Pichani, Daraja Kigamboni hiloo... Kigamboni yakufikirika yawa kweli

Ulienda kudai hela yako NSSF ukanyimwa?

Unafikiri fedha inayokaa NSSF ikikaa tu bila kufanyiwa kazi itazaa na kukupa faida?
swala sio kunyimwa hela wala kukaa bila kutumika swala ni kuzitumia kwa maslahi ya walengwa sio kuzitungia sheria za ajabu ajabu.
 
Hapana mimi sina hisa kwenye mgodi wowote wa dhahabu. Mimi nanuwa dhahabu za kuwavalisha wake zangu, sina kazi nazo zaidi ya hapo.

Kama unataka dhahabu si uende ukachimbe, unashindwa nini? kuna mtu aliyekuzuwia? au hujui kuna watanzania wengi wanachimba kila aina ya vito, tazama wenzako, hawaandikii mate, wanafanya kweli:

Wachimbaji%2Bwadogo%2Bkijiji%2Bcha%2BNgasamo.jpg
Wachimbaji wadogo wakikusanya vifusi vya mawe yaliyo na dhahabu...

Wachimbaji%2Bwadogo%2Bkijiji%2Bcha%2BNgasamo%2B12.jpg

Huku akiwa ameshikilia kipande cha dhahabu mdau mwananchi wa kawaida anaronga.... "Mimi ndiyo 'taita' wa mgodi huu"

Source: WACHIMBAJI WADOGO NGASAMO WILAYANI


Hivi umeweka picha habari yenyewe umeisoma?. Maana ni kuwa Serikali ya Huyu Jei Kei imewanaynganya eneo lao lakuchimbia.
Nikukumbushe iulisema hapo mwanzo kuwa kama si JK hivi vitu tungesikia majina tu. Ukweli ni kuwa huyu JK ndiye natufanya tuvisikie majina tu maana anatunyanganya nakuwapa hawa hapa
attachment.php
 
Sidhan kama hapo ndio mwisho, kwenye plan ilionekana daraja kubwa la kupita malori mawili kwa wakt mmoja bila kusimama au kujibanabana,
 
Katika pitapita zangu nimeona daraja hili linatua Kilwa Road, maeneo ya Bandari. Unless otherwise but, nikifikiria ile njia ya bandari mpaka gerezani pale roundabout ilivyo nyembamba nachoka kabisa. Foleni yake asubuhi na jioni kwa gari za Kilwa Road na Kurasini ni mziki tosha sasa sipati picha magari ya kigamboni yakiwa yanakatiza hapo. Natumai kuna mpango wa kupanua hiyo njia kabla ya 2015 (daraja litakapokamilika) au la iwe daraja liwe halitui pale Kilwa road vinginevyo itakua disaster.
 
daraja hili likikamilika litakuwa na njia sita za magari kulifanya kuwa daraja kubwa kuliko yote Afrika mashariki
 
swala sio kunyimwa hela wala kukaa bila kutumika swala ni kuzitumia kwa maslahi ya walengwa sio kuzitungia sheria za ajabu ajabu.

Kama vile kujenga darala la Kigamboni, kama vile kujenga mgodi wa makaa ya mawe yakayosaidia umeme kupatikana kwa wingi, au sio?
 
Na ile plan ya ''The blue diamond city of kigamboni'' imeishia wapi? Si walisema wakazi wote wa kule watahamishwa? Sasa mbona watu wanazidi kununua viwanja tu? All i have is my full eye on it.
 
Power tiller zina sehemu yake na Tractor zina sehemu yake SUMA JKT wanakupa mafunzo, ukiwapa data kamili za unapotaka kutumia na wanakushauri ni aina ipi ya zana uitumie hapo. Si kila kilimo unaweza kutumia power tiller na si kila kilimo ni lazima utumie tractor kubwa.

Daraja la mianzi na udongo wa mfinyanzi kwa mayai ya kuku wa kienyeji lilishindikana kwa kuwa tu, kuku na mayai stahiki yalikuwa hayapatikani, Teknolojia ya miaka 30 au mia nyuma siyo ya leo na wala haitakuwa ya miaka 30 au 100 ijayo.

