Picha za vivutio wilayani Kyela,nchini na nje ya nchi ,kila siku nitakuwa naweka picha moja,picha zote nimezipiga mwenyewe kwa kutumia kamera na simu.

  • Thread starter Tupilike Mwakajumba
  • Start date

Tupilike Mwakajumba

Tupilike Mwakajumba

Senior Member
Joined
Apr 14, 2019
Messages
107
Points
250
Tupilike Mwakajumba

Tupilike Mwakajumba

Senior Member
Joined Apr 14, 2019
107 250
Kuanzia leo nimeamua kupitia jukwaa hili kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini hususa wilaya yangu ya Kyela ,mkoa wa Mbeya na sehemu nyingine ambazo natembelea nikiwa hapa hapa Tanzania na nje ya nchi,hobby yangu kwa sasa ni upigaji picha za mnato,napiga picha za wanyama,ndege,wadudu,majumba,sehemu ninazotembelea ,matamasha .kwa sasa naishi wilayani Kyela .

Naitwa Tupilike Mwakajumba,upigaji picha za mnato nimejifunza mwenyewe kwa kupitia YouTube Video clips na kujisomea makala mbalimbali,ni hobby ambayo nimeianza baada ya kustaafu kazi.Sio kwamba nimebobea sana katika upigaji picha za mnato lakini angalau nina mwanga kiasi kuhusu upigaji picha,kamera na lensi hasa upande wa Canon,ruksa kuchangia.Nakaribisha watalaamu wa ndege na wadudu waweze kutaja majina ya wadudu na ndege mbalimbali ambao picha zao nitaanza kuziweka hapa,baadhi ya picha ni zile nilizozipiga nikianza kujifunza upigaji picha na hazilko katika ubora unaostahili lakini zinabaki kuwa ni kumbukumbu nzuri,ndege wengi nimewapiga hapa Kyela na baadhi Tegeta jijini Dar Es Salaam .Kuwapiga hawa ndege natumia lens ya Canon 70-200mm ambayo kwa upigaji ndege si nzuri sana,hii lensi ni kwa ajili ya portrait lakini inabidi kutumia kile nilicho nacho.

Karibuni sana.Kila siku nitakuwa naweka picha moja za vivutio mbalimbali au matukio tofauti.Hapa chini ni picha ya kiboko akiwa na familia yake nilioyopiga karibu na Matema Beach ,Kyela.
8b2b2230-jpg.1072460
 
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2007
Messages
22,615
Points
2,000
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2007
22,615 2,000
Utuambie na sehemu nzuri za kufikia kama hotel na mengineyo.. tuje kutalii
 
E

E2BK

Senior Member
Joined
Jul 8, 2012
Messages
102
Points
225
E

E2BK

Senior Member
Joined Jul 8, 2012
102 225
Utuambie na sehemu nzuri za kufikia kama hotel na mengineyo.. tuje kutalii
Ukiwa na shemeji Ngonga beach ( kwa mwamunyange kama wengi wanavyoita) panaweza kukufaa sana vyumba vyao vizuri.

Ukiwa na Muda mzuri Matema Beach itakua nzuri zaidi (angalia wimbo wa Tamu wa yule kijana wa wasafi) beach ni kubwa Resort zipo nyingi utajichagulia kutokana na uwezo wako.

Sehemu zote hizo usafiri wa uhakika, hali ya hewa ni joto kiasi maana wengi mmekariri kwamba mbeya yote ni baridi mwanzo mwisho.Sent using Nokia ya tochi
 
D

Deceiver

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2018
Messages
471
Points
1,000
D

Deceiver

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2018
471 1,000
Huyo mnyama kiboko nae unamuita kivutio?
Mi labda nione picha ya mwanamke wa kinyakyusa hasa aliyejazia ndio naweza sema ni kivutio.
Eti hata fisi ni kivutio. Are you people mad???
 

Forum statistics

Threads 1,285,935
Members 494,834
Posts 30,879,477
Top