PICHA za UFUNGUZI na RAIS wa BURUNDI: CRDB BANK YATUA BURUNDI KWA KISHINDO

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=1][/h]


Jengo la Benki ya CRDB Burundi.

Rais wa Burundi Piere Nkurunziza akiwasili katika sherehe za ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB jijini Bujumbura, Burundi. Benki ya CRDB imekuwa Benki ya kwanza ya kizalendo kufungua tawi lake nchini Burundi.

Rais wa Burundi,Mheshimiwa Piere Nkurunziza akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB nchini Burundi.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei.

Raisi wa Burundi Mheshimiwa Piere Nkurunziza akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB Tully Esther Mwambapa alipokuwa akiwasili katika sherehe hizo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Dkt. James Nzagi (Kushoto) na Katibu wa Benki hiyo Bwana John Rugambo(2 kushoto) na Meneja Mkuu wa Benki ya CRDB Nchini Burundi Bw. Bruce Mwile.

Raisi wa Burundi Mheshimiwa Piere Nkurunziza akiwa katika ya pamoja na uongozi wa juu wa Benki ya CRDB.

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB nchini Burundi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzano kutoka Dar es Salaam.
 
Safi sana haya ndiyo maendeleo tunayoyataka,kuwa na multi national companies za kutosha!
 
Thanx, but hii ni habari ya biashara sio siasa. tread hii ni kwa ajili ya political affairs
 
Thanx, but hii ni habari ya biashara sio siasa. tread hii ni kwa ajili ya political affairs

Ni Sasa kwanza iliyowezesha CRDB kuwa BURUNDI then Biashara... Mafanikio ya KISIASA ndio yamewezesha Uhusiano wa KIBIASHARA... Kama haukubali nenda kawekeze Afghanistan bila Governnment Blessings
 
Ongera Charles Kimey na CRdb walioficha hela Uswis ungekuwa na akili kama ya kwako tatizo la ajira nchini lingepungua.
 
Hongera CRDB. Jambo la kufungua matawi katika nchi jirani tulianza kulipigia kelele miaka kadhaa iliyopita, hususan baada ya benki hii kupata mtaji wa kutosha na kujitwalia sehemu kubwa ya soko la ndani. Ni muhimu kuwezesha shughuli za kibiashara za Watanzania katika nchi zinazotuzunguka na pia kuwezesha biashara za nchi hizo nchini hasa kuhusiana na bandari ya Dar es salaam. Sasa tunatarajia CRDB itafungua matawi mengine nchini Zambia, Malawi(??), Uganda, Kenya, Congo DRC na Rwanda. Hii itakuwa fursa kubwa kwa Wafanyabiashara wa Tanzania kupanua wigo wao and venture out ! We should now stop politicking and talk real business with our neighbours.
 
Waende na Kenya na Rwanda!!! Tunataka waende kwenye competition kujipima nguvu siyo kwa wadhaifu bana!!
 
Angalau CRDB mmejitahidi sana. lakini kuonyesha ukomavu kafungueni Kenya ili tuone ushindani wenu kati ya KCB na nyie huko Nairobi. All in all mwanzo mzuri mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
 
isije kuwa inaitwa tu crdb kumbe ni ya [wawaziri] wetu maana hii nchi haieleweki kabisa.
 
Hongera sana CRDB kwa kututoa kimasomaso wayz. Hiyo ni hatua muhimu sana. Nasubiri tawi litakalofunguliwa Jijini Nairobi.
 
nashangaa mmefurahi kweli, na wakati wawekezaji ndio wanafaidika zaidi. Benki si ilishabinafsishwa bwana. si tunafaidika nini sasa hata kama wakifungua tawi mbinguni.

History

CRDB Bank was formed when the former Cooperative Rural Development Bank which was wholly government owned was privatized, recapitalized and restructured. DANIDA played a significant role in re-structuring the new institution and is a part owner of the new bank.

Ownership


As of December 2011, the stock of CRDB Bank is owned by the following institutions and individuals:
CRDB Bank Stock Ownership

<tbody>
</tbody>
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom