Piga kura BBA bila kusubiri saa moja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Piga kura BBA bila kusubiri saa moja

Discussion in 'Entertainment' started by Kilongwe, Sep 21, 2010.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Piga kura mfululizo BBA bila kisubbiri saa moja

  [​IMG]
  Ni ukweli kuwa wengi wetu tutakuwa tunafahamu nini kinaendelea kule mjengoni kwenye BBA,kwani wiki hii Mtanzania pekee yupo kwenye harakati za kutolewa kama tusipokuja pamoja na kumsaidia,binafsi sio fan wa BBA ila nimeamua kuja na hili kwa ajili ya Tanzania,kwani kama mshiriki wa Tanzania akijichukulia hichi kitita basi kuna faida kwa upande mmoja au mwingine kwa Tanzania vievile itasaidia hata kulitangaza taifa letu.Ndio maana AfroIT imeamua kuja na hii mada ya leo.

  Katika siku za awali niliwahi kuzungumzia kuhusu umuhimu wa kutumia Captchar kwenye mambo ya mawasiliano ya habari,niliwahi kugusia kipengele cha kupiga kura za online na jinsi gani zinaweza kuathiriwa na watu wenye ujuzi wa mambo ya mitandao. Bonyeza hapa kama haukusoma hiyo makala.

  Sasa leo hii nitakueleza jinsi ya kuhack kura za BBA ili uweze kumpigia kura mwakilishi unayempenda bila kikwazo,tunategemea atakuwa ni mtanzania mwenzetu na ndio maana nimeandika makala hii tena kwa lugha ya taifa ili kutuwezesha sisi pekee kujifaidi na huu ndio umuhimu wa kuiwezesha lugha yetu kiteknolojia na ndio lengo la AfroIT.
  Kabla ya kuendelea,labda nikueleze ni jinsi gani mfumo wa kura za BBA zinavyoenda(ninamaanisha kura za kupiga online).

  Kila kompyuta inakuwa na anuani mbili zinazoitambulisha au kuitofautisha na nyingine,ambazo ni IP address na MAC address,huitaji kuwa mtaalam wa hivi ili kuweza kufanikisha hili zoezi.

  Sasa pindi unapologin kwenye website yoyote,hiyo website huacha kumbukumbu zao(cookies) zinazounganishwa na IP na anuani zako na vitu vingine ambapo hutofautiana toka website moja hadi nyingine.Sasa website hizo hutumia hizo cookies ili kubaini watumiaji wake,vilevile kuweza kuchunga matumizi ya website yao,Biggie naye anatumia mfumo huu huu.

  Wiki mbili ziliyopita,nilifanya majaribio katika kuhakikisha Mwisho anarejea kundini kwa kupiga kura nyiiingi kwa kutumia akaunti nyiiingi,katika majaribio yangu nikagundua jinsi gani BBA wanavyoweza kuchunga upigaji wa kura ili kukuzuia kupiga kura hadi lisaa limoja liishe kama ifuatavyo.

  Kila mtumiaji huwa na viunganishi vinavyoweza kumbaini kama amepiga kura au la na ndani ya viunganishi hivyo kuna

  1.E mail address(na sio username au details nyingine za kwenye akaunti yako)

  2.Cookies wanazozipandikiza kwenye komputa yako

  3.IP addreess ya kompyuta yako

  Sasa basi,kupambana na e mail address inawezekanika ila ni kinyume cha maadili ya AfroIT hivyo siwezi kuliweka hadharani hili na nitakuelezea sula la pili na la tatu,katika lugha laini kazi kwako itabakia ni unatakiwa kutumia e mail mbalimbali huku ikiambatana na maelekezo yanayofuata.

  Futa cookies (Bonyeza hapa kuangalia video yake kwa kiswahili! )

  Ili kuondoa utambulisho wako kwa Biggies,unatakiwa kuondoa vijifaili vyote walivyoweka kwenye kompyuta yako,ili kuweza fanya hili ni rahisi fuata hatua zifuatazo

  1.Kwenye internet explorer yako bonyeza Tools->Internet Options

  [​IMG]

  2.Delete,kutatokea kawindow kapya (Hakikisha umechagua kila kitu kama inavyoonesha kwenye picha)

  [​IMG]

  3.Bonyeza Delete

  Hapa umeshaondoa vijifaili vyote Biggie alivyoweka kwenye kompyuta yako, Sasa twende kwenye hatua inayofuata.

  Kubadili IP address

  Inatakiwa kubadili IP address ili kuondoa uhusiano wako na Biggie uliopo kwenye kumbukumbu zake,hivyo kuna njia mbili za kufanikisha hili,

  (a)Unatakiwa kurestart kompyuta yako,itakapowaka tu kuna uwezekano mkubwa ukapata IP mpya,hii ni kwa wale wasio na ufahamu mkubwa wa kompyuta

  (b) Hii ndio njia yenye uhakika mkubwa,unachotakiwa ni kufuata hatua zifuatazo(Kwa wale wenye ufahamu kidogo na Kompyuta)

  1.Nenda kwenye Start->Search programs and files. Halafu andika CMD Kwa wale wa windows XP basi Nenda Start->Run halafu andika CMD
  [​IMG]


  2.Katatokea kajiwindow/kijibox cheusi, upo kwenye kijibox cheusi andika ipconfig /renew ,hii itakuwezesha kupata IP mpya,

  [​IMG]

  NB:Maelekezo ya juu ya kubadili IP address inategemeana sana na aina ya mtandao unaotumia,kwa wale wa Static IP hii haiwahusu,kwa wale wanaoshare IP jarinu kuwasiliana na provider wako.

  Sasa,baada ya kumaliza hizi hatua kadhaa,unachotakiwa ni kujisajili kwenye website yao kwa kutumia e mails tofauti tofauti halafu kupiga kura kwa kila e mail bila kusubiri saa moja,kumbuka kubadilisha nchi unayotoka katika kila e mail ili kuongeza uwingi wa kura kwa kila nchi husika kama ifuatavyo.

  1.Baada ya kulogin,bonyeza My Profile inayopatikanika juu kabisa kulia.

  [​IMG]

  2.Chagua nchi tofauti tofauti kwa kila e mail,ila angalau nchi moja kwa kila e mails mbili ili kuongeza uwingi wa kura kwa nchi husika

  [​IMG]

  Kwa leo naishia hapa nikitegemea mutafaidika na hili.

  Source:AfroIT blog
   
 2. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  [​IMG]  Kama kijana wa kundi la MBWA MWITU wa Mbagal
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  tukipiga kura ili iweje?
   
 4. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu maelezo yako tumeyasikia japo hutatoa maelezo kwa wale watumiaji wa browsers nyingine kama Safari, Firefox etc. Na pia kwa wale wenye Static IPs na pia wenyekutumia Internet kwenye simu (mfano Opera) inakuwaje?

   
Loading...