Picha za Wanataarabu wa 5 Stars waliokufa Morogoro!

hakuna walichokiacha zaid ya matendo mema,kilichobaki ni kuwaombea zaid ya kuwasikitikia!ALHAMDULILLAH!
 
Mwenyezi Mungu akupeni pumziko la kheri! Mmeimaliza safari yenu! Pole kwa Wandani wenu na wote waliokua tegemezi kwenu ikiwa ni pamoja na ndugu jamaa,marafiki na mashabiki wa muziki wenu pendwa! Tutawamiss sana!
 
Hakika sote ni wamwenzi mungu na kwake tutarejea! Wana JF tujifunze katika hivi vifo, Dunia ina mwisho, muhimu kwetu ni kufanya mazuri ili yatusaidie siku ya hukumu. Mungu atupe mwisho mwema inshaallah!
 
Baba Mwenyezi wapumzishe kwa Amani. Poleni wafiwa ndugu na jamaa. Inasikitisha!
 
Haya maafa yamenikumbusha yale maafa yaliyotokea mwaka 1992, Pale timu ya taifa ya Zambia ilipoangamia kwa ajali ya ndege.
RIP 5stars.
 
Mungu wangu! inasikitisha kwa kweli. Mwenyezi Mungu zailaze roho za marehemu wote pahali pema...Amen:crying::crying:
 
dah jamani Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. amina
wafiwa poleni sana Mungu awape nguvu na mzidi kuwaombea ndugu zetu hawa wafike salama kwa Muumba.
Mliopona katika ajali hii jamani kumbukeni kuwa Mungu yupo na pia muwaombee waliotangulia, poleni sana najua itachukua muda kusahau tukio hili ila nawatia nguvu na ninawaombea mpone haraka majeraha yenu katika miili na moyo pia.
 
Hii inasikitisha mno , inaumiza sana!
Nashindwa kuvumilia kububujikwa na machozi. Hizi picha zimezidisha simanzi maana zinaonyesha mengi sana:
1.Ajali za barabarani zitatumaliza jamani.
2. Umaskini uliokithiri nchini mwetu - yaani tumeshindwa hata kuwasitiri hawa marehemu japo hata kuwafunika vizuri! Hapo wamesitiriwa na vitambaa vya mabango yao wenyewe tu. Halafu wamewekwa chini - thamani ya binadamu hapo hakuna kabisa.Kama mzazi nimeumia sana!

MUNGU WA REHEMA NA NEEMA ZISIZO NA MWISHO, UWAJAALIE PUMZIKO LA MILELE.

DUNIANI TUNAPITA TU......

Mliotangulia, pumzikeni kwa amani, ole wetu siye tuliobakia!

WOS. Hiki kitu nilishakisema siku nyingi sana. Maisha ya binadamu Tanzania hayana thamani sana akiwa hai hata akiwa amekufa. Nilishaweka post hapa kinsi maiti zinavyobebwa kwenye landrover za polisi utadhani ni nyama zinatoka butcher. Serikali kweli imeshindwa kununua gari maalumu za kubebea maiti na kuzisambaza kila mkoa? Imekuwa ni rahisi mno kwa serikali kununua magari mengi ya kifahari kila mwaka, lakini imeshindwa kununua magari ya kubebea wagonjwa na maiti. Jinsi unavyodhalilisha maiti, inaonyesha ni jinsi gani kiwango cha utu wako ulipofikia.

coroner-michael-jackson.jpg
 
mmmh nothing to say ila nasi niwakati wakujitafakari, nakujileta karibu na Mungu maana kifo kinakuja kama mwizi. MWENYEZI MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI. AMINA
 
Jamani Watanzania wenzangu, tuamke! Madereva wahuni wanatumaliza au kutuachia vilema vya kudumu! Mungu awaweke marehemu wetu mahali pema peponi!
 
Back
Top Bottom