Picha za Makamanda Vitani na Wapiganaji wao: CHADEMA yaweza kujifunza somo?

mhh...nadhani Chadema wanavaa magwanda yao kwa maana zao. Huwezi kuweka reasoning ya jeshi itumike kote. Vita hizi sio physical. we are in a mental battle ambapo thinking ya wengi inahitaji kubadilishwa!
 
e0AAAAABJRU5ErkJggg==

imgres
; zaidi ya mh Mdee na wengine wachache, sioni kama wapenzi wengine wanavaa sare zozote zinazojieleza,ambazo wengine wameshauri viongozi wavae pia. Ni kila mtu alivyotoka kwake anashiriki na kujiona anahusika. Hapo hata sijaongelea gharama za kuchapisha fulana na kuzigawa bure ambazo hata zimepelekea UFISADI mahala pengine.

8Pxhzl43146qEAAAAASUVORK5CYII=

Mnatamani kufanana na hawa? Mnafahamu what it takes kuwapendezesha hawa na hivyo vivazi? Unajua PAYE yako imehusika sana humo?

8D7uq0ilV2lBMAAAAASUVORK5CYII=

Kwa vipi hii iwe mbaya jamani? Labda mie nina matatizo ya kutopenda kubadilika. Ninaanza kujiogopa!
 
Uniformity is important.kuna mwalimu wangu aliniambia chanzo cha kuvaa uniform shuleni ni kuondoa utofauti(matabaka).nimesoma na watoto wa majaji,wakuu wa polisi,madaktari na wauza vitumbua na siku zote nilijihisi mwanafunzi.lazima tuwajenge wafuasi wetu nao wajihisi ni makamanda.
Heko mwanakijiji!

kwa hiyo matabaka yanaruhusiwa ukifika chuo kikuu au vyuo vingine mbalimbali?
 
Mkuu kwa mara ya kwanza nimeshindwa kukuelewa, na hoja yako imekosa mifano inayoeleweka ili kuiunga mkono. Naliona tatizo kubwa liko kwenye maneno haya... na si uniformity kama ulivyodai maana umetoa mfano wa vazi la CCM....Hebu angalia hapa kuna Uniformity...?

05_11_qv7s9r.jpg

mfano mzuri
 
Mkuu you have pointed an important issue which has been bothering me for a long time. I think we should now look beyond the robes. Since the hood does not make the monk, we must insist that issue-driven message, rather than costume, should be the rallying point of political campaigns. Mbona akina Obama na Blair walikuwa wanapiga kampeni wakiwa wamevaa suruali na mashati ya kawaida tuu? Wao walikuwa wanapiga kampeni juu ya real issues na jinsi vyama vyao vitakavyo-solve hayo matatizo.

Indeed, tena wanaohudhuria kwenye kampeni za vyama vya siasa huko Marekani huwa wanabeba bendera ya taifa lao. Ukumbi unapabwa na rangi za taifa lao, sio rangi ya chama fulani. Lakini hapa Tanzania ni tofauti. Kwa waliofuatilia zile kampeni mwaka jana, watu walijipamba kwa rangi na bendera za vyama vyao, nk. Our national flag was no where to be seen, which led me to think if the parties were actually campaigning for the national or party interests. Badala ya kutu-unite through our national flag, our political parties are dividing us through their party colours. Watanzania siku hizi tunaji-identify zaidi kupitia rangi za vyama vyetu kuliko rangi za bendera ya taifa. Unapita mitaani unakuta watu wametundika bendera za vyama vyao badala ya bendara ya taifa. Ukija mgogoro wa kidini who knows wakristu na waislamu nao wataji-identify kwa mavazi yao. Makabila nayo yatafanya hivyo hivyo.

Let's emphasize issues, not dresses. Wanasiasa wanaweza wakavaa kawaida tuu na wakawa na focus kwenye rallies. Let's not dress up our politicians more than we address the issues affecting us on a daily basis. Even if we want to dress them up, then let's try dressing up using our national colour. But the important issue is that our politicians should be more natural and place more emphasis on delivering the substance of their manifestoes. They should go for the substance and not for the form, for the latter would not help the average voter to make an informed choice. Tuvijunie zaidi rangi za taifa letu, sio rangi za vyama. Vyama vitakuja na kuondoka, but our national colour will always be there.

tanzania-flag.gif
 
This is craaaaaaaaaaaaaaaaappppppppppp

unaweza kujishionea gwanda kwa shilingi 25,000...mie pia nijnalo...

