Piga Kura: Mchezaji Bora wa JF kwa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL)

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,087
103,318
Kama kawaida wanaJF hakuna kinachotupita. Ligi kuu Tanzania Bara inaelekea ukingoni huku Simba ikijichukulia ubingwa kwa rekodi ya bila kufungwa.

Tukiwa tunaelekea ukingoni kabisa mwa ligi kuu napendekeza tupate maoni mwa mashabiki na wapenda soka wa JF,ni nani anafaa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu?

Kwa upande wangu kichwa kinauma. Wachezaji kama Okwi, Bocco,Kichuya,Kiyombo,Aishi Manula, Mkude wameonyesha kiwango kizuri sana,lakini ni mmoja tu anapaswa kuwa mchezaji bora. Piga kura mwanaJF ni nani anafaa kuwa mchezaji bora
 
JAMAA HAWA WAMEPIGA KAZI SANA
Erasto Nyoni
Gadiel Michael
Emmanuel Okwi
Kelvin Yondani
Aishi Manula
John Bocco
Mudathri Yahya
Shiza Kichuya
Shaffiq Batambuze
Asante Kwasi

kura yangu kwa ERASTO NYONI
 
Umewahi kupata majibu kwa nini Azam iliwaacha Bocco,Nyoni,Manula,Kapombe. Huwa naona ni ujuha
Mpango mkakati hao ni mamluki ili Simba iwe bingwa..na usijifanye hujui..wapi Duniani umeona unawauzia wapinzani wako key players wanne kama sio upuuzi wa wanna be Arabs
 
Back
Top Bottom