Picha Za Vijana Bungeni: Report Kamili - Week 1

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Source: herman mwampyate: RIPOTI KAMILI





attachment.php

Bunge la 2010-2015 ni la vijana, mandhari na kila kitu kinabeba tafsiri hiyo na hapa kuna ripoti kamili ya kilichochukua nafasi mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 10.


attachment.php

Bunge.​

Jicho la Ijumaa Wikienda bungeni lina tathmini ya jumla kuwa bunge jipya lina idadi kubwa ya vijana kuliko wazee, tofauti na ilivyozoeleka miaka ya nyuma.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho pekee kinachoongoza kwa kutumbukiza wazee mjengoni, ingawa vijana ni wengi zaidi, kikifuatiwa na Chama cha Wananchi (CUF).


attachment.php

John Mnyika, Ubungo.​

Chama cha NCCR-Mageuzi, ndicho kilichotia fora zaidi kwa kuingiza wabunge wanne na kati yao robo tatu ni vijana chini ya umri wa miaka 30, isipokuwa mwana mama Agripina Zaitun Buyogera wa Kasulu Vijijini.

NCCR kimevunja rekodi ya CHADEMA katika bunge lililopita, wakati mbunge wake, Zitto Zuberi Kabwe alipoingia mjengoni akiwa na umri wa miaka 28, hivyo kuwa kijana mdogo zaidi kutoka jimboni.


attachment.php

Mchungaji Peter Msigwa, Iringa Mjini.​

Safari hii, Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR) ndiye mbunge mdogo zaidi ambapo ameingia mjengoni akiwa na umri wa miaka 24.

JUMANNE, MPAKA ALHAMISI ILIYOPITA

Idadi ya wabunge waliowasili kwa ajili ya kujisajili ilikuwa ndogo Jumanne, siku iliyofuata (Jumatano) iliongezeka lakini walifurika Alhamisi ambapo ndiyo ilikuwa mwanzo wa utambulisho bungeni.

attachment.php

Catherine Magige, Viti Maalum (UVCCM- Arusha) .​

Mandhari ya Jumatano yalikuwa ni yenye kuchangamka, wabunge wakipongezana kwa kufanikiwa kushinda, wengine wakirejea na wale waliofanikiwa kwa mara ya kwanza.

SLAA, MBOWE WAITEKA DOM USIKU

Msafara mkubwa wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Willibrod Slaa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe uliwasili Jumanne usiku mjini Dom na kufanya mkutano kwenye makao makuu ya chama mkoa.

attachment.php

David Kafulila, Kigoma Kusini.​

Mkutano ulipambwa na shamrashamra, wakazi wa Dom wakimshangilia Slaa alipokuwa anawasili na hata alipoanza kuhutubia.

Hata hivyo, baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu' kuwasili kwenye mkutano huo, wananchi walipoteza umakini kwa Slaa na kuanza kumshangilia shujaa huyo wa Bongo Flava.

attachment.php

Zitto Kabwe, Kigoma Kaskazini.​

Busara za Slaa, zilimuongoza kumwita mbele Sugu a.k.a Mr. II aweze kuwasalimia wananchi kwa uwazi na baada ya hapo mkutano ulifungwa.

SITTA AVUTA HISIA

Jumatano majira ya saa 5 asubuhi, Spika wa Tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta aliwasili bungeni kujisajili na kuzungukwa na umati mkubwa wa watu, wengi wakiwa ni waandishi wa habari na wabunge.


attachment.php

Ezekia Wenje, Nyamagana.​

Akiwa mwenye uchangamfu, alikuwa akiwatania wabunge hasa wale waliopita mbali naye, huku akiwakumbusha kwamba yeye ni mgombea wa uspika.

HARUFU MBAYA BUNGENI

Dalili ya hatari ndani ya CCM na bunge, zilionekana kwenye viunga vya bunge kutokana na kampeni za waziwazi ambazo zilikuwa zinaendeshwa.

attachment.php

Lucy Mayenga, Viti Maalum (Wanawake-Shinyanga).​

Makundi ya wazi yalionekana, upande mmoja ukitaka Sitta apite, wakati mwingine ukishinikiza aenguliwe mapema.

