PICHA: Zitto akiwa jimboni kwa Msigwa leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PICHA: Zitto akiwa jimboni kwa Msigwa leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kamandamakini, Jun 17, 2012.

 1. k

  kamandamakini Senior Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 158
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]  [​IMG]
  Mh. msigwa
  [​IMG]


  [​IMG]
  [​IMG]
  Mh. zitto.

  magamba yavuliwa watu wamiminika toka chama chamapinduzi kuhamia chama cha demokrasia na maendeleo. katika mkutano huu mh. msigwa alichukua maoni na maswali toka kwa wananchi ilikwenda kuwawakilisha vyema wananchi walio mtuma bungeni hasa katika bunge hili la bajeti,

  Mh. zitto Akihutubia mkutano uliohudhiriwa na mamia ya wakazi wa manispaa ya Iringa katika viwanja vya Kihesa Sokoni, Manispaa ya Iringa, Naibu katibu Mkuu wa Chadema ambaye ni Naibu waziri kivuli wa fedha, alisema bajeti iliyosomwa bungeni, inaonyesha wazi kwamba Serikali imeshindwa kujali wananchi maskini badala yake inajali matajiri
  .
  "Jumatatu tutaenda kuwakatalia bajeti yao, hatutaikubali kamwe! bajeti hii imeshindwa kudhibiti mfumko wa bei ambao umepaa kwa kasi hadi kufikia asilimia 18.7 toka asilimia 6.6, iliyokuwepo wakati bajeti iliposomwa mwaka jana," alisema Kabwe.

  Alisema vitu vinavyofanya maisha ya watanzania kuwa magumu ni mfumko wa bei ya chakula ambao ni asilimia 25 na nishati ambayo ni asilimia 27, huku Serikali ikishindwa kudhibiti hali hiyo kwa kuandaa bajeti inayoshindwa kutekeleza ahadi zake.

  Alisema bunge lilipitisha mpango wa maendeleo wa taifa uliotaka asilimia 35 ya mapato ya ndani, yatengwe kwa ajili ya bajeti ya maendeleo jambo ambalo, limekuwa kinyume na bajeti iliyosomwa ambayo, imetengewa asilimia sifuri, kwa ajili ya mpango huo.

  "Tutahoji kwa nini Serikali imeshindwa kutenga asilimia 35 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya mpango huu, kwanini inafanya vitu kinyume cha sheria na kutenga asilimia sifuri?...jambo hili hatutakubaliana nalo," alisema.

  Alidai kuwa hali halisi ilivyo sasa ni kwamba, mtanzania anatumia asimilia 48 kwa ajili ya kununua chakula, asilimia tisa kwa ajili ya nishati hali ambayo ni hatari.

  Alidai kuwa, kwa mujibu wa bajeti hiyo, shughuli zote zitaendeshwakwa fedha za mkopo na misaada toka kwa wahisani huku akidai kuwa, kwa mwaka huu Serikali itakopa sh trioni tano, huku deni la sasa likiwa trioni 22.

  "Trioni 22 ni deni kubwa ambalo linafanya kila kichwa cha mtanzania kudaiwa sh laki 4.18, fedha ambayo ni kubwa kuliko hali halisi ya mtanzania," alisema.

  Alidai kuwa tatizo sio kukopa isipokuwa tatizo ni pale ambapo Serikali inakopa kwa ajili ya anasa kama mafuta ya mabenzi, na kulipana posho

  source: Mbunge Wako Iringa Mjini
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  CCM kwisha habari yake
   
 3. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naona ukombozi unakaribia. Peoplezzzzzzzz
   
 4. m

  mahoza JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Hongera CDM.

  Peoplezzzz zzzz paw.
   
 5. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Wakati natoka kihesa narudi homu nikaona gari la nape kumbe nae alitaka kufanya mkutano mwembetogwa lakini magamba waliogopa kukosa watu maana iringa nzima ilikua kwenya harakati za ukombozi so CCM nayo itakua mwembetogwa ikimwaga sera chini ya Nape.
   
 6. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  T2015CDM at its escape velocity(i.e 11.2km/s) wewe Nape utaweza? Chunga sana...
   
 7. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nikisikia nasahau,nikiona nakumbuka,nikisia,nikiona na kugusa ninakumbuka,ninaelewa na kufahamu.ASANTE SANA KWA COVEREGE MKUU.
   
 8. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #8
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Ukombozi umesha wadia kwa kasi ya kimbunga, hakuna rangi magamba wataacha kuona. Bajeti tri 15 deni tri 22.
   
 9. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kila mtanzania anadaiwa 488'000/ ili kulipia deni la taifa, hii ni pamoja na mimba iliyotungwa leo! NAPE anatamka 2015 ccm haitakabidhi nchi kwa wahuni. Wahuni ni nani? Nani anamdanganya huyu bwana mdogo? Wanaokabidhi ni wanananchi na wala si SISIEMU.
   
 10. R

  RMA JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wanasemaje? Bado Chadema ni Chama cha kaskazini?
   
 11. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mleta habari umedanganya umma, hao siyo mamia ya wakazi, ni maelf ya wakaazi.
   
 12. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Kaza buti Mh ZITTO KABWE watanzania tupo , na tuna waamini kamwe msiogope kuusema ukweli mchana kweupe

  Hawa jamaa kiukweli nchi inawashinda kuongoza ndiyo maana wanashindwa kuyabaini mambo ya msingi badala yake wanajali zaidi anasa
   
 13. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kinachofurahisha ni kwamba hapakuwa na kampeni jaza uwanja ile inayafanywa na ccm
   
 14. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Sasa ile taswira niliyokuwa nimeiona inakaribia kutokea, hali ya uongozi wa tanzania (ccm) iko hati hati, wabunge wetu wa cdm sisi tuko nyuma yenu kesho twasubiri kuona uzalendo wenu wa kupinga hiyo bajeti, hivi yale mashangingi hayauzwi tena?
   
 15. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  mkutano huko Kilolo
   
 16. m

  mohermes Senior Member

  #16
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa halaiki hyo nadhani siku ya ukombozi imewadia hapa Tanzania.Kila dalili iko wazi kwamba CCM hawana chao hapa tena.Viva CHADEMA.VIVA wanamageuzi
   
 17. I

  IDIOS Member

  #17
  Jun 17, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nna asilimia tisini na tano ss kuwa 2015 ni kuchukua nchi. Hakika hakuna wa kutupinga.

  Pipoz pouwer.
   
 18. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Magamba wanakosa usingizi nyomi hii inaonyesha mabadiliko makubwa sana...ama kweli Vua Gamba Vaa Gwanda!!!
   
 19. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kweli maji hufuata mkondo, ngoma inogile 2015.
   
 20. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kamandamakini inamaana wewe ndo Mch. Msigwa? weell safi sana nimependa hii watu wanaamka sana hii ya kuwasiliana na wananchi kwa karibu mara kwa mara nzuri mno!
   
Loading...