Picha za Makamanda Vitani na Wapiganaji wao: CHADEMA yaweza kujifunza somo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha za Makamanda Vitani na Wapiganaji wao: CHADEMA yaweza kujifunza somo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 20, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Unapokuwa vitani kuna suala moja ambalo mtu yeyote anayefuatilia mambo ya vita au jeshi analijua. Makamanda na Wapiganaji wote huvaa mavazi yanayofafa bila kujitofautisha. Kuna sababu kubwa mbili: Kwanza ni suala la uniformity (sare) wakati wa vita ili kuonesha ule umoja wa wapambanaji wote majemedari na wapiganaji wote wako katika vita vimoja - hivyo makamanda hawavai nishani zao au mavazi yao ya sherehe au mapambo bali huvaa mavazi ya wapiganaji wote. Sababu ya pili ni ya kiusalama zaidi - kamanda akiwa amejitofautisha kwa mavazi yake na wapiganaji wake ni rahisi adui kumlenga yeye hivyo wanapovaa mavazi yanayofafa ni vigumu kwa adui aliye mbali kujua kamanda ni yupi zaidi. Hapa kuna somo. Yote haya mawili yanatoa sababu ya tatu kwamba Kuna umoja wa kamandi toka walio juu kwenda walio chini katika mapambano ya pamoja.

  Niliandika jambo hili zaidi ya mwaka mmoja uliopita sipendi mavazi ya mgambo ya Chadema ambayo yanawatenganisha viongozi wao na wanachama wao na hivyo kufanya wawepo "makamanda" ambao wako tofauti na wapiganaji wao. Haya mavazi ya mgambo kwangu ni kama mavazi ya mapambo ya wanajeshi ambayo wakipenda wanaweza kuvaa ofisini, wanapokutana wao wenyewe n.k lakini inapokuja kwenye kukutana na wananchi wao au kuhamasisha wananchi wao (wapiganaji) ni muhimu wakavaa mavazi ya rangi ya chama ili kutimiza malengo hayo matatu.

  Na hili pia linanifanya nisielewe kabisa kwanini wanapoandamana wanazungukwa kwenye mduara na watu walioshikana mkono wakati wako kwenye mapambano!! Nani anawazunguka mkono wananchi wengine. Kuna utaratibu mzuri wa kusimamia ulinzi - kuweka mistari ya walinzi nyuma ya kidogo ambao nao wamefanana kimavazi na wanachama wao.

  picha:
  [​IMG]

  Gen. Tom Hobbins (left), U.S. Air Forces in Europe commander, and Chief Master Sgt. Gary Coleman (right), USAFE command chief, greet Senior Airman Kenyata Jenkins (second from right) and other members of 376 ESVS during the general's trip downrange July 5. (kuoka USAF)

  [​IMG]

  Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje Ulinzi na Usalama Wilison Masilingi (kushoto kwa afande Mwamunyange) wakipata maelezo mara baada ya ufunguzi wa maonesho na maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45. Mh. Masilingi alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho hayo yanayoendelea katika kikosi cha 603 cha jeshi eneo la Airwing ,Ukonga jijini Dar (Kutoka Kadidi Blog)

  [​IMG]

  Mwamunyange akiwa na Dr. Mwinyi baada ya milipuko ya Gongo la Mboto (angalia wapiganaji walio nyuma yake)

  [​IMG]

  Nyerere akimvisha nishani Kanali Mahfoudh.

  [​IMG]

  Kamanda Mkuu wa CCM na chipukizi - fikiria Chipukizi huyo anavyojiona ni sehemu ya CCM.

  [​IMG]

  Inatuachia chaguzi mbili au tatu:

  a. Makamanda wa Chadema na wanachama wavae rangi za chama wote
  b. Wanachama wote wavae mavazi ya kikamanda
  c. Kila mmoja ajivalie kivyake alimradi kila mmoja anapigana kivyake.

  Kwa ufupi, ni lazima kuwe na uniformity of sort siyo katika ujumbe tu bali pia katika mwonekano. Ndio maana ya kuwa kwenye mapambano pamoja. Unless... ni mapambano ya makamanda.

  My fifty cents.
   
 2. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  I couldn't agree with you more..............

  Uniformity means, we are all in this battle together
   
 3. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  thea you are
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Nadhani tutaelewana tu
   
 5. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mwanakijiji kwa hili ckubaliani na wewe,mwalimu mmoja alikua anatoa maelezo juu ya wanafunzi wavaaje,yeye alisema hata mtu aje amevaa suti au hata msuli yeye aje,mana anafundisha "KICHWA" na si mavazi.likewise to chadema wanaelimisha vichwa si mavazi.
   
 6. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Uniformity is important.kuna mwalimu wangu aliniambia chanzo cha kuvaa uniform shuleni ni kuondoa utofauti(matabaka).nimesoma na watoto wa majaji,wakuu wa polisi,madaktari na wauza vitumbua na siku zote nilijihisi mwanafunzi.lazima tuwajenge wafuasi wetu nao wajihisi ni makamanda.
  Heko mwanakijiji!
   
