Picha zangu za leo ni hizi hebu toeni maelezo yenu Mtaa kwa mitaa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
ni maandalizi ya vita ama nini??


maana kila kukicha lazima ukutane na mahandaki kama haya ambayo yamejaa katika kila kona ya jiji letu hili,wenye data na mahandaki haya tumwagieni hapa mtaani.hili lipo pale Namanga jirani kabisa na kituo cha daladala cha mbuyuni kama unatoka mjini.




hatimae kile kipande korofi cha mtaa wa mafia,kariakoo chapatiwa ufumbuzi

leo katika katiza katiza zangu za mtaa kwa mtaa,nilipita katika mtaa huu ambao siku chache zilizopita nilileta picha za eneo hili (zicheki hapa) lililokuwa limeharibika vibaya sana.lakini nilipopita leo nimekuta mambo yapo kama yanavyoonekana hapa.
hapa mtaalam wa kuendesha kile kimashine cha kushindilia akiwajibika ili kuhakikisha mtaa unakuwa poa.
hata magari yanapita vyema sasa,sio kama hali ilivyokuwa hapo awali.



hadha ya pikipiki za kichina

huyu rafiki yangu leo almanusura alipukiwe na hii pikipiki,maana ilipiga shoti katika waya za taa ya mbele na kuanza kusambaa huku akiwa katika wendo kuelekea kwenye mishe mishe zake.yaani hapo mnapomuona hana hata hamu na hiyo pikipiki ila kwa kuwa na yake,inambidi aikokote tu kuipeleka kwa fundi.daah hizi pikipiki noma kweli.



mambo yetu yaleee

wamelamba mfuniko,wameweka tairi chakavu.mambo yanakwenda kama kawa.



soja wa ukweli

huyu sasa ndio soja olijino,maana wewe mwenyewe ukimuona tu lazima uchachawe.



watoto na ujasilia mali


Baadhi ya watoto wakivuka eneo la wapitao kwa miguu katika Barabara ya Msamvu , mjini Morogoro wakiwa na mzingo mkubwa wa chupa tupu za maji baada ya kuziokota toka maeneo ya baa na vioski eneo la Msamvu, Manispaa ya Morogoro kama walivyokutwa mwishoni mwa wiki katika eneo hilo. Picha zote na John Nditi


Deiwaka Inapoingia dhahma


Leo nimeazima hii ToYo ya jamaa yangu na kwenda nayo katika misele yangu ya mtaa kwa mtaa.lakini yaliyonikuta huko sina hamu nayo tena maana imenikatikia mnyororo sehemu ambayo ni mbaya kama nini na kunibidi niipige kibega mpaka kwa fundi J na hela juu ikanitoka ya kununua mnyororo mpya.ama kweli hii ni dhahma ya deiwaka,maana ningeirudisha hivi mwenyewe angenirushia hata ngumi.

Haya ndio Maisha yetu ya kila siku Matatizo tu kila siku shida haziishi mpaka lini jamani???????????

 
Adha Ya Maji



Tunapofikiria kuchagua viongozi wa kisiasa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba 31, wananchi tuna kila sababu ya kuchagua Rais, Wabunge, Madiwani wenye sera madhubuti zinazoweza kutuondolea kero kuu katika maisha yetu. Sera zenye muelekeo wa kupambana kwa dhati na maaduwi watatu, Ujinga, Maradhi na Umaskini. Kwako mpiga kura,,,,,
 
taswira za pemba ya leo
Hapa ni Chake Chake, Pemba, ambako taswira yake inaenda ikibadilika kila siku kwa majengo mapya pamoja na miundombinu ikiwa ni pamoja na umeme wa uhakika toka katika gridi ya Taifa kupitia Tanga. Pia watu wa Pemba ni wakarimu na wacheshi, jambo ambalo limeongezeka maradufu baada ya muafaka kukamilika na makubaliano ya serikali ya mseto visiwani kupotishwa kwa kauli moja. Leo hii wakati kampeni zinaendelea Pemba iko poa na kila mtu anashabikia chama anachokitaka bila kelele wala mikwaruzo kama ilivyokuwa awali kabla ya muafaka.
Ni majira ya mchana ambapo vijana wengine wanatoka Darsa na wengine wakielekea skuli kwa furaha na utulivu ambavyo ni asili ya visiwani humu

Majengo ya kisasa yanachipua kila kona ya Pemba sasa
Nidhamu mahotelini kama kawa....
Ng'ombe ni mojawapo ya njia kuu za kusafirisha bidhaa
Chake Chake ya leo Rutuba kwa wingi Pemba kiasi kwamba inafanana na Tukuyu, Moshi ama Bukoba kwa mazao na hali ya hewa pamoja na ukijani usio wa kawaida kwa sehemu ya pwani Vespa ni usafiri muhimu kisiwani Pemba Mtangazaji mahiri wa TBC 1 wa Songea, mdau Gerson Msigwa, akifurahia mandhari Pemba


Bado tupo nyuma kimaendeleo jamani tunakokwenda tutafika lini jamni??????????Ahhhhhhhhhhh
 
IMitaa ya Ilala sehemu ya pili.

Leo watu wa Ilala nipo mitaa ya Karume

Soko letu jipya la Machinga ndo kama hili

Hapa nawaonesha uwanmja wa Karume na mbaali Mwalimu House

Mitaa ya kati hapa kama unatokea TRA hapa Shaurimoyo.

Waliosoma hapa Alharamain wataikumbuka hili jengo.

Mambo flani ya maji ya Ilala hapa Mchikichini kiwanda cha TBL

Mtaa wa Suwata huo hadi Karikoo

Hapa kati ni Shule ya Uhuru Mchanganyiko na nyuma ni magorofa ya NHC TBL.
Nafikiri waliotoka mitaa hiyo wameona kidogo maendeleo na mandhari ya mji wao.
 
Mzizimkavu uwe unajaribu kuacknowledge kazi za watu kwa kuweka sources basi duh
 
Wewe jamaa inaonekana una akili sana lakini wakati mwingine unaleta mada za ajabu ajabu...mfanao hapa hizi picha ni nzuri na zinafurahisha na kulenta mantiki kubwa ila unapo leta mambo yako ya hisia za kidini katika mambo yasio ya kidini huwa una haribu hali ya hewa kabisa............Mfano eti shekh yahaya asizungumziwe humu JF why? yule ni mtu maarufu anazungumziwa humu kwasababu ya umaarufu wake.

Kwa hizi picha nakupa thenkisi.
 
Nyongeza yangu hii hapa...kids who are both SAD and HAPPY

pli_enguiki_girls.jpg
 
Ni maisha tu, inabidi kuhangaika kutafuta shilingi kwa aendeleo yako binafsi na familia
 
mdau nakushauri uanzishe blog yako maana unatuchosha tu hapa na mapicha ambayo mengine ume-download kutoka kwa Michuzi kuja kutuchosha tu hapa
 
hiyo ilikua ari mpya nguvu mpya na kasi mpya sasa tunasubiria ari zaidi nguvu zaidi na kasi zaidi nahis hali itaendelea kuwa mbaya zaidi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom