Picha za Viwanja 10 vya ndege vilivyo mbali zaidi na Miji Duniani..

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Uwanja-wa-Ndege.jpg



Mara nyingi nimesikia ndani ya vikao vya Bunge kuhusu ishu ya jinsi kuwahamisha watu wanaoishi pembeni ya Viwanja vya ndege ili Viwanja vitanuliwe.. kuna waliofuata Viwanja na kuanzisha makazi yao, ishu ni Kiwanja kiondoke kwenda mbali au watu waondolewe viwanja vitanuliwe?

Nimekutana na hii ripoti ya Daily Mail iliyotolewa June 04 2015.. inaonesha Viwanja vya Ndege vilivyojengwa mbali zaidi na Miji.


Paris Vatry Airport.. Uwanja uko umbali wa kama Kilometa 210 toka Jiji la Paris, Ufaransa.


Oslo-Torp Airport.. Huu uwanja uko umbali wa Kilometa 117 kutoka Oslo ambapo ni Mji Mkuu wa Norway. Ukitaka kufika Town inabidi utumie taxi au usafiri wa treni.


Munich West Airport. Ukisikia jina la huu Uwanja unaweza kuhisi kwamba uko ndani ya Mji Mkuu wa Ujerumani, Berlin. Lakini ukweli ni kwamba Uwanja huu wa ndege uko Memmingen. Na bado Umbali wa kutoka Uwanjani mpaka kwenye Mji ni Kilometa 112.


Frankfurt (Hahn). Uwanja huu wa Ndege uko umbali wa kama kilometa 109 kutoka Mji wa Frankfurt, Ujerumani.


London Oxford Airport, uwanja uko umbali wa Kilometa 98 kutoka katikati ya Jiji la London.


Stockholm Skavsta Airport. Kutoka hapo mpaka ufike Stockholm Town, Sweden ni umbali wa Kilometa 97


Barcelona Girona Airport, uwanja ulipo na katikati ya Jiji la Barcelona ni umbali wa Kilometa 93.


Barcelona Reus Airport.. Hapa napo umbali wake mpaka kufika Barcelonatown ni Kilometa 93 mtu wangu.


Ndani ya Ujerumani mtu wangu, hapa ni Dusseldorf Airport.. Kutoka hapa mpaka kufika katikati ya Jiji la Dusseldorf ni Kilometa 49 pia.

Picha za Viwanja 10 vya ndege vilivyo mbali zaidi na Miji Duniani.. - MillardAyo.Com
 
Mleta mada unatulazimisha kuwa na gear box kuhusu ukweli wa hizi taarifa. Tembelea Paris Vatry Airport halafu uje tena
 
Mleta mada unatulazimisha kuwa na gear box kuhusu ukweli wa hizi taarifa. Tembelea Paris Vatry Airport halafu uje tena
nikipepeta pumba chagua chuya ila nimeweka chanzo cha taarifa ukija njoo na masahihisho siyo kutuacha weupe kizani
 
Ilinichukuwa 20min kutoka Frankfurt airport mpaka mjini na ni 12km tu.
Kwa kweli sijaelewa hapo maana kama naelekea London ni lazima nishukie Heathrow airport maana ni karibu zaidi na itanichukua nusu saa tu kufika mjini.

Charles de Gaulle airport ndio iko karibu na jiji naomba unieleweshe kidogo

Nakuja Tanzania halafu nashukia kigoma airport then nachukua train au
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Back
Top Bottom