Piga kampeni kwa simu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Piga kampeni kwa simu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Albedo, Oct 3, 2010.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kuna Watu wamekuwa wanajaribu kuufananisha Uchaguzi wa 2010 na ule wa mwaka 1995, wamekuwa wakijaribu kulinganisha Umaarufu alionao nao Dr. Slaa na Umaarufu aliokuwa nao Augustino Lyatonga Mrema alipokuwa anagombea Urais Kupitia NCCR-Mageuzi. Watu hao wanadiriki kutumia ufanano wa Umaarufu huo hata kujaribu kutabiri eti Dr. Slaa ataanguka kama alivyoanguka Mrema 1995.

  Watu hao wamejivika upofu wa Kufananisha watu hao wawili huku wakikwepa ama kwa makusudi ama kwa kutojua Tofauti ya Kimazingira kati ya Mwaka 1995 na mwaka 2010

  Kuna mambo ambayo inabidi yaangaliwe kabla ya kufananisha hali ilivyokuwa 1995 na 2010

  Mwaka 1995 technolojia ya habari haikuwa imeenea sana kama 2010, Sasa hivi karibu kila Mzazi kijijini mwenye mtoto Mjini anatumia simu ya Mkononi. Nimekuwa nikifuatailia kura za mtandaoni ambazo zimekuwa zikimpa Ushindi mkubwa Dr. Slaa dhidi ya Wapinzani wake.

  Japokuwa Baadhi ya Watu wamekuwa wakiziponda polls hizi ila kwa mtu makini hawezi kuzipuuzia hata kidogo na hata Wapinzani wa Dr. Slaa hawawezi kuzipuuzia hata kidogo kwa sababu wanatambua ni Ujumbe gani unaotolewa

  Baadhi ya Watu wanaweza kuja hapa na kutoa Hoja kwamba ni Watanzania wangapi wana access na internet? Watanzania Wangapi wanajua JF? Hizi ni Hoja Mfu zinazofanana na Mgombea mmoja wa Urais aliyena kwamba kura 350000 ni ndogo sana kwake bila kuangalia ni watu wangapi wako nyuma ya hao watu 350,000

  Ndugu wana JF wapenda Mabadiliko leo nina Ujumbe Muhimu sana kwenu

  Wanaweza kutubeza kwa Uchache wetu, wanaweza kutubeza eti hatupigi kura, Wanaweza kutubeza eti kwamba sisi ni watu wa kulalamika kwenye Mitandao, wanaweza kutubeza kwamba tunaota ndoto za mchana

  Lakini Ukweli ni Kwamba

  Sisi wana JF tuna Wazazi, tuna Wadogo zetu na kaka Zetu na hata Ndugu zetu wale wanaobezwa kwa kukosa huduma hii ya Mtandao, Lakini ndugu zetu hawa asilimia kubwa wana Simu za Mikononi

  Sasa Wana JF wote wapenda mabadiliko, wataopiga kura na ambao hawatapiga kura kwa sababu yeyote Nyanyua Simu yako Mpigie Shangazi yako, mama yako, bibi yako, babu yako, kaka yako dada yako, mjomba wako Mwambie tunahitaji mabadiliko.

  PAMOJA NA UCHACHE WETU TWAWEZA KULETA MABADILIKO, PLAY YOUR PART

  NyU
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Leo Nimeonge na watu wa Kjijini kwa kweli nimehamasika sana na mwamko wao! Nadhani hata UWT na Jeshi wameshaliona hili

  Mwana JF Play your part
   
 3. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Simu zikitumika vizuri ni silaha nzuri ya ushindi kwa CHADEMA;

  Kuna message zinatumwa kila siku za kuhamasishana kumchagua Dr Slaa na chadema.
   
 4. M

  Masauni JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfano mzuri ni huu hapa, mama yangu yuko kijijini na amehaidi kumpigia Dr.Slaa kura, wadogo zangu na kaka zangu bila kumsahau baba yangu ambaye alikuwa anasema hawezi kupiga kura lakini baada ya kuongea naye kwa simu sasa ni mfuasi mzuri sana wa Dr. Slaa
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Leo nietoka kuongea na mama mdogo hakuwa na mpango wa kupiga kura eti kisa kachoshwa na CCM, nikamwambia kama amechoshwa na CCM dawa si kuzira kupiga kura bali ni kupigia chama kingine kura, kwa kweli amenielewa akatoa kauli hii " Kama wewe mwanangu msomi unaniambia Nimpigie kura Slaa nitafanya hivyo"
   
 6. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mimi nina kaka wa 2= watampigia slaa
  baba na mama= watampigia slaa
  wadogo zangu 2= watampigia slaa
  Mimi mwenyewe slaa

  ofisini kwangu kuna watu saba, wote wanataka mabadiliko, wamechoka maisha ni magumu, na watampigia slaa

  kwahiyo nauakika kura hizi zote = 2+2+2+1+7=14, ni ZA SLAA

  Hao , wanaodharau kura za maoni za JF, waendelee, october 31, usiku baada matokeo kuanza kutangazwa, watapigwa na bumbuwazi.
   
