Picha za miili ya Wanafunzi 12 walio ungua kwa moto Idodi

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
Picha za tukio zima la moto. Mtaniwia radhi kwa wale watakao pata usumbufu kwa kuangalia picha hizi.
1251010732_the_main_entrance_to_the_center.jpg

Hili ndo bweni walilo kuwa wakilala wanafunzi inasemekana lilikuwa linabeba zaidi ya wanafunzi 400 kama mnavyo ona mlango ni mmoja tu wakuingia na kutokea.

Naibu waziri wa Elimu na ufundi Mwamtumu Mahiza na badhi ya viongozi wakiangalia maiti.

Maiti za wanafunzi 12 walio ungua moto.


Mabaki ya miili ya wanafunzi 12 ilivyo ungua.


Naibu waziri Mwamtumu akimwaga chozi.


<HR style="BACKGROUND-COLOR: #ebebeb; COLOR: #ebebeb" SIZE=1><!-- / icon and title --><!-- message -->
<!-- google_ad_section_start -->
Mabaki ya miili ya wanafunzi wa shule ya sec.Idodi.
Niwieni radhi kwa wale watakao pata shock.



Huyu ni majeruhi Sabrina Abdulahiman<!-- google_ad_section_end -->


Hivi ndivyo wanafunzi walivyo teketea kwa moto
<!-- / message --><!-- sig -->
<!-- google_ad_section_end --><!-- / message --><!-- sig -->
 
Last edited:

Mabaki ya miili ya wanafunzi wa shule ya sec.Idodi.
Niwieni radhi kwa wale watakao pata shock.



Huyu ni majeruhi Sabrina Abdulahiman
 
inasikitisha sana na kutia uchungu mno...mungu awapumzishe pema marehemu ndugu zetu. Amen
 


Wananchi na wanafunzi wakitafuta miili kwenye majivu



Hivi ndivyo bweni lilivyo teketea kwa moto.


Wanafunzi wa Idodi wakiwa wamekaa makundi makundi
wakingoja kuhesabiwa ili kujua idadi kamili ya walio ungua kwa moto




Waziri Mahiza akiwafariji wanafunzi
 
Ni tukio la kusikitisha sana. Tuwaombee marehemu Mungu aziweke mahali pema roho zao. Amen. Kwa ushauri siku za baadae ni vyema kukawa na practical trainig katika shule zote kuhusu namna ya kukabiliana na majanga kama haya. Enzi zetu tukisoma tulikuwa tunafundishwa namna ya kutumia ngazi za emergency hasa kwa kuwa tulikuwa na mabweni ya ghorofa. Ujenzi wa haya mabweni pia uangaliwe kuwa na milango ya emergency kama ilivyo katika mabasi ya usafiri.
 
Hivi serikali inashindwa kuweka mikakati kila bweni liwe na fire xtingisha 2 na ninakumbuka kuna somo lipo jinsi ya kujiokoa pindi majanga yanapo tokea sijui somo lile linaitwaje.
 
Haya majanga ya moto mashuleni yamekwepo muda mrefu tukianzia na lile la Shauritanga. Mpaka leo hii bado wizara haijafikiria namna gani mabweni yajengwe ili kuweka milango ya dharura. Nafikir iwepo exit doors hata sita kama si ghorofa. Na kama ni ghrorofa basi ile milango ya dharura iwepo na chini pia. i.e kila floor iwe na emergency doors not less than two. Inatia huruma na majonzi kumzika mtoto wako bila kumwona, itabaki kuwa ni pigo maishani mwako. Wazazi wenzangu poleni sana na mungu awape nguvu ya kusahau. Kama mzazi unaweza kupata permanent disability kabisa kwa jambo kama hili.
 
Poleni sana wafiwa wote na Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,amen. Hili janga ukifikiria sana utakuta kama haiingii sana akilini kama jengo wanalolala watu 400 lina mlango mmoja tu wa kutokea na kuingilia, huo uongozi wa shule unatakiwa kubeba lawama hizi zote kwa sababu hata kama ingekuwa huo moto sio mkubwa ila kwa kundi hilo kubwa kujiokoa kupitia huo mlango mmoja ukiambatanisha na hofu pamoja purukushani za huku na huko, lazima mtajikuta wote mmeisha humo ndani. UONGOZI WA SHULE UCHUKULIWE HATUA KWA KUFANYA HUO UZEMBE KURUHUSU WANAFUNZI HAO 400 KULALA KWENYE HILO JENGO LISILO NA EMERGENCY DOORS......HUU UZEMBE WA KUWEKA WANAFUNZI WENGI BWENI MOJA UTALETA MAJANGA ZAIDI HASA KTK MATUKIO KAMA HAYA.
 
