Pigo jingine kwa wasiojulikana: Waporomoshwa vyeo wote

Ex Spy

JF-Expert Member
Jan 15, 2007
213
1,726
Wameondolewa rasmi kwenye nafasi za juu na kupelekwa wilayani kama Field Officers.

Wamenyang’anywa magari ya kifahari ambayo yalikuwa yanawapa viburi mjini na sasa wanaugulia maumivu.

Tutarajie mabadiliko chanya katika taasisi? Tuwape muda!
 
wewe Ex Spy kama uko hapa kufanya crisis management ya TISS nenda kamuambie yeyote aliyekutuma kwamba namna pekee inayoweza isafisha serikali hii na uchafu wa kuhusika na utekaji pamoja na mauaji yanayofanywa na hao wasiojurikana ni kumuondoa Bashite.

Hata kama hausiki, aondolewe Bashite awa akina kapilimba wanaonewa tu.
 
Watu pekee wanaoweza kuwapa raha Watanzania (kuikomboa nchi hii) ni TISS,enyi TISS tupeni raha ,Tufanyeni tuwe watu wenye furaha hapa Duniani,Watanzania huwa muda mwingi hatuna raha.Nyie ndio mnaweza kuikomboa nchi hii,nyie tendeni kazi zenu kwa manufaa ya wengi,.Tuko milioni zaid ya 40 WENGI HATUNA RAHA.sikilizeni kilio cha wengi.
 
Wameondolewa rasmi kwenye nafasi za juu na kupelekwa wilayani kama Field Officers.

Wamenyang’anywa magari ya kifahari ambayo yalikuwa yanawapa viburi mjini na sasa wanaugulia maumivu.

Tutarajie mabadiliko chanya katika taasisi? Tuwape muda!

Hata kama wataletwa watu wengine wapya kabisa kwenye Taasisi hii ya TISS, lakini kama Sheria, Kanuni, Miongozo NA Taratibu mbalimbali zinazotumika ktk. Usimamizi NA Uendeshaji wa Shughuli za kila siku za Taasisi hii zikabaki hivi hivi kama zilivyo sasa, hakuna cha mabadiliko chanya yanayoweza kutokea.

Ni ndoto za Alinacha, wala tusitarajie mabadiliko yoyote Chanya kutokea ktk Taasisi hii endapo kama Sheria na Kanuni zilizopo hazitabadilishwa.

Kumbukeni ya kwamba " daima maji hufuata mkondo".

Kamwe, Maji hayawezi kwenda tofauti na mkondo wake.

Hicho kinachofanyika sasa ni sawa na kubadilisha chupa ya mvinyo, wakati mvinyo yenyewe imebaki kuwa ile ile na ukali wake ule ule wa miaka yote.
 
Wameondolewa rasmi kwenye nafasi za juu na kupelekwa wilayani kama Field Officers.

Wamenyang’anywa magari ya kifahari ambayo yalikuwa yanawapa viburi mjini na sasa wanaugulia maumivu.

Tutarajie mabadiliko chanya katika taasisi? Tuwape muda!
Ama wewe ni mmoja wa kitengo cha propaganda, au hujui wanasiasa wanavyo cheza na akili zetu. Tunaelekea kwenye uchaguzi. TISS ni kitengo ambacho nipo maskioni mpaka kwa mtoto ambaye hajaongea. Si kwa sifa nzuri, bali ujambazi wa kidola. Yote yafanyika ni kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Ni wale wale, leo mpaka dahali.
 
Watu pekee wanaoweza kuwapa raha Watanzania (kuikomboa nchi hii) ni TISS,enyi TISS tupeni raha ,Tufanyeni tuwe watu wenye furaha hapa Duniani,Watanzania huwa muda mwingi hatuna raha.Nyie ndio mnaweza kuikomboa nchi hii,nyie tendeni kazi zenu kwa manufaa ya wengi,.Tuko milioni zaid ya 40 WENGI HATUNA RAHA.sikilizeni kilio cha wengi.
Usiwape dhamana wao ni kuhakikisha CCM inashinda tu na wapinzani wanobaki ni wale mamluki tu, wajahidina wasinyanyuke popote walipo
 
Back
Top Bottom