Leo mnahangaika na vidaraja, miaka 100 ijayo, unapanda gari lako, ukikuta bahari unaingia nalo linakuwa boat, au unavaa jet pack yako mgongoni, daraja litabaki kuwa makumbusho. Taaluma zinaendelea na hazina mwisho, mimi na wewe tuna mwisho.

Idea zinawezza kuwa nzuri kwenye maneno na zikawa tatizo kwenye kuetekeleza kama vile idea ya Nyerere ya Ujamaa na Kujitegemea, tuliokuwepo siku hizo sote tuliona hiki ni kitu kizuri sana na ndicho kitakachotufaa, lakini hakikuweza kutekelezeka na ikawa big failure ingawa tukishindana mimi na wewe sasa hivi naweza kukuaminisha kuwa hakuna mfumo bora kama huo, lakini ni kwa doctrine nilizojazwa enzi hizo kabla ya kuona mifumo mingine.

Mimi nna idea ya kuruka bila mashine, wengine wanaitekeleza, nasikia wanaruka kwa ungo, Jee, ni idea nzuri hiyo au mbaya?

Hilo linajulikana ila kwa sie tunaobahatika kuhudhuria mikutano ya watendaji wa serikali huku chini, the way wanavyoleta ujumbe kwa wananchi ni tofauti, hata jembe la mkono bado linatumika, power tiller hali kadhalika. Tatizo waliokuwa watupa ujumbe mara baada ya kupitisha hii kitu power tiller as if ni njia mbadala ya plau na tractor hapo ndio shida (na sehemu nyingi wamefanya hivyo natambua kabisa kuna sehemu tractor lina kazi kubwa na kuna sehemu power tiller lina kazi yake. My concern hapa wanaohamasisha wanasahau kuwaunganisha wananchi na wataalamu wa kilimo wao wanafanya conclusion kwa kila kitu
 
Mimi hapa ndio nilishangazwa eti watu watavuka kwa kulipia...sielewi..!!

Na vipi ile habari ya kuwa Kigamboni imeuzwa??

Ndugu yangu ni kitu cha kawaida katika nchi nyingi, vinginevyo tukisubiri serikali ijenge kwa pesa za walipa kodi tutaendelea kuteseka zaidi wakati serikali uwezo wake unazidi kupungua.
 
Hawa wanakimbizana na uchaguzi wa 2015 tu hakuna lingine, yaani morogoro road hajui itakamilika lini, hivi mandela road wao hawahitaji kwenda kwa kasi?? bagamoyo road je?? why wasingemalizia hilo kwanza ndo waanze na daraja la kigamboni? hizo ni kampeni za chini kwa chini tuu!!
 
Yani nyie na utaalamu wenu wote hamjui kuwa kuna matayarisho ya ujenzi? hicho kinachoonekana pale ni maandalizi (Preliminaries & Mobilization) Daraja litajengwa kubwa la njia sita (3/3)

Wengi wetu hapa si mainjinia wa road construction, tutaandika mengi tu, lakini cha msingi tusuburi picha zaidi zitazidi kumiminika kadiri shughuli hiyo inavyozidi kufanyika na itatupa somo la kujua madaraja haya yanavyojengwa.
 
Wewe nawe! mbona viwanja vya serikali vipo vingi sana unahangaika na viwanja ambavo havijapimwa? kiwanja cha eka moja au mbili ni wazi kitakuwa hakijapimwa, na huu mradi uwe muangalifu wa kununua ardhi hovyo kigamboni au sivyo itakula kwako! nenda gezaulole kuna viwanja bwelele !