Nina Uchungu lakini zaidi sana nina HASIRA! Nakubaliana na Ping Pong na sitaki mtu aseme ni bahati mbaya. Kwa aliyeona picha za tv atakubaliana kuwa inaonyesha wazi kuwa shule bweni lenyewe liko vichakani. Pili, ni ajabu kuwa katika karne hii ambayo serikali inajisifia kujenga shule nyingi za kata bweni la shule halina umeme na kulazimika wanafunzi kusoma kwa kutumia mshumaa!!! Na bado watu wanajisifu kuwa utawala wao umejenga sekondari nyingi kuliko tawala nyingine!
Lakini pia ninajiuliza sana hasa ninapoangalia ile maiti ya yule binti yetu pale juu. Hivi huu unaweza kuwa moto wa magodoro na mabati tu jamani?? mbona ninapoangalia vile binti yetu alivyogeuzwa majivu napata picha ya moto wa petroli??
 
Poleni sana wazazi, wanafunzi, waalimu na wote walioguswa kwa namna moja ama nyingine na kadhia hii.

Kama nchi, nadhani tuna tatizo la kutojifunza kutokana na majanga haya. Itaundwa tume, itatoa matokea na mapendekezo lakini hakuna hatua za makusudi zinazochukuliwa kutekeleza mapendekezo ya wataalamu. Hili si tukio la kwanza kutokea. Sasa cha kujiuliza wizara ilijifunza nini katika matukio yaliyopita?

Kadhia hii inaibua pia tatizo la kukosa umeme kwenye shule zetu na pia kutokuwapo kwa mazingira muafaka ya wanafunzi kujisomea.
 
Mungu azilaze mahala pema peponi roho za wanafunzi hawa, na awafariji na kuwapa moyo wafiwa wote. Bwana alitoa na Bwana ametwaa.
 
Ni uchungu mkubwa sana.......can't imagine pain waliopitia hawa watoto kabla ya kifo chao.....Mungu awalaze mahala pema peponi sana!
 
Nami nawapa pole sana wazazi na wanafunzi wengine wote walioathiriwa na janga hilo la moto,MWENYEZI MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREMU MAHALI PEMA PEPONI
 
Inasikitisha sana na inauma sana,nawapa pole wazazi wote waliopata msiba wa kuondokewa na watoto wao,mhhh jamani nimeshtuka sana na nimesikia vibaya sana!
 
Hivi serikali inashindwa kuweka mikakati kila bweni liwe na fire xtingisha 2 na ninakumbuka kuna somo lipo jinsi ya kujiokoa pindi majanga yanapo tokea sijui somo lile linaitwaje.



Emergency Evacuation Plan
  • Draw your building’s floorplan, then draw your evacuation
  • routes and a meeting place.
  • Make one drawing for each story of the building. Keep in a safe place and review often with your people.
  • Have maps ready for the following:
  • Closest evacuation centers.
  • Main and Alternative routes for leaving the area in North, South, East and West directions.
  • Meetup spots outside the affected areas. For example: I live approximately 50 miles east of a nuclear power plant. Should there be an accident or an attack and the wind is blowing in an Easterly direction, our plan is to head north and meet up in a town approximately 60 miles north of my area.
You should have at least two (2) escape routes from each room.
You should mark the locations of any escape ladders, or other special equipment.
You should mark the locations of fire extinguishers, smoke detectors, first aid kits, disaster 72 hour kit.
You should mark the locations of the shutoffs for gas, water, and electricity.
For people with medical conditions or disabilities, mark their location as well as the location of any special equipment they will immediately need

Government should think of such issues!!!!!!!!!!!!
 
Inasikitisha sana! Ni lazima serikali ifanye ukaguzi wa shule zote za bweni na kuhakikisha kwamba zina milango na madirisha ya kutosha kuwawezesha wanafunzi kutoka wakati wa majanga ya aina hii. Lakini pia kuwe na fire extinguishers kwenye kila shule, na wanafunzi wote waelekezwe namna ya kuzitumia.
 
OMG! I am shocked. Ee Mungu wapumzishe kwa amani, tayari moto huo na mateso ya kufa kwa maumivu makali yamewatosha.
I hate to say this but why Tanzania we take for granted maisha ya watu/ hakuna fire extinguisher, mlango mmoja na ni mashule mengi ni hivyo, hakuna huduma za kuzima moto na matokeo yatakuwa haya haya kila siku.
poleni wanafunzi,walimu na wazazi above all.
 
Poleni sana wafiwa/
Janga kama hili ni uzembe mkubwa ambao ulifanyika kwa nini ?hata fire ext/ kulikuwa hakuna? au watu walikuwa washajisahau?
 
Back
Top Bottom