Picha za vivutio wilayani Kyela,nchini na nje ya nchi ,kila siku nitakuwa naweka picha moja,picha zote nimezipiga mwenyewe kwa kutumia kamera na simu.

House Sparrow-jina la ndege kwa hisani ya Mwalimu,mtunzi wa vitabu ,mpiga picha na mtaalamu ndege ndugu Mustapha Semeni Kayoka
1092800
 
AHSANTE MKUU, BEI GANI HIKI CHUMBA?
Ni TZS
AHSANTE MKUU, BEI GANI HIKI CHUMBA?
Ni TZS 100,000 ni nyumba ndogo inajitegemea ina jiko dogo,na sebule kubwa yenye makochi mawili na meza ya kusomea au kuandikia ikiwa na taa yake pembeni,nimeshindwa kuupload picha za sebule sababu faili ni kubwa na JF wana limiti na faili ambazo unaweza kuupload,pia kuna WiFi vyumbani
 
Kikolo mwaga mipichapicha bana ya Kyela,Tokyo, Kiwira kule, KK,Rungwe story nyingi sana watu tunasubiri picha usituchanganye mara Azania front mara twin tower hazipo Kyela hizi?
Tuoneage huruma wenzio
Ama mwenye camera kachukua tukuletee🤔?
 
Kikolo mwaga mipichapicha bana ya Kyela,Tokyo, Kiwira kule, KK,Rungwe story nyingi sana watu tunasubiri picha usituchanganye mara Azania front mara twin tower hazipo Kyela hizi?
Tuoneage huruma wenzio
Ama mwenye camera kachukua tukuletee🤔?
Hapana mambo tu yameingiliana hard disk yangu yenye picha ilianguka kwa hiyo haisomi,najipanga kuipeleka kwa mafundi waangalie kama wanaweza kuretrieve data zote,wewe una kamera gani?isije kuwa una kamera ya simu lakini,pia nimepost hivi karibuni picha za ndege ninaowapiga hapa Kyela sijui kama umewaona.
 
Malafyale Kyela town pale pazuri sana aisee mji umepangika vizuri sana

Sasa zile barabara zenu waweke Lami zote ili papendeze vizuri.

Kyela ndio home kwetu huwa napata feelings flani kila nikila samaki aina "MBASA" au vitui au dagaa Nyasa wale wakubwa na Ugali wa muhogo .

Ila kyela kwa gesti ni noma kila kona kuna gesti aisee watu wanapenda papuchi si mchezo hahahahah
 
Hii picha niliipiga kwa simu nilipokuwa jijini Atlanta Marekani,hapa ndio makao makuu ya ya shirika la utangazaji la CNN na pia pana hoteli maarufu inayoitwa OMNI HOTEL ,Atlanta ni kati ya majiji makubwa nchini Marekani .Leo nitazungumzia kidogo juu ya vijana ambao hawajawahi kufika Marekani na wanataka kwenda Marekani,kwa wale mliowahi kufika au mnaishi Marekani nadhani haya nitakayoongelea mnayajua zaidi.Kwanza nikiri kabisa kuwa Marekani ni dunia nyingine,hakuna nchi ambayo inaifikia Marekani karibu kwa kila jambo,si miundo mbinu,maendeleo ,fursa,teknolojia n.k. pia wenzetu hawajifikirii wao tu kama taifa bali wanafikiria nadhani miaka 200 ijayo,hii Marekani ya sasa tunayoiona misingi ya ustawi wake haikuanza miaka ya jana ni kizazi kingine kilichopita. Sasa nije kwenye suala lemnyewe la maisha ya Marekani,Marekani kama Marekani ni taifa lenye fursa nyingi lakini pia maisha ya Marekani si lele mama kama tunavyodhani huku kwenye vijiwe vyetu vya kahawa,Marekani kugumu,kunahitaji mtu kujituma,ukiwa mvivu au mtu wa kusubiri dili basi Marekani haikufai,wenzetu wanafanya kazi kwelikweli,bila kufanya kazi maisha ya Marekani utaona shida hutayaweza,tatizo la kutofanya kazi ndio linawakumba Wamarekani Weusi wengi,ambao nao huwachukia hata watu weusi wenzao kutoka bara la Afrika.Marekani ni nzuri ukienda kwa malengo na ukiwa na ''makaratasi''ajira zipo nyingi ,lakini ni ajira za muda /masaa na kama huchagui kazi basi mambo yanakuwa sio mabaya. Pia kuhusu maisha kwa hakika yapo kwa kila daraja ,vyakula ni bei ya chini na hata nguo kuna maduka aina mbalimbali yale ya bei kubwa ,bei ndogo,mitumba n.k. Nguo inayouzwa maduka fulani kwa usd 300 unaweza kupata kwenye maduka mengine kwa USD 30 au usd 40 .Kuna maduka ya Wahispania na hata Wahindi haya ni kama visupermarket vidogo huko kunakuwa na vyakula vingi vyetu sisi weusi,lakini pia Marekani tofauti na huku kila kitu kipo kwa mpangilio ,hakuna kwenda kukopa kwa Mpemba,na kodi inakatwa kwa kila kitu,bei ya kitu iliyoandikwa sio bei ambayo unaenda kulipa,tofauti na huku kitu kikiandikwa TZS 20,000 unalipa hiyo hiyo lakini Marekani kitu kinaandikwa USD 10 lakini kulipa unaenda kulipa USD 12 au zaidi .Kifupi Marekani ni kujituma hakuna lelemama au kupoteza muda kupiga porojo kama huku kwetu,maisha ni magumu kwa asiye na makalatasi/vibali.Kuchangia ruksa kwa yeyote.

1102295
 
Back
Top Bottom