Kwani umefikia wapi katika kujivua gamba?
 
Ulichofananisha apo ni vitu viwili Tofauti,
1. Umeusisha chama na Serekali, elewa vazi la kichama aliwezi kuwa sawa na lakiserekali(Unapozungumzia jeshi unamaanisha serekali)
2. Sijawai kuona Chama chochote apa duniani kila mwanachama akiwa na sare za chama.
kwaiyo kwailo mkuu sikubaliani na ww kwamba CDM wanakwenda rong na mavazi wanayo tumia viongozi wao.
 
Napata tabu kuona kwamba hata wewe huwezi tofautisha kati ya jeshi na chama cha siasa! na nadhani huna uelewa wakutosha kuhusu mambo ya jeshi na usalama na kupelekea kufananisha dhana ya sare za jeshi na sare za chama cha siasa, sina uhakika kama unajua kwa nini wanajeshi wanavaa sare za namna ile au unasema tu kwa kubahatisha au kwa jinsi unavyodhani wewe. Kama unadhani sare ya mavazi ya ccm ndo inaleta mshikamano zaidi, je ni kweli ccm ya leo ina mshikamano? na kama mshikamano wao umepungua au kuzidi, je ni kwa sababu ya sare? Hivi mshikamano hautokani na ari,imani na mapenzi ya watu kwa jambo wanaloamini? una hoja gani hapo? cdm wanajenga hoja ambazo wanataka zikubalike na kuaminiwa na wafuasi wake,it's not a fashion show mr. mwanakijiji! kama wewe unaona magwanda hayakuvutii basi uelewe kuna wengine yanawavutia pamoja na mimi na hasa ukitupia shingoni ile scarf yenye rangi ya bendera! huna haki ya kufanya wengine wasipende magwanda kama ambavyo wengine hawana haki ya kulazimisha wewe na wengine na baadhi uliofanikiwa kuwashawishi wasipende magwanda. Nadhani umekuwa ukifatilia kampeni za uchaguzi marekani siku zilizopita,je wagombea na wafuasi wao ni kwa kiasi gani walikuwa wanavaa sare kuwakilisha vyama vyao? mimi kwa kiasi kikubwa nilikuwa naona bendera na alama mbalimbali kuwakilisha vyama vyao lakini suala la mavazi sikuona kama limechukua nafasi sana. Kuhusu watu kuwazunguka viongozi wa chama kwa kushikana mikono, unauliza hao wanaowalinda viongozi wanalindwa nani? jiulize bodyguards wa marais nao wanalindwa na nani? kwani wao hawastahili kuwa salama au ni wajibu wao!?
Tatizo lako ni kwamba huna sababu zenye mashiko kuhusu hayo magwanda zaidi ya kuwa unayachukia tu au huyapendi kama ambavo mtu mwingine anaweza akawa hapendi kuvaa suti na hiyo haizuii wengine wanaopenda kuvaa suti wasivae, hata mtu akisema kuvaa suti kunamfanya mtu aonekane decent, je decency ya mtu ipo kwenye suti au kwenye dhamira yake? wangapi wavaao suti si wastaarabu na wangapi wasiovaa suti wanaweza kuwa wastaarabu? Kuhusu thread yako this time umechemsha au hukujipanga vizuri au ulikuwa na lengo fulani jema ambalo labda sijapata concept yake mpaka hapo utakapofafanua vizuri.
 
Kuna watu wamerudia suala la kuvaa rangi za taifa; kwa kweli hili nimelipenda vile vile na naamini litabadili pia mtazamo wa kichama; binafsi ninachopendekeza mimi awali ilikuwa ni kuvaa rangi za chama chao (kwa sababu tuna utamaduni wa kuvaa rangi za vyama tayari) lakini kama hilo ni gumu basi wavae rangi za taifa na kuhamasisha wanachama nao kufanya hivyo hiyvo. Haya magwanda (ni maoni yangu tu) kwa kweli yamepitwa na wakati wake.
 
