makada halisi wa chama dume hivyo hata rules zitakuwa zinafavavour watu fulani.

  Kabuye ni mwanasiasa makini anayesimamia ukweli na anaishi ktk maneno yake na kubw zaidi anamuenzi baba wa taifa..

  Namuoombea ashinde ktk rufani yake.
   
 13. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  kama Edward hosea anasema maneno ya Rais ndio muongozo wa kazi yake,unategemea kwa majaji wa mahakama itakuwa vipi?same thing
   
 14. m

  macinkus JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2007
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kosa Kubwa Alilifanya Kabuye Ni Kwenye Bunge Lililopita. Alisema Ni Yeye Peke Yake Na El Ndio Walipata Ubunge Bila Kutoa Rushwa !!!
   
 15. J

  Judy Senior Member

  #15
  Oct 12, 2007
  Joined: Aug 13, 2007
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Whats wrong with that kama ana uhakika na anachokisema? hawa mafisadi wanamtoa kafara tu. Ndio walewale majaji wao, pccb wao, hakuna haki kabisa. But yana mwisho, your dayas are numbered.
   
 16. M

  Masatu JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Teh teh teh teh teh...
   
 17. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2007
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Masatu hebu twambie nini kimekukuna?

  Hawa jamaa walikuwa wanamuonea donge huyu mzee mimi nafikiri kambi ya upinzani inaweza kuhamia huko na kuwaibisha hawa hakina Mafisadi bila tabu yoyote maana hata Kabuye mwenyewe tu anaubavu wa kujieleza na kuwashinda hawa walioshindwa mtihani mdogo tu.
   
 18. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hahaaa, ndio siasa hiyo !
   
 19. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Jamani kwa kusema na EL ndio hawakuingia kwa rushwa nadhani aliteleza na alitaka huruma ya EL kwani alianza kwa kusema wabunge wote.. Huo si mchango, wangu kwa leo nasema taarifa zinasema kwamba, WABUNGE WA UPINZANI WANATAKA UCHAGUZI UFANYIKE SASA NA SI BAADAYE NA KWAMBA WATAHAKIKISHA KABUYE ANARUDI BUNGENI KWA NGUVU ZOTE. Tayari mfano umeonekana kule Chunya, wapinzani wamechukua kiti cha ubunge, na upepo ulivyo SISI EMU HAWATAKUBALI KUFANYA UCHAGUZI SASA
   
 20. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Halisi,

  Katiba iko wazi kuhusu uchaguzi wa bunge wala sio CCM au serikali ambao wanaweza kuzuia hili.

  Sehemu kubwa itategemea na mbunge mwenyewe kama anataka kukata rufaa.

  Inabidi kujua hukumu inasema nini maana huko nyuma kuna watu walipoteza ubunge pamoja na haki ya kugombea ubunge. Hili ndilo la kuliogopa.

  Kama wamemvua ubunge tu nafikiri njia nzuri ni yeye kusema haendi mahakamani na badala yake anarudi kwa wananchi.

  Kwa nguvu ya sasa ya upinzani, pamoja na mbunge mwenyewe alivyo, nina uhakika atashinda tena jimbo lake.
   
Loading...