Picha za utupu isiwe kitanzi katika jamii kwani mbinu za upatikanaji wake ni wakijasusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha za utupu isiwe kitanzi katika jamii kwani mbinu za upatikanaji wake ni wakijasusi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mbasamwoga, Jul 21, 2011.

 1. m

  mbasamwoga Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dunia imebadilika sana hasa kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Vifaa vingi vya kiteknolojia ni vigeni miongoni wa wanajamii wetu hivyo hata matumizi yake ni ya kubahatisha. Vifaa kama simu za mikononi, laptops, ipod, saa, miwani,modem, n.k. Kwa bahati mbaya sana vitu hivi vinamatumizi mengi kuliko tunavyofikiria! Simu inaweza kutumika kama kupiga na kupokea simu,saa,redio,computa kwa ajili ya kukuunganisha mtandaoni, camera, tochi,kalculator, kifaa cha kuhifadhi siri n.k. Haya ni matumiz machache tu miongoni mwa kifaa hicho kimoja yaani simu ya mkononi.
  Ukweli ni kwamba wengi wetu hatuna utaalamu na vitu hivi, mtumiaji anaweza kujipiga picha akiwa ndani kwake, ofisini kwake, ama akiwa sehemu yoyote ya starehe au mapumzikoni bila kuwa na nia mbaya ya kuzisambaza kwa jamii lakini bila kutarajia mwisho wa siku akajikuta matatizoni kutokana na picha zake alizopiga kwa nia nzuri tu.*
  sasa kwanini picha hizi zisiwe kitanzi kwa jamii, na jinsi upatikanaji wake ulivyo:
  • picha zinaweza kuaptikana kwa njia ya mtandao bila mmiliki kujijua kwamba akiwa kwenye mtandaoni simu yake ama komputa yake inaweza kuonekana kwenye watumiaji wengine wenye vifaa hivyo wakatumia vitu vyake kama picha na ujumbe mwingine wa siri bila yeye kujijua. (njia hii pia inaweza kutumika pia kuibia nyaraka za siri, mitihani kumbukeni out, kumbukeni *mtandao wa *wikleans unavyodiriki kuiba nyaraka hata marekani kwenye sekta nyeti)
  • kuibiwa simu ama komputa hivyo mhalifu akatumia fursa hiyo kupata siri hizo.
  • kupeleka kifaa matengenozoni kwa fundi ambaye anaweza kutumia siri za mteja wake vibaya(kumbukeni mtandao wa ze utamu na picha chafu za wanafunzi wa saut - mwanza).
  • marafiki wabaya wenye lengo la kukuharibia jina au sifa katika jamii
  • wahalifu waliotumwa kwa lengo la kulipiza kisasi au kukudhalilisha hasa ukiwa na wadhifa unaolipa sana, ukiwa hupendi rushwa so wanafanya hivyo ili kukukomoa au kukufukuzisha kazi.
  • kutengeneza picha feki zenye sura halisi ya mtuhumiwa.
  watanzania wenzangu tujihadhari na kuchukua maamuzi ya ghafla juu ya jambo hili wakati mwingine watuhumiwa wanakuwa watu safi sana kuliko tunavyowafikiria.
   
 2. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Imekuwaje hadi unaandika haya?
   
 3. m

  mataka JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 287
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  hata mimi nashangaa
   
 4. P

  Penguine JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Kweli wewe ni MbasaMWOGA, umeandika ktk namna ambayo inaashiria kwamba PICHA ZAKO ZA UTUPU zimepotea na hujui zilikopotelea hivyo unajihami!

   
 5. Wizzo

  Wizzo JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  afu nmeshakujua na nmeshajua unamtetea nani...haya bwana jitahd jamii itaweza kukuelewa
   
 6. k

  kakolo Senior Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Good point, itungwe sheria yaani inayowabana wanaopata Habari kwa njia ZISIZO HALALI. Kama inavyowa cost NoW.Mawazo yangu.
   
 7. V

  Vonix JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wewe mbasamwoga unazunguka nini si useme yaliyokusibu!!!
   
 8. S

  Siimay Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahaha jaman jamaa mwambieni anyoshe maneno yamemkuta huyo
   
 9. M

  Martinez JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Wachangiaji inaonekana mmeathiriwa na mchangiaji wa kwanza. Mada ina ukweli na umuhimu wa pekee. Tunaona kila siku magazeti ya udaku yanatoa picha za siri za watu walizopigwa bila ridhaa yao au wakati mwingine zilizoibwa. Ikumbukwe kuwa kila binadamu ana faragha. Sasa mtu akitegesha kamera akakupiga unabadili nguo halafu akaitungia leading stori utajisikiaje? Mfano mzuri ni gazeti la amani la tarehe 21. Yule afande waliyemtoa uchi hana kosa lolote maana yupo NDANI kwake. Na hakujipiga picha bali alipigwa picha. Fitina, chuki nk
   
 10. m

  mchongi Senior Member

  #10
  Jul 24, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nahisi yamemkuta huyu maana ni kama anatuadithia hv.. we sema wazi kilichotokea nasi tuchangie
   
 11. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  weka picha bana tunataka vitu practically
   
 12. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  pole kama yamekusibu ndio ukubwa huo.......
  utaumia kwa kuwa betrayed ila maumivu yatakuwa ya muda tu....sooon utamove on na life yako...
  niulize mie!
   
Loading...