Sawa mkuu,
Kwanza kabisa napingana na huo uchaguzi wa tatu ya kuwa kila mtu avae kivyake.
Tukichua huo wa pili wa rangi ya chama nadhani na wenyewe una ugumu wake ukizingatia kuwa hata bendera za chama zenyewe kuna wakati inabidi tushone vitambaa vyenye sifa (material) tofauti ili mradi tupate rangi takikana, itakuwaje kwenye nguo ya kuvaa iwe imechanganywa material hapa polista, hapa kotoni, hapa sijui nylon; hii haijakaa sawa.

Chaguo la kwanza kwangu naona limekaa vizuri, yaani kuvaa komboti. Suala linabaki kuwa zinapatikana vipi na wapi, kwa wenzetu chama cha magamba nadhani utaratibu wa kupatikana sare zao unafahamika: ni kuwa unapewa sare, unalipwa pesa na unaletewa usafiri wa kwenda na kurudi kwenye mkutano.

Nakubaliana na wewe kuwa imejengeka taswira kuwa kombati ni mavazi ya viongozi. Nadhani ni wakati sasa wa kuondoa taswira hiyo, na viongozi watuweke wazi ni namna gani wapiganaji wa cdm wanaweza kupata kombati hizo. Kuna wakati nilishawahi kuuliza zaidi ya mara mbili kule kwenye page ya slaa (facebook) namna gani nitapata kombati hizo, lakini sikufanikiwa kupata jibu hivyo nami kama wananchi wengine ikanijengea picha kuwa huenda hizo ni sare za viongozi.
Natoa rai kwa viongozi kutengeneza utaratibu wa wanachama wote kuwa uniform hasa wakati wa mikusanyiko.
 
Sare ni muhimu ila ikumbukwe kuwa wapo wananchi wanaounga mkono hoja za CDM na ni wafuasi wa vyama vingine hivyo sio lazima wavae sare za CDM kwa sababu kadha wa kadha.

Kwanza wapo wafuasi ambao ni wa chama tawala (CCM) na kutokana na nafasi zao katika jamii hawawezi kuvaa sare za CDM, hawa wakiulizwa watasema wameenda kusikiliza hoja za CDM.

naunga mkono hoja ya hapo juu.........mapambano na harakati hizi ni za umma! inabidi yapate sura kuwa ni ya waTZ wote bila kujali itikadi zao za vyama, dini, rangi au kabila, inabidi yawe karibu zaidi na umma, cio wapenzi wa cdm tu! cdm bado inahitaji wanachama zaidi zaidi wale walioko vyama vingine na wasio na chama pia...

so HOJA YANGU NI :- kama jinsi vile wana'CDM watakavyohisi kuwa wao ni sehemu ya mapambano kwa kuvaa mavazi yao (kama Mwanakijiji anavyosema) VIVYO HIVYO wale wasio na chama au wasio CDM ndivyo watajihisi kuwa wao sio sehemu ya mapambano na harakati hizo. ni hayo tu wadau!
 
Hapa naona utata wa hoja.
Kuwe na sare ama kusiwe na sare?
Je viongozi wa CHADEMA wakivua hiyo sare wanayovaa watakuwa kwenye sare ipi inayowaunganisha na watu wake?
Askari kwenye picha wamevaa sare ambayo wale wananchi wao wanaowalinda na kuwapigania hawavai.
Nafikiri mtu hazuiliwi kuvaa sare ya CHADEMA.
 