Upande mmoja ulikuwa ukiwaomba wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM (CC), wakate jina la Sitta kwa kile walichodai kwamba matokeo ya kushuka ilichopata chama hicho katika Uchaguzi Mkuu uliopita yalisababishwa na yeye.


attachment.php

Halima Mdee, Kawe.​

Hata hivyo, upande wa pili, walidai Sitta ndiyo sababu ya ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu 2010, vinginevyo chama hicho kingeangushwa mwereka mkubwa.

Walidai kuwa uongozi wa Sitta ulionesha wananchi kwamba ndani ya CCM kuna watu makini walio tayari kujikosoa ndiyo maana wakakipigia kura.


attachment.php

Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu, Mbeya Mjini.​

KIGOGO AVUJISHA SIRI YA KAMATI

Jumatano, saa saba mchana, kigogo mmoja wa chama alivujisha siri alipowasili bungeni baada ya kumnong'oneza mbunge mmoja kwamba mwaka huu spika atakuwa mwanamke.

Sababu alizotoa, ndizo zilizoonekana katika taarifa rasmi kwa vyombo vya habari, iliyosainiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati siku hiyo hiyo jioni.



WAHESHIMIWA CLUB 84

Jicho la Ijumaa Wikienda lilizama ndani ya Club 84 ambayo ina jina kubwa na kujionea waheshimiwa kadhaa (majina tunayo) wakijirusha, huku wengine wakiondoka eneo hilo karibu na majogoo.

BUNGENI KIMYA

Alhamisi kwa watu wengi ilikuwa kama msiba bungeni, wakisikitikia uamuzi wa kamati, ikiwemo wafanyakazi wa bunge lakini hakukuwa na jinsi.


attachment.php

Kikao cha kamati ya Wabunge wa CCM, kilikaa kuchagua kati ya majina matatu, Anna Makinda, Anna Abdallah na Kate Kamba ambapo jina la Makinda liliposhinda, shamrashamra zilianza.

Wakati hali ikiwa hivyo, CHADEMA kilikuwa ‘bize' na vikao, kuunda Kambi ya Upinzani Bungeni.

attachment.php

Idd Azzan, Kinondoni.​
DOM GESTI, HOTELI

Tathmini Dodoma, kila mtaa kuna gesti na hoteli kadhaa na kwa hesabu, bila shaka ndiyo mkoa wenye gesti na hoteli nyingi Tanzania.

MADENTI U-DOM

Wanafunzi wanaosoma Chuo Kikuu cha Dodoma (U-Dom), walionekana wakirandaranda kwenye hoteli za waheshimiwa, na walipatikana pia mitaani wakati huu wa bunge jipya.


30.JPG

Neema Mgaya Hamid (Viti Maalum, UVCCM-Dar)​

NI MREMBO?

Bunge lililopita lilikuwa na warembo wengi lakini mwaka huu ni ‘funika bovu'.

Nani mkali ni mchuano kati ya Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), Catherine Magige ‘Pamela', Mbunge Viti Maalum CCM (Geita), Vicky Kamata ‘Madame V' na Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee.


attachment.php

Vita Kawawa,​

Wengine ni Mbunge wa Viti Maalum CCM (Shinyanga), Lucy Mayenga, Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA (Kigoma), Mhonga Ruhanywa, Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), Neema Mgaya Hamid na Mbunge wa Viti Maalum CCM (Zanzibar), Tawhida Cassian Gallus.

HANDSOME BOYS

Ingizo jipya la wabunge vijana linafanya mchuano uwe mkali katika bunge hili.

attachment.php

Mnyika na David Silinde wakibadilishana mawazo.​

Zitto, Mkosamali, Sugu wamo kwenye orodha, halafu wapo wengine kama Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika, Mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba na Mbunge wa Mbozi Magharibi (CHADEMA), David Silinde.

