Pictures: Uwanja wa ndege Songwe - Mbeya waanza kutumika, ndege zaidi ya tatu zatua

Infrastructure bado kwani naona abiria wakikanyaga matope. huwezi kulinganisha huu uwanja na ule wa Mwanza kwani huu umeharakishwa ili CCm ijidai ime keep promise. keep promise iliyoenda shule na si ubabaishaji kwani mwenye macho hahitaji kuambiwa tazama
 
Taratibu mkuu
Kwamba hata kukamilika na kufunguliwa ni ushindi mkubwa kwa watu wa Mbeya na mikoa inayaozunguka.

Uwanja huu umepigwa vita sana na viongozi wanaojulikana.
Waziri Mkuu aliyejiuzulu aliupiga mwara na kutokubali uwanja huu kutengewa fungu, na ndio maana ujenzi ulisimama kabisa.

Kwa suala kwamba uwanja una VUMBI nafikiri inabidi uende CCBRT kwa matatizo ya macho.

Kama wewe si mtaalam wa masuala ya usafiri wa anga inabidi ueleweshe kuwa ujenzi wa uwanja ni kitu kimoja, lakini uratibu wa matumizi ni fani nyingine kabisa!

Ni jana tu Mamlaka ya Usafiri wa anga nchini TCAA imetoa habari kwa ICAO (mamlaka ya usafiri wa anga dunia nzima), kwamba uwanja wa ndege Songwe upo tayari kwa matumizi.

Zaidi ya hapo , uwanja ni runway, runway ya Songwe ina urefu wa 3.3km , na ni ndefu zaidi hata ya DSM Int Airport.

Watu husema ROME was not build in one day, nakushangaa sana kwa lack of objectivity-kukataa maendeleo!

Ni kweli Mambo ya Urais wa CCM yalisababisha uwanja usiendelee kujengwa , Mmoja wa viongozi waliong'olewa kwa kashfa ya Richmond alihujumu ujenzi , kisa ! Eti uwanja huo ungempromote Mwandosya ! Bado naomba watu wa Mbeya kuuangalia uwanja huo kwa jicho la tatu , maana mafisadi hawajaridhika kabisa ,na wanaweza kufanya lolote ili mradi tu uwanja huo uonekane haufai .
 
Infrastructure bado kwani naona abiria wakikanyaga matope. huwezi kulinganisha huu uwanja na ule wa Mwanza kwani huu umeharakishwa ili CCm ijidai ime keep promise. keep promise iliyoenda shule na si ubabaishaji kwani mwenye macho hahitaji kuambiwa tazama
Ungekuwepo mwaka 1961 wakati wa uhuru naona ungedai flyover kwa mji(sio jiji) wa Dar es salaam.
 
Upuuzi mtupu kutujengea kakiwanja zaidi ya miaka 8. Tatzo la hii serikali wanatudharau sana Southern Higherland ilhali bila sie kitika kilimo nchi hii raia kibao wangekua washakufa kwa njaa.
 
After 10 (ten!) solid years of construction tumeibuka ni hii kitu. Aisee!!

Hapo unakuta kuna wahandisi wameumiza kichwa sana na kutoa kitu kama hiki 2012?? ni aibu kwa kweli.
Bora mtu usubiri, utoe kitu kizuri hata kama ni kidogo.
 
Fast Jet wanatumia ndege kubwa tu aina ya Boeing zaidi ya hiyo mikoa mitatu kuna mkoa gani mwingine ambao boeing inaweza kutua?

MTWARA; Uwanja MPYA wa MABOKSI wa MBEYA; Uwanja wa DODOMA; Kigoma ATC 737 ilikuwa inakwenda
Sasa HAPO ni MIKOA 4 zaidi inaweza kutua BOEING ...

Wataleta NDEGE ndogo PIA sababu Safari za KENYA hazijaanza Nairobi MOMBASA KISUMU na PIA KAMPALA ENTEBBE
 
Ni kweli Mambo ya Urais wa CCM yalisababisha uwanja usiendelee kujengwa , Mmoja wa viongozi waliong'olewa kwa kashfa ya Richmond alihujumu ujenzi , kisa ! Eti uwanja huo ungempromote Mwandosya ! Bado naomba watu wa Mbeya kuuangalia uwanja huo kwa jicho la tatu , maana mafisadi hawajaridhika kabisa ,na wanaweza kufanya lolote ili mradi tu uwanja huo uonekane haufai .

Wanasiasa wanafiki sana.
Juzi juzi Lowassa alienda na tumilioni 20 kutoa kanisani Moravian pale Mbeya, wakati ndiye aliyehujumu ujenzi wa uwanja huu.
Kweli pesa yake itamchoma moto.
 
MTWARA; Uwanja MPYA wa MABOKSI wa MBEYA; Uwanja wa DODOMA; Kigoma ATC 737 ilikuwa inakwenda
Sasa HAPO ni MIKOA 4 zaidi inaweza kutua BOEING ...