 7. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji ninakubaliana nawe kabisa - tena tayari wana rangi nzuri tu (nyekundu, bluu, na nyeupe, nyeusi) ambazo zitawapa uhuru wanachama na wapenzi kuchanganya kwa namna kila mtu anavyopenda. Nina matumaini viongozi ama makamanda watazingayia hoja yako.
   
 8. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kweli mkuu!gwanda la rangi yoyote linavutia hata nyeupe kuashiria amani.hata humu jf mara nyingi watu wanaulizia jinsi ya kupata magwanda ya cdm.
   
 9. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 880
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 80
  Siyo rahisi kutegemea wavae sare wote, na wala siyo fair kuwalaumu. Hata Chama tawala hawavai sare wote.

  Siyo vema ku-extend falsafa za majeshi kwenda kwa raia ambao kila mtu anaishi kwake na kujihemea kivyake. Wanajeshi wanaweza hii kwa sababu;

  - inabidi wafanane kuleta nidhamu
  - kazi zao zinalazimu wavae magwanda ya kijeshi
  - wana uwezo wa kifedha na ki-logistic
  - magwanda yanatolewa bure kwa wavaaji

  Lakini yote haya unayajua MMKJJ, au you are just pulling our leg?:tonguez:
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Jamani, What is the story behind that COl Mahfoudh? Is he dead or alive? what was the highest rank he reached in the JWTZ?
   
 11. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Yatakuwa yaleyale ya watu wa ccm, kila sehemu na mijezi yao!
  Mi nadhani hizo Kombati za kikamanda kama aliyoipiga mzee Nyerere hapo na kama ambavyo zinatumika na CDM saiv ndio itakuwa poa!
  Hivyo ingewekewa namna nzuri zaidi ya upatikanaji wake kwa wapenzi wooote.... lakini mirangi ya bendera itakuwa ni copy n' paste ya ccm.
   
 12. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Remained a Colonel for the rest of his career.He spent his later days in Mozambique and died there. They buried him in Mozambique in full national honours (Mozambican)
   
 13. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  chadema mambo yote!
   
 14. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  ukweli halisi kuhusu sare za chadema ni zile zilizopo kwenye bendera ya chama na ndizo rangi rasmi za chama . lkn ni muhimu kutambua kitu kimoa kuwa ubunifu wa kutumia magwanda umeongeza hamasa zaidi ukizingaatia kuwa mavazi yana nafasi yake katika kufanikisha jambo fulani. siasa ni mzchezo unaohitaji ubunifu wa hali ya juu. huu ni ubunifu mkubwa katika sisa. go chadema!
   
 15. T

  T.K JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  MMKJJ hayo mavazi unayoyaita ya mgambo ni kwa mtazamo wako kama ulivyosema. Lkn amini usiamini hayo mavazi yanaleta hamasa kubwa sana miongoni mwa vijana ambao ndi supporters wakubwa kwani yanaongesha ni mavazi ya watu walio tayari kwa mapambano....ukisema viongozi wavae mavazi ya kichama sawa labda huko kwenye mikutano ya ndani lkn kwa hapa kwenye maandamano acha tu wavae hivyo hivyo. Ukianza mambo ya wote kuvaa sare za chama haitakuwa na tofauti na CCM...siasa sio lazima wote mtumie staili ile ile.
   
 16. H

  Hosida Member

  #16
  May 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sare ni muhimu ila ikumbukwe kuwa wapo wananchi wanaounga mkono hoja za CDM na ni wafuasi wa vyama vingine hivyo sio lazima wavae sare za CDM kwa sababu kadha wa kadha.

  Kwanza wapo wafuasi ambao ni wa chama tawala (CCM) na kutokana na nafasi zao katika jamii hawawezi kuvaa sare za CDM, hawa wakiulizwa watasema wameenda kusikiliza hoja za CDM.

  Wapo watu ambao kutokana na kazi zao hawawezi kujiweka hadharani kuwa wao ni wafuasi wa CDM kwa ajili ya usalama wa kazi zao na maisha kwa ujumla.

  Hoja ya kuvaa sare ni nzuri ila sio lazima sare zivaliwe kwa wafuasi wote.
   
 17. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #17
  May 20, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe sio wakati wa kufuata mkumbo wa CCM, sare ya viongozi wa CHADEMA liko nuetral CHADEMA ni chama kinachojaribu kuwatetea wananchi bila kujali ni wachama kipi, kujikita katika sere za chama kitawanyima uhuru baadhi ya wanachama au wasio wanachama ambao hawataki kuonyesha hisia zao hadharani na ambao wanakubaliana na sera za CHADEMA.
   
 18. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mbona Nyerere alikuwa anakula gwanda pia?

  [​IMG]
   
 19. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #19
  May 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mahali popote pale penye umoja na mshikamano kuwa na vazi moja huwa kunaleta maana kubwa sana,kwani huuonyesha mshikamano wenu na kauli yenu huwa ni moja tu,sare hujaribu kuleza kwa vitendo mahusiano yaliopo kati ya mvaa sale na asiyekuwepo ktk sare

  hivyo basi ili tuwe wamoja na kuonyesha mshikamano wetu sare ya pamoja huwa ni muhimu sana kwa kauli moja kwa maendeleo ya Taifa letu
   
 20. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,915
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Mavazi...So cheap!!ngoja tu-brush vichwa na matongotongo kwanza...badae tuangalie mengine
   
Loading...