Natofautiana na wewe, maelezo yako hayatoshi kwa vazi hilo kuachwa kutumika kwa makamanda wa chama
 
haya magwanda ulipenda yatumike kipindi gani ndo ungeona yanakwenda na wakati? mbona mimi naona kama hayo magwanda yanatumika kama vazi wakilishi tu! yaani unayashupalia kama vile yanakuathiri kisaikolojia utadhani labda ulishawahi vamiwa na majambazi waliovalia magwanda kama hayo! halafu mi nadhani ni vema katika shughuli za kitaifa watu wawe katika muonekano unaoashiria utaifa i.e bendera,mavazi n.k lakini katika shughuli za kichama watu wawe katika muonekano wa viashiria vya chama husika.
 
mwanakijiji inaonekana shida yake ni magwanda tu, hayapendi. si suala la muonekano wa pamoja. hii naona c issue, kubwa hapa ni cdm kuzidi kupiga mikutano wawafungue watu vichwa, tatizo letu tz imekuwa ni vichwa kulala juu ya uozo wa ccm na haja ya mabadiliko haswa vjjini c sare. hata ccm c wote wanavaa kijani, mwenye kupenda ananunua mwenyewe anavaa.ni kama watu wanavopenda timu za mpira za ulaya na kununua jezi za timu husika wanavaa.
 
Hivi kwani hizo combat zinatofautiana kwa mpiganaji na mpiganaji kulingana na renk yake (CHADEMA), Navyojua mm nikuwa kila mtu anashona ama ananunua sare hiyo kulingana na mapenzi yake, hazuiliwi kununua ya mikono mirefu ama mifupi! Hata slaa huwa namuona sometimes anavaa lile shati la nyekundu, blue na nyeupe na kepu yake. Tusiwe strict sana; hili siyo jeshi, wacha kila mpiganaji awe huru kuvaa jezi aipendayo kwa mapenzi yake.
 
Chadema siyo chama cha kijeshi wala cha kimgambo (not a military or para-military party). Ni chama cha kiraia na chenye malengo ya kufikia malengo ya kisiasa kwa kutumia njia za kiraia na siyo za kijeshi. Kama hili ni kweli basi symbolism ya chama inapaswa iwe hivyo hiyo kuanzia mavazi yake, lugha yake, na hata mwonekano wake. Kuna tofauti kati ya Wanaharakati na Wapiganaji (activists and fighters); kuna tofauti kati ya Viongozi na Majemedari (leaders and commanders).

Sasa mimi sina tatizo kabisa kama Chadema kinajionesha kama chama cha kijeshi au kiupaganaji; hili liwe wazi. Ni tatizo lile ambalo liko CCM vile vile - angalau CCM inasema ni chama cha "Mapinduzi" na katika historia yake kuna umwagikaji damu na militarization ya Chama. Nacho vile vile kama ilivyo hata CUF vinatakiwa vyote kuwa vyama vya kiraia kweli. Ningekuwa hata na uwezo yangefanyika mabadiliko ya kisheria kukataza kabisa vyama kuwa na semi-military identity kama hayo ya Makamanda, Red Guards, Blue Guards n.k Unless kweli tunataka kuwa na vyama vyenye mwelekeo wa kijeshi kama tulivyonavyo sasa.
 
ndugu yangu mzee mwanakijiji, ni chadema ipi uliyoona inavaa mavazi ya kijeshi? kama ni hapa tz mimi bado sijaona na sidhani kama dola mpaka leo hii ingekuwa haijawachukulia hatua, kwa uelewa wako wewe hivi unatumia kigezo gani kutambua vazi la kijeshi, je ni mshono wake, material yake,decoration pattern yake au kitu gani? vyama vya kijeshi huwa vina exist kwa nia ya kuchukua madaraka ya nchi kwa mtutu wa bunduki na hiyo si itikadi ya chadema ninayoijua mimi. halafu mimi sina hakika kama tafsiri ya neno mapinduzi katika ccm kuwa ni umwagaji damu kama unavyotaka kutuaminisha.
Hebu twende upande mwingine fikiria pale wanamuziki wanapovaa mavazi ya kijeshi na kunengua jukwaani huwa unapata taswira gani? ni bendi ya kijeshi au? mimi naona unakereka na jambo ambalo dhana yake haina mantiki unayofikiri wewe bali ni aina fulani ya ubunifu ambayo naona wewe hukubaliani nayo lakini wapo wanaokubaliana nayo and u r going to exhaust yourself trying to convince people who will always disagree with you on this issue, just try something else!
 
Back
Top Bottom