Wataleta NDEGE ndogo PIA sababu Safari za KENYA hazijaanza Nairobi MOMBASA KISUMU na PIA KAMPALA ENTEBBE

Uwanja wa Dodoma naujua mkuu haiwezi kutua pale sina uhakika na Mtwara na Kigoma,Mbeya kwa huu mpya inaweza sio ule wa zamani
 
Yan kwa wakazi wa mbeya hasa Songwe walikuwa wanandoto kubwa sana kuliko hicho kiwanja kilicho jengwa hapa, walitegemea kutakuwa na shugul mbalimbali za biashara ila sidhan kama usanii huo umeisha tendeka hzo ndoto wasahau.
 
Mi naona kama inafanana na nyumba si nyumba, guest si guest.

Only in Tanzania mkuu, hata proximity inaonekana hatujajali saaaana, muhimu ni shahidi afu iende kwenye outcome ya report ya mtu, kuwa airpot imekuwa succesful operating before 2013 as promised.

Tuna safari ndefu, tukomae mpaka kieleweke, vinginevyo tutaiona nchi inazama kusikofikika na divers.

ulizeni gharama na chengi ndo mjue wa 1880
 
Uwanja wa Dodoma naujua mkuu haiwezi kutua pale sina uhakika na Mtwara na Kigoma,Mbeya kwa huu mpya inaweza sio ule wa zamani

Boeing 737 Ilikuwa Inakwenda DODOMA; MTWARA PIA na MBEYA ni UWANJA wa KIMATAIFA MPYA unabeba NDEGE kubwa zaidi ya BOEING
 
international aiport gani iko hivyo?
au nini maana ya neno international airport?

Ukitoka mikoani ukatua Dar utaona kweli uwanja wa Dar ni International lakini siku ukifika Jomo Kenyata International nikajifunza kumbe wetu wa Dar ulitakiwa ujengwe Mwanza au Mbeya alafu Dar kikapigwa kitu chenye akili ambacho hata kama ndege zinazoondoka ni 10 bado zoezi la ku-check in linaendelea kwa pamoja si kama uwanja wetu wa Dar check in mlango mkuu ni mmoja wengine wanasubiri kwa nje

Hata hivyo huo ni mwanzo tu si mbaya sana kwa kuanzia na hicho kiwanja kama run way ni 3.3m matatizo mengine kama majengo yatarekebishwa, pia serikali iache siasa vile viwanja ambavyo ni busy kama Mwanza ambacho ni namba mbili kwa kuhudumia abiria wengi wafikirie kuviboresha viwe na kiwango cha juu kupita hata hicho cha Mbeya maana ni aibu uwanja unaohudumia abiria zaidi ya 400 kwa siku unakuwa upo upo hasa waiting room na huduma za upakuaji mizigo
 
Boeing 737 Ilikuwa Inakwenda DODOMA; MTWARA PIA na MBEYA ni UWANJA wa KIMATAIFA MPYA unabeba NDEGE kubwa zaidi ya BOEING

Dodoma haikuwahi kutua Boeing 737, ndege ambayo ilikuwa inatua ni Forker na ile ya serikali Jet maana nilikuwa naishi hatua jirani na uwanja wakati ndege ikitua ilikuwa ni nadra kukosa kusogea eneo la tukio kushangaa, nimekuwepo mji ule tangu nipo underground na uwanja si mrefu kivile kuweza kurusha Boeing

SABAYA
, uwanja wa Mtwara kuna kipindi Boeing ilikuwa inatua, kwa uwanja wa Dodoma ndege kubwa kutua uwanja ule ilikuwa ni ya mizigo ilikuja kuchukua ndege ya rais wa serikali ya zanzibar ilikuwa imeharibika hivyo ikaja kubebwa kwa matengenezo hata hivyo hiyo ndege ilitua kwa shida kwa timing ya kuanza kutua mwanzo kabisa mwa uwanja which means kama angeshindwa angepitiliza Chadulu na kugonga nyumba za watu, otherwise umenikumbusha mbali those days nilipokuwa Dodoma
 
Mie nashangaa serikali hii...viwanja vinavyo hudumia abiria wengi havitengenezwi mfano mwanza, wanakimbilia mbeya ambapo abiria hawafiki 500....serikali haijafikiri kabla ya kutenda....
 
Infrastructure bado kwani naona abiria wakikanyaga matope. huwezi kulinganisha huu uwanja na ule wa Mwanza kwani huu umeharakishwa ili CCm ijidai ime keep promise. keep promise iliyoenda shule na si ubabaishaji kwani mwenye macho hahitaji kuambiwa tazama

Hapo nilipo-bold, umeufunika wa mwanza kwenye hayo majengo though kwa watu wanaosafiri huku na kule yanaonekana kituko
 
Back
Top Bottom