Maria Roza
JF-Expert Member
- Apr 1, 2009
- 6,797
- 1,567
mungu awalaze mahali pema peponi
Hii inasikitisha mno , inaumiza sana!
Nashindwa kuvumilia kububujikwa na machozi. Hizi picha zimezidisha simanzi maana zinaonyesha mengi sana:
1.Ajali za barabarani zitatumaliza jamani.
2. Umaskini uliokithiri nchini mwetu - yaani tumeshindwa hata kuwasitiri hawa marehemu japo hata kuwafunika vizuri! Hapo wamesitiriwa na vitambaa vya mabango yao wenyewe tu. Halafu wamewekwa chini - thamani ya binadamu hapo hakuna kabisa.Kama mzazi nimeumia sana!
MUNGU WA REHEMA NA NEEMA ZISIZO NA MWISHO, UWAJAALIE PUMZIKO LA MILELE.
DUNIANI TUNAPITA TU......
Mliotangulia, pumzikeni kwa amani, ole wetu siye tuliobakia!
ina tisha sana jamani, mungu awarehemu
tusiwalaumu sana wahusika sister kwa kuwasitiri na mabango ya burudani zao, hospitali zetu si unajua hata panadol hakuna? sasa sanda/shuka lipo kweli? hata wagonjwa waliolazwa tunaona wakijifunika kanga zao.
masikini nchi yetu. mashangingi kila mtaa, viongozi wetu kila siku safari za nje ya nchi na msururu wa wasidizi, ofisi na makazi ya kifahari, samani za kifahari zinabadilishwa maofisini kila siku! lakini umasikini hausemekani. eti tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru mwaka huu na chama tawala kimekuwa kikishinda kwa kishindo kila uchaguzi toka uhuru! uchaguzi wa mwisho kushinda ulikuwa mwaka jana tu!
lol, RIP wapendwa wetu
in God we trust
amen
Glory to God
WOS. Hiki kitu nilishakisema siku nyingi sana. Maisha ya binadamu Tanzania hayana thamani sana akiwa hai hata akiwa amekufa. Nilishaweka post hapa kinsi maiti zinavyobebwa kwenye landrover za polisi utadhani ni nyama zinatoka butcher. Serikali kweli imeshindwa kununua gari maalumu za kubebea maiti na kuzisambaza kila mkoa? Imekuwa ni rahisi mno kwa serikali kununua magari mengi ya kifahari kila mwaka, lakini imeshindwa kununua magari ya kubebea wagonjwa na maiti. Jinsi unavyodhalilisha maiti, inaonyesha ni jinsi gani kiwango cha utu wako ulipofikia.
View attachment 25559