Wengine ni Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA), Ezekia Wenje, Mbunge wa Ilemela (CHADEMA), Highness Kiwia, Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema na wengineo.


attachment.php

Sugu na Mnyika wakipata msosi.​
 
Subira yavuta heri . . . .
 

Attachments

  • Picha 2.jpg
    Picha 2.jpg
    40.5 KB · Views: 733
  • Mnyika.jpg
    Mnyika.jpg
    32.5 KB · Views: 728
  • Kula Muhimu.jpg
    Kula Muhimu.jpg
    49.3 KB · Views: 688
  • Zitto.jpg
    Zitto.jpg
    33.2 KB · Views: 697
  • Ze Two.jpg
    Ze Two.jpg
    36.8 KB · Views: 712
  • Battle.jpg
    Battle.jpg
    47 KB · Views: 684
  • Wenje.jpg
    Wenje.jpg
    45.8 KB · Views: 687
  • Shinyanga.jpg
    Shinyanga.jpg
    44.3 KB · Views: 716
  • Arusha.jpg
    Arusha.jpg
    34 KB · Views: 756
  • kafulila.jpg
    kafulila.jpg
    42.3 KB · Views: 700
  • Halima.jpg
    Halima.jpg
    40.7 KB · Views: 688
  • Sijui nani.jpg
    Sijui nani.jpg
    40.3 KB · Views: 693
  • CCM No 1.jpg
    CCM No 1.jpg
    39.2 KB · Views: 120
  • Bunge.jpg
    Bunge.jpg
    43.3 KB · Views: 786
  • Sugu.jpg
    Sugu.jpg
    51.7 KB · Views: 685
  • Master.jpg
    Master.jpg
    51 KB · Views: 686
  • RIPOTI.jpg
    RIPOTI.jpg
    58.7 KB · Views: 739
Mashallaaaah . . . . nadhani sasa ziko sawa . . . .

We hope hawa Wabunge vijana hakika watapigania maendeleo ya nchi . . . moto chini . . . moto juu. Kazi na dawa!
 
They are looking really good, but hapo kwenye kuchakachua sasa, si sketi si suruali, lets wait and see!!:bowl:
 
Mashallaaaah . . . . nadhani sasa ziko sawa . . . .

We hope hawa Wabunge vijana hakika watapigania maendeleo ya nchi . . . moto chini . . . moto juu. Kazi na dawa!
Mabadiliko hayawezi kuletwa na hawa wabunge wa CCM labda hao wa Chadema tu. Kwani Superman umesahau bunge lililopita pia kulikuwa na vijana kambi ya CCM? kwani ulisahau walivyokuwa wakilalamika kisha wanaishia na kauli ya naunga mkono kwa asilimia 100?
Hawa ni vijana mizigo tu bungeni. Nategemea kuona Changamoto toka kwa vijana wa Chadema na NCCR period. Wengine hao tulishajua wamekwenda kama visusio vya wakubwa. Hahahahahaha
 
Eee Mola walinde vijana wetu wa CHADEMA na Wengine wa Upinzani wenye nia ya dhati ya ukombozi wa taifa letu wasije wakakamatwa na Makokoro haya ambayo yameingia mjengoni wala hata hayajui yanaenda kufanya nini. Wasaidie hawa wanamabadiliko wasijewakachakachuliwa. Aaaamen
 
Jama hao vijana, hizo ni sodaaa au kuna kakonyagi, hapo kwa meza ya ngika na sugu, naona kuna vitu vigumu pale kwa jamaa haoinekani vizuri, wamemuweka chambo kumbe na wao kwenye soda ni danganya toto. Haya tusubiri kipyenga kipulizwee, hoja na mijadala mikali ikianza. sikukuu njema!!
 
Nimependa hii sooo simple . wanakamata mdudu na ugali

attachment.php

wapeni miezi miwili tu, hamtawaona tena sehemu za hivyo! ha ha ha! otherwise picha imetulia, naona waheshimiwa wanaaga-aga maisha ya kigetogeto!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom