Piga kura kuchagua jina la sayari-nje ya Tanzania

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
279
202
Piga kura kuchagua jina linalofaa kwa sayarinje ya Tanzania

Sayarinje ni sayari zinazozunguka nyota ambazo zipo nje ya mfumo wa Jua.

Tanzania tumepewa fursa ya kuipa jina sayarinje mojawapo iliyogunduliwa karibuni.

Wanafunzi wa shule na wanavikundi mbalimbali wameshindanishwa kupendekeza majina ya sayarinje hiyo kwa kufuata asili na utamaduni wa Kitanzania.

Kamati ya Kitaifa ya Sayarinje imeteua majina kumi kati ya yale yaliyopendekezwa ili wewe na watanzania wengine muweze kupigia kura majina matatu tu kwa kuangalia sababu zilizotumika kupendekeza majina hayo, yakatakayotambulisha Nchi yetu angani milele.

Kupiga kura, nenda kwenye hii tovuti: PIGIA KURA MAJINA YA SAYARI-NJE NA NYOTA ZA TANZANIA (Vote for Tanzania ExoWorld Names) - Mwisho wa Kupiga Kura 14/11/19

MWISHO WA KUPIGA KURA NI Tarehe 14 Novemba 2019

Kwa msaada zaidi tuma ujumbe mfupi (SMS) au ujumbe kwa WhatsApp kwenda namba 0778 517 009 au kwa baruapepe: Assat.Astronomy@gmail.com

Tanzania Exoplanet KUPIGA KURA KUCHAGUA SAYARI-NJE YA TANZANIA=.png
 

Attachments

  • Tanzania Exoplanet KUPIGA KURA KUCHAGUA SAYARI-NJE YA TANZANIA.png
    Tanzania Exoplanet KUPIGA KURA KUCHAGUA SAYARI-NJE YA TANZANIA.png
    100.1 KB · Views: 1
Back
Top Bottom