PICHA: Zitto Kabwe afunika Mkutano wa Hadhara huko Kigoma Mjini

Status
Not open for further replies.

Mohamed Mwaupete

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
375
0
Nipo Live hapa Kigoma Mjini Muda huu wananchi wanaendelea kumiminika kwenye Uwanja wa Mwanga CENTRE kwaajili ya Mkutano wa hadhara wa Mh.Zitto Kabwe.

Kama kawaida Steji imepambwa kwa bendera ya Taifa ishara ya wazi kabisa kuwa Zitto Kabwe anafanya siasa za Kitaifa,Lakini Pia mapokezi yake na Mikutano yake imejaa Utaifa Kwanza.


UPDATES

Mh.Zitto Kabwe ameshawasili kwenye Viwanja hivi vya Mwanga CENTRE na Utambulisho unaendelea kwa viongozi wa chama,Kubwa ZItto ni Mbunge wa Kitaifa,Wanakigoma hawababaishwi na ubaguzi unaeondelea CHADEMA.

MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA KIGOMA
Wanakigoma,ZItto ni mmoja wa vijana wa kigoma,tunakila sababu ya Kumlinda,kumpigania na kusimama naye katika hatua zozote zile.Naomba tuungane kupambana naye kwenye hatua hii inayaoendelea ndani ya chama.
Inauma sana kuona tumepigwa mabomu,risasi,tumetumia muda wetu kuijenga chadema,Leo matunda yameanza kutoka wanakata mti kwasababu tu wao wanataka kujinufaisha.HAPANA.

KATIBU CHADEMA MKOA ANASEMA
Nimeulizwa mwasali mengi sana kwanini hakuna bandera,kwanza ni salamu kwa Katibu Mkuu kuwa Chadema Kigoma hatuna bendera,fedha za kununulia hatua(ruzuku).Pia mapokezi ya zitto licha ya kuwa ya chama,ZItto tumempokea Kitaifa.
ZITTO KABWE AMEPANDA JUKWAANI


Nimekuja kuzungumza nanyi wanakigoma kwa Mujibu wa katiba ya chama,kama Katibu Mkoa alivyoeleza na katibu wa chadema hapa Kigoma mjini.

Hivyo msithubutu kusikia propaganda zozote zile eti nitawajibishwa kwasababu ya kufanya mikutano nje ya Kigoma kaskazini,katiba ya chama inaniruhusu na katiba ya nchi inaniruhusu pia kwenda popote na kufanya chochote bila kuvunja sheria.

Wote mnakumbuka nilichukulia kadi kwenye uwanja huu mwaka 1993 nikiwa na miaka 16. Nimepata Ubunge nikiwa na miaka 29 kwenda kuwawasilisha wananchi wangu wa kigoma kaskazini na nchi nzima. Mnakubaliana nami namna nilivyokuwa kiongozi bora ndani ya bunge,Kuanzia hoja ya Buzwagi,Kumng'oa waziri mkuu na sasa Mabilioni ya Uswis.

Pia namna nilivyopigania ujenzi wa rami mkoa wa Kigoma,Lakini lengo langu ni kutaka siku zote wanakigoma mjivunie kutaja kuwa ww ni mzawa wa kigoma,na nimeshaijenga heshima hiyo.


Lakini ndugu zangu Ng'ombe akiumizwa malishoni anakimbilia zizini. Nimekuja Nyumbani kuzungumza na wananchi wangu, Ndani ya chama nimeumizwa ,Nimevumilia sana kwa mikuki ninayopigwa na wenzangu ndani ya chama.

Uchaguzi wa ndani ya chama wa Uliopita nilijitosa kugombea Uenyekiti,Lakini wazee wa chama wakaniita nimuachie mwenzangu awe mwenyekiti, NIKAKUBALI.

Lakini kuna vijana wamesurubiwa ndani ya chama kwasababu tu wamekuwa wakiniunga mkono. Mchange Habib alishinda uchaguzi wa Umoja wa Vijana, Lakini matokeo yake yakafutwa na kupewa mtu mwingine, Kwasababu yangu.

Akina Kafulila pia walishughulikiwa ndani ya chama kwasababu ya Kudai haki,Bahati mbaya sana Kafulila akaondoka kwa hasira chadema.

MIMI NITAPIGANIA HAKI YANGU kwa sababu ndani ya chadema kuna jasho langu, Kuna nguvu na mali zangu nilizopigania, Kuna watanzania waliopigwa risasi, mabomu na wengine kufariki kwasabau ya kupigania chadema.

KUONDOKA CHADEMA NI KUWASALITI WAPIGANIA HAKI, KUWASALITI WALIOKUFA KWASABABU YA KUIPIGANIA CHADEMA ISIMAME HADI HAPA ILIPO.

Pia naomba mtambue hoja yangu ya PAC inanimaliza chadema,Wenzangu ndani ya chama wananiandama kwasababu sikuwajulisha mapema kuhusu mahesabu ya ruzuku/mapato ya chama. Hakika katika hili nitaendelea kusimamia hoja yangu kwa Maslahi ya chama,Chadema lazima ikaguliwe kwa mujibu wa kanuni na sheria za nchi.

Jana mmesikia Slaa kwenye vyombo vya habari akisema atanifukuza eti vijana wanaoniunga mkono na wananchi wananiponza,Watanzania hukusio kufukuzwa??

Slaa ni katibu Mkuu wa chama na ndiye mwendesha vikao,Leo hii anatoa huku kabla ya Vikao,huku sio kufukuzwa?

Mwenyekiti wa chama pia alinukuliwa na vyombo vya habari kule mwanza,Eti zitto akirudishiwa vyeo vyake ndani ya chama labda mimi sio Mbowe! Wanzania huko sijafukuzwa tayari?

Leo hii wajumbe wa mkutano mkuu wameshaanza kuandikisha majina yao wakiomba mkutano mkuu uitishwe ilikujadili hatma ya mambo yanayoendelea ndani ya chama,Pia kujadili rufaa yangu. LAKINI DR. SLAA ANAWATISHIA ETI WAOAFANYA HIVYO NI WASALITI NA WAHUJUMU WA CHAMA!


Mh.ZItto kabwe akiondoka huku gari lake linasukumwa


Zitto kabwe yupo jukwaani anahutubia Muda huuZitto anakaribishwa sasa jukwaani

zi

Ujumbe unaendelea kufika kwa wahusika


Mamia ya Wananchi wakimiminika Viwanja vya Mwanga hapa Kigoma mjini.

Wananchi wanaendelea Kumiminika Viwanja hivi vya Mwanga CENTREZitto amemaliza kuhutubia hapa sasa ni wimbo wa Leka Dutigite
 

Wed

JF-Expert Member
Mar 7, 2011
316
500
Mtakumbuka Mrema alivuma sana katika siasa za Tanzania. Baada ya watu kumgundua kuwa ni Msaliti ule umati uliokuwa unamfuata uliishia kumtelekeza. Siku hizi Mrema akipanda jukwaani huishia kupata watu kiduchu. Kama siyo CCM kumbeba asingepata hata ubunge wa Vunjo..... Kadhalika Zitto baada ya kugundulika kuwa naye ni Pandikizi la CCM, nampa Zitto miaka 2 tu.. mtajaona, naye ataishia kama Mrema
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom