Picha za ndani ya ndege,Bush,Obama,Clinton etc wakielekea south africa kwenye mazishi

Do! Wale wa mbezi zote, yaani mbezi ya kimara na mbezi ya beach wanajiuliza nyumbani watafika saa ngapi make foleni zinatisha, walio wengi wanaenda nyumbani kupiga mswaki na kubadili nguo afu warudi ofisini.

Walio wengi Dar kuondoka ofisin saa 11 kufika nyumbani saa sita usiku, kurudi kesho yake kazini kuamka saa 10. Alfajiri. Ndo maana walio wengi wanasisitiza mpango wa uzazi, hakuna muda wa kutoa madozi kwa wenza wao! Obama endelea kutanua make hapa Tanzania CCM ilisha tuondolea matanuzi hayo

HAta utendaji wa kazi serikalini na sehemu zote maofisini hauwezi kuwa wa ufanisi
 
Kama Laptop kiswahili chake ni kompyuta mpakato, Air Force One ni nini? Kwa wataalamu wa kiswahili tu.

LAPs ni mapaja Top juu ....Laptop kwa kuwa ilibuniwa kuweza kuwekwa juu ya PAJA.

Air Force ni ndege ya kijeshi...rais ni amri jeshi mkuu inafaa kuweka code ya one ..kwa ndege ya amri jeshi mkuu..."my thoughts"
 
hiyo picha ya pili nadhani hao waliosimama ni wasaidizi wa rais. So relaxed na mmoja hapo mikono mifukoni. Ingekuwa ni huku ungeona kanyooka kama dereva wa kibajaj.
 
Behind-the-scenes photos from Air Force One show the Obamas mingling with the Bushes and Hillary on journey to South Africa for Mandela's memorial


1461853_bush_jpga67b5d185d5878455939f60e75968d81

1461854_bush2_jpg258227b8fbfa9ecf609af3f016883674

Daaaah, hivi jmn hii inaweza kutokea hapa kwetu bongo? Yaani viongozi wa upinzani na chama tawala wakakaa hivi pamoja na kuchat?
 
hii level ya demokrasi ni ngumu sana kufikia huku kwetu mtu kama wassira anaweza zungumza mbele ya kadamnasi kwamba nafasi ya wapinzani kwenda ikulu kunywa chai haipo!!!! alafu ndio waziri huyo!!!
 
hii level ya demokrasi ni ngumu sana kufikia huku kwetu mtu kama wassira anaweza zungumza mbele ya kadamnasi kwamba nafasi ya wapinzani kwenda ikulu kunywa chai haipo!!!! alafu ndio waziri huyo!!!

Sie tunatabu viongoz wetu wanaongea vitu visivyo hata na maana,Hasa chai ya Ikulu ni tabu nayo?
 
Ubabe wote ule wa Bush anamkubali Obama kiac hiki?

Wenzetu wamefanikiwa kujenga mfumo wa kiutawala pamoja na kuwa na maslahi ya taifa hivyo ukishindwa unakubali matokeo na kuweka mkakati wa nini kifanyike uchaguzi ujao uchukue dola. Sie bado tupo katika hatua ya "ukinichagua nitajenga daraja, nitaleta meli mpya na kuchimba visima virefu kila kijiji" alafu usipochaguliwa unakwenda na ahadi zako na mgombea mwenzako humsalimii
 
Back
Top Bottom