 7. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii ni njia safi sana, nami jana nilikuwA LIFT MOJA NA WATU WENGINE KAMA TISA HIVI, NIKACHOMEKEA SWALA LA UCHAGUZI, WENGINE WALIKUWA WAKISEMA WAMECHOSHWA HAWAPOTEZI MUDA WAO KUPIGA KURA, NILIWASIHI WASIFANYE KOSA HILO,
  ILA WALINISHANGAZA WALIPOSEMA KWAMBA SAWA WATAMPA MDEE UBUNGE, SASA URAISI WAMPE NANI? ILIONISHTUA KWANI ILIELKEA WALIKUWA HAWAJUI UHUSIANO KATI YA CHADEMA, SLAA, NA MDEE! BASI NIKAWAELEWESHA NA KUWASIHI KWAMBA KURA YAO MOJA NI MUHIMU SANA!

  MY TAKE:
  JITIHADA KAMA HIZI NI MUHIMU SANA, KWANI HAO WATU NI WA DAR HII HII, ILA WALIONEKANA KUTO ELEWA, JAPO UMRI WAO HAUZIDI MYAKA AROBAINI, YAANI SI WAZEE HATA KIDOGO! AMA KWELI CCM IMETUMALIZA WATANZANIA...
   
 8. M

  MC JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Good idea, kuna watu ambao hawaelewi kinachoendelea TZ, ukiwapa taarifa kuwa chagua flani kwa sababu hii na hii wanakuelewa na wanabadili msimamo. Mimi hatanikienda Restaurant, ofisi mbalimbali na hata Bar huwa nauliza uliza wahudumu/wafanyakazi "Hivi wewe ulijiandikisha kupiga Kura"? Wengi jibu huwa ni Ndio; Je utampigia nani mwaka Huu? majibu huwa Ni Dr. Slaa au Kikwete! sehemu ambazo zimekaa 'kishule shule'/advanced watu wengi hujibu Dr. Slaa, sehemu kama Bar wahudumu hujibu Kikwete! sasa huwa nachukua kama dakika chache sana kuwashawishi ni kwa nini wasimpe kura yao Kikwete, wengi wamebadili mawazo na kushawishika kumpigia Dr. Slaa;

  Nina ndugu zangu wengi nimewashawishi, na kwa jinsi wanavyonifahamu mimi sijawahi kujihusisha moja kwa moja na chama chochote cha siasa Tanzania, kwa hiyo huwa nikiwambia Chagua Dr. Slaa na CHADEMA wengi hunielewa na kukubali, kuna mifano mbalimbali huwa ninawapa ikiwemo ya Kihistoria. Mfano, huwa naamini na nashawishi watu kuwa Tanzania yenye Maendeleo makubwa inawezekana, baada ya Kufika nchi mbalimbali na naweza kulinganisha kwa uwazi kabisa kihistoria ni kwa nini Tanzania haikutakiwa kuacha mbali na hizo nyingine, 'lazima tuwe na wivu wa kimaendeleo' mfano Singapore na Malaysia nakumbuka jinsi nchi hizo zilivyokuwa maskini kama Tanzania miaka ya Nyuma, jinsi viongozi wa Singapore walivyoamua kuwa Serious na mara moja maendeleo makubwa yakaanza kupatikana, na Malaysia wakapata Wivu wa kimaendeleo nao Viongozi wao wakaamua kuwa Serious na leo wana maendeo makubwa.

  Kwa hiyo nakubaliana na wewe, Tuitumie Technologia hii kuwapasha wengine habari Njema
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Vizuri sana Mkuu Paygod, Watu wengine ni Wavivu sana, sasa kampeni zinaisha tar 30 Oct lakini Kampeni za Simu zipapigwa hata mpaka kwenye foleni za kupigia Kura

  PIGA KAMPENI KWA KUTUMIA SIMU YAKO YA MKONONI HII NI ZAIDI YA KAMPENI YA SHUKA KWA SHUKA
   
 10. h

  hagonga Senior Member

  #10
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nina ndugu na jamaa huko kijijini, sikuwa na uhakika kama watapiga kura kwa Slaa, ilinibidi nisafiri kwenda vijijini angalau nionane nao uso kwa uso, kwa kweli nilifurahi sana maana nimewaelimisha na wamekubali na kudhamiria kwelikweli kupiga kura 31 oct kwa Dr, na pia ofisini kwetu wafanyakazi wenzangu wote zaidi ya 40 wakanihahikishia kuwa watampigia kura Dr SLaa na CHADEMA.
   
 11. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mungu akipenda ninategemea kusafiri hivi karibuni kabla ya uchaguzi mkuu huko mashariki ya kati, lakini kivumbi nilichokiacha huku nyuma, wazazi wangu n dk slaa,baba mdogo na mkewe ni dk slaa,wadogo zangu hata wale wasiopiga kura hawataki kabisa kuisikia CCM kwa sasa..hii inanipa moyo sana kwamba hata wakifikia umri wao kwao ccm itakuwa ni kero .....
   
