Ndio ukweli, na hata kama hili daraja lina uwezo huo si rahisi kuisoma picha kwa vile picha hajapigwa kwa kiwango cha vipimo vya kujua upanda wa daraja. Mpiga picha alijitahidi kuvuta lens ili kupata taswira ya hatua za ujenzi ilipofikia, huenda tunatoa hitimisho mapema kabla hatujawa na uhakika wa vipimo vya ukubwa huo.
Madaraja kama haya ambayo tunaona picha zake, si rahisi kujua yana lane ngapi, kwa vile picha haiwezi kutoa scale ya ukubwa.
Ahsante Kikwete, rikodi nyingine.
Mchakato mzima wa kujenga daraja ulianza sometime back. JK amekamilisha tu. Tumpongeze kwa lipi? Siasa pendwa hizi...
Mchakato mzima wa kujenga daraja ulianza sometime back. JK amekamilisha tu. Tumpongeze kwa lipi? Siasa pendwa hizi...
Tumechangia sana baada ya kuonekana miaka hii zikawa nyingi ndio ikaonekana kuna haja ya asilimia 60% ya michango yetu ichangie na serikali imalizie hiyo 40% (kwa hili kudos kwa serikali na si JK pekee si unajua mlolongo huu ni wa siku nyingi) ila na sie wenye hela pia utupongeze zomba kwani kuna shida gani.
Swali la kizushi; Kwani idea ya kujenga hilo daraja imetoka lini? na upembuzi yakinifu umefanyika lini?
Kuna michakato ya kila aina si ya kujenga daraja tu, ipo kwenye makaratasi na ndoto za mchana, kabla wewe na mimi hatujakuwepo, Jee, tuipongeze kwa kuwa ipo kwenye ndoto zao au tumpongeze aliyeifanya ikawa kweli na si ndoto tu? Fikiri.
Kikwete anafanya kweli.
Yani nyie na utaalamu wenu wote hamjui kuwa kuna matayarisho ya ujenzi? hicho kinachoonekana pale ni maandalizi (Preliminaries & Mobilization) Daraja litajengwa kubwa la njia sita (3/3)Dr. Kupeng'e nadhani ulijibu haraka, hata udaktari wa falsafa huanzia na elimu ya msingi na kupanda kidogo kufikia bachela kabla ya kuamua kuibukia graduate college yenye kukutuza PHD.
Little is better than nothing. Madaraja mengi kutokana na gharama kubwa iliyopo hujengwa kwa kusaidia tatizo la wakati uliopo, siku za usoni upo uwezekano wa kupanua kwani hakuna lisilowezekana.
Unataka Ulaya nao waige kujenga hotel ya kitalii kama ya Tanzania inayoongoza number one kwa miaka miwili mfululizo? Jibu hapana kwa sababu kila kifanyikacho hutegemea uchumi, mazingira na uwezo.
Ninachofahamu ni kuwa process ilianza muda mrefu. Akikamilisha katiba njoo na thread ya kumpa pongezi.
Daraja halijajengwa na kodi za wananchi, bali ni mwekezaji ambaye daraja hilo tutalivuka kwa kulipia. Sijajua itachukua miaka mingapi mwekezaji kurudisha gharama kisha tupate huduma bure.