Umenifungua vizuri nakushukuru, lakini sipendi kakiwanja kadogo kwani home kwa wazazi wangu lilizoea kuchuma mapera, maembe, machungwa, apples, na kulima mbogamboga kando ya kaya yetu, hilo nimelizoea hivyo sipendi kakiwanja kakubanabana hata mzunguko wa hewa kuwa mdogo. Kigamboni kunagombaniwa na wengi, hapa nilileta kautani tu kadogo, kwangu bora nje kidogo ambako home kunakuwa kama ka-lunch ka kimaskini ninapostaafu niwe nakula mayai ya kuku wa kufuga mwenyewe, maana sitakuwa na kipato cha uhakika tena.
 
kwa hiyo ni rekodi nyingine ya kipumbavu.rekodi ya kimatonya matonya.rip

Utaratibu wa mwekezaji kujenga daraja kama hili ni kitu kigeni kwa nchi maskini kama Tanzania, lakini mataifa makubwa ni jambo la kawaida, ndio maana ukienda huko UK, USA, Canada na kwingineko utakutana na madaraja ya kulipia unapovuka na barabara za kulipia kila baada ya kuendesha umbali fulani kwa baadhi ya barabara kuu. Hii ni kwa sababu ujenzi wako ulitolewa kwa mkopo kutoka kwa mwekezaji au mashirika ya fesha. Daraja au barabara itakuwa mali ya serikali baada ya gharama za toso ushuru wa watumiji kumaliza deni na riba yake.
 
Umenifungua vizuri nakushukuru, lakini sipendi kakiwanja kadogo kwani home kwa wazazi wangu lilizoea kuchuma mapera, maembe, machungwa, apples, na kulima mbogamboga kando ya kaya yetu, hilo nimelizoea hivyo sipendi kakiwanja kakubanabana hata mzunguko wa hewa kuwa mdogo. Kigamboni kunagombaniwa na wengi, hapa nilileta kautani tu kadogo, kwangu bora nje kidogo ambako home kunakuwa kama ka-lunch ka kimaskini ninapostaafu niwe nakula mayai ya kuku wa kufuga mwenyewe, maana sitakuwa na kipato cha uhakika tena.

Mkuu uko sahihi, ukiwa na eneo la kutosha kuna raha san, kaeneo kadogo hata wakati "unamtandika" wife majirani nao wanajua!! ya nini hiyo?
 
Hilo linajulikana ila kwa sie tunaobahatika kuhudhuria mikutano ya watendaji wa serikali huku chini, the way wanavyoleta ujumbe kwa wananchi ni tofauti, hata jembe la mkono bado linatumika, power tiller hali kadhalika. Tatizo waliokuwa watupa ujumbe mara baada ya kupitisha hii kitu power tiller as if ni njia mbadala ya plau na tractor hapo ndio shida (na sehemu nyingi wamefanya hivyo natambua kabisa kuna sehemu tractor lina kazi kubwa na kuna sehemu power tiller lina kazi yake. My concern hapa wanaohamasisha wanasahau kuwaunganisha wananchi na wataalamu wa kilimo wao wanafanya conclusion kwa kila kitu

Kilimo kwanza haihusihi power tiller pekee, sijui unachotaka kubishana hapa nini? hapa kuna mada ya daraja la Kigamboni na limeshaanza kujengwa.

Kama unataka tuanze kuongelea Kilomo kwanza na matractor, nakuomba sana funguwa nyuzi ntakuja tulumbane kwa hoja.

Iwe power tiller au tractor au jembe la mkono, kumbuka kuwa Kikwete amekuwa mfano wa kuigwa Duniani (rikodi nyingine kwa Jakaya Mrisho Kikwete) kwa initiative yake ya mpango wake wa SAGCOT ambayo ni part and parcel ya Kilimo Kwanza kama ilivyo power tiller na mengineyo, au hulijui hilo?

Kikwete anafanya kweli, katika kila nyanja:

The eight most industrialized countries have pledged 897 million US dollars support to Tanzania under the new alliance to bolster agriculture and food security in Africa announced by President Barack Obama last Friday.

President Jakaya Kikwete, who attended a G8 special session on Africa at Camp David near here on Saturday, said in an interview yesterday that the US made the largest single pledge of 315 million dollars.

Soma zaidi:
Tanzania Clinches Multi-Million Dollar Agriculture Deal | AfricanLiberty.org



 
Back
Top Bottom