 12. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Namshukuru Mungu sana kwa ajili ya ujumbe huu.......
  ni muhimu sana kutumia simu ili kushiriki ktk kampeni hizi za mabadiliko......
  mimi nimeongea na dada yangu ambaye alikuwa haelewi kitu zaidi ya CCM,mpaka nakata simu amekubali kumpigia dr Slaa...mama yangu alipoteza kitambulisho ila naye alikuwa amenielewa.
  Jamani kama Marekani walivyo na influence kwa marais wa nchi maskini...sisi pia tulio mijini/wafanyakazi tuna influence kwa ndugu zetu huko vijijini,kama kila mtu ambaye ameyakubali mabadiliko akipiga kampeni na kuhakikisha anapata watu kumi wa kukipigia CHADEMA basi ushindi ni dhahiri....Mh Kakobe namsifu sana kwa kutoa elimu ya uraia nzuri sana....kwa ambao hawakuona waangalie star tv kesho saa tatu kamili usiku na unaweza kutumia hiyo kuwaconvince watu wengine..wambie waangalie tv muda huo basi na baada ya lipindi watakuwa wamebadilika.....
  Mh Kakobe haongei kama mtu wa kawaida bali ni Upako usio wa kawaida na impact yake ni kubwa sana....
  KURA LAZIMA ZITATOSHA TU....just play your part ikiwa ni pamoja na kuchangia chama kipate fedha kiendelee na kampeni...
   
 13. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  aisee mwanangu msomi umeleta hoja ya msingi sana, mimi nilianza kutumia simu kwa kampeni toka 2005 kwa mbowe na hivyo nitaendelea mpaka kieleweke, wapo watakaobeza, puuza, shangaa na wengine watashtuka. cha msingi message sent
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Maneno Mazito sana haya

  KAMPENI KWA NJIA YA SIMU ZA MIKONONI NI KIBOKO KULIKO KAMPENI ZA SHUKA KWA SHUKA
   
 15. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,550
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimeipenda hii lets play our part, I will play my part
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hii kitu imekuja kwa wakati wake. Mimi na rafiki yangu mmoja tulishagundua jambo hili na tumelitumia ipasavyo. Kwa wale wanaotumia Zain kuna huduma ya bure ya sms 100 kila siku usiku baada ya saa 6 kamili.

  Tumia nafasi hiyo usilale. Tuma message kwa watu 100 unaowafahamu na kuwakumbusha kwamba nchi inaelekea katika mabadiliko makubwa na haya mabadiliko yatakuja kwa kumuingiza ikulu ya Tanzania Dr Slaa.

  Hii ni kampeni ya aina yake ambayo haihitaji mabango makubwa wala kibali cha polisi. Nimeitumia kwa mafanikio makubwa.

  Mimi nina kanuni ninayoitumia na kuwashawishi wengine kuitumia. Kila mtu aliye nyuma ya mageuzi ya nchi yetu ahakikishe anashawishi watu 25 kupigia kura Dr Slaa. Namna hiyo tutashinda.

  Kama huna line ya Zain basi ni wakati wa kuinunua kwa makusudi tu upate kupiga kampeni kirahisi. Ni wakati wa mabadiliko na twahitaji kutumia kila njia kufanikiwa. Pamoja tutashinda.

  CHAGUA DR SLAA CHAGUA CHADEMA CHAGUA MABADILIKO CHAGUA MAENDELEO YA TANZANIA.
   
 17. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Pamoja tutashinda  KAMPENI ZA KUTUMIA SIMU ZA MIKONONI ZINA TIJA KULIKO KAMPENI ZA SHUKA KWA SHUKA
   
 18. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2010
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Jambo lingine la muhimu ni kuhakikisha watu wengi zaidi wanapata fursa ya kupiga kura. Kama wewe ni mfanyakazi katika shirika ambalo wafanyakazi wengi wanatumwa nje ya makazi yao ya kudumu ni muhimu uongozi wa mashirika hayo waelewe na wawe tayari kutoa ruhusa kwa wafanyakazi wao ili waweze kupiga kura ifikapo oct 31st.

  kama HR wa mahali ninapofanya kazi nimejitahidi sana kuhakikisha wafanyakazi ambao hawatakuwa na shughuli za lazima siku hiyo wapewe nafasi ya kwenda kupiga kura.

  Kila mmoja akijitokeza kufanya sehemu yake hasa hasa kupiga kura nina hakika huu utakuwa ni mwaka wa kukumbukwa katika historia ya TANZANIA
   
 19. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Leo nimewasiliana na watu 2 na kuwashawishi kumpigia Dr. Slaa kura. Wameahidi kufanya hivyo.
   
 20. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii ni Kampeni Endelevu, tutaifanya mpaka 31 Oct, Ukimpigia Ndugu yako mwambie naye awapigie wenzie, hatuna Pesa ya Kutembeza Familia zetu na Magari ya kifahari kwa ajili ya Kampeni  KAMPENI KWA NJIA YA SIMU NI KIBOKO, IFANYE ASUBUHI, IFANYE MCHANA, IFANYE HATA USIKU
   
Loading...