Picha za kuogofya: Amzika mwanae akiwa hai kisa ameahidiwa kuolewa na tajiri

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
863
1,000
AZIKA MWANAE AKIWA HAI KISA AMEAHIDIWA KUOLEWA NA TAJIRI
112.jpg
Mama mmoja amezika mwanae wa miezi mitatu akiwa hai baada ya kuahidiwa kuolewa na kijana tajiri. Mama huyo hakutaka kumwambia mwanaume huyo kuwa tayari alikuwa amezaa mtoto na mwanaume mwingine.

Kwa ajili ya kutaka kudumisha uhusiano mpya na tajiri huyo ndipo alipoamua kufanya tukio hilo la kutisha. Alimvizia mtoto huyo amelala na kwenda kumzika akiwa hai.

Tukio hili limebainika baada ya ndugu na majirani kumuona pekee pasipo mtoto ndipo walimbana hadi akasema ukweli kuwa amemzika mtoto huyo siku mbili zilizopita.

Source: Mother buried her 3 months old baby after she met a rich man who
 

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
16,479
2,000
ALAFU BADO MTU ANANISHAURI NIWAHESHIMU HAWA WANAWAKE WENYE AKILI ZILIZOPO UKENI.???


Mnisamehe ,nitakua wamwisho...Wanawake wakileo bana ,,Wachache wanaojitambua.
 

talentboy

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
1,893
2,000
kummamake huyu dada..aise sipati picha huyo mtoto tafrani alizojipatia akiwa anakata roho ndani ya hilo shimo...yaani wakati anaipapatua pumzi ya uhai wake huku taratiibu na kwa maumivu makali sna akipoteza tumaini la uhai.

Mungu sijui atamfanya nini huyu mama kama akifa bila kutubu toba ya kweli.
 

Sagungu 1914

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
829
500
Eti baadaye utasikia tunataka haki sawa,haki sawa na viumbe hawa,hapo kwa kweli mm siko tayar kuwapa haki sawa.Hawana adabu
 

Dinazarde

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
37,758
2,000
Nnavyompenda mtoto wangu nampenda kuliko mtu yeyote hapa duniani
Huyu dada anatakiwa aishi sayari nyingine maana sijui hiyo roho yake,,nimesikitika sana ni bora kuacha kuzaa kama huwezi kulea,,angenipa hata mie nikalea tu maana naweza lea mtoto yeyote tu ,nawapenda sana watoto aisee ,,huyo mme alieoa ajiandae kutolewa roho
 

Nsamaka

JF-Expert Member
Sep 4, 2016
5,785
2,000
Aisee kisa ndoa tu??? Bora kukosa ndoa kuliko kuua mtoto wangu.
Hv huyo mama alipata kweli uchungu?
 

Ty_Vigilante

JF-Expert Member
Jan 19, 2015
2,703
2,000
Alafu utasikia GENDER EQUALITY, mmh nadhani elimu na ukaribu unahitajika sana kwa hawa wake na Dada zetu, cause wakiamuaga kufanya ubaya kwa nia ya kupendwa ama kupata wanalotaka lolote wanafanyaga tuu, Mola atupe uhai tuzidi kuelimishana japo taratibu ila kwa uhakika b4 hilo pepo chafu la equality halijasambaa sana.
 

TEAM VIBAJAJI

JF-Expert Member
Oct 9, 2016
1,863
2,000
Kama ameweza kuua mtoto aliye mzaa kwa uchungu atashindwaje kuniua/kumuua mumewe kwaajili ya mali ....nimewaza kwa sauti tu
 

kifaduro

JF-Expert Member
Nov 27, 2017
224
250
AZIKA MWANAE AKIWA HAI KISA AMEAHIDIWA KUOLEWA NA TAJIRI

Mama mmoja amezika mwanae wa miezi mitatu akiwa hai baada ya kuahidiwa kuolewa na kijana tajiri. Mama huyo hakutaka kumwambia mwanaume huyo kuwa tayari alikuwa amezaa mtoto na mwanaume mwingine.

Kwa ajili ya kutaka kudumisha uhusiano mpya na tajiri huyo ndipo alipoamua kufanya tukio hilo la kutisha. Alimvizia mtoto huyo amelala na kwenda kumzika akiwa hai.

Tukio hili limebainika baada ya ndugu na majirani kumuona pekee pasipo mtoto ndipo walimbana hadi akasema ukweli kuwa amemzika mtoto huyo siku mbili zilizopita.

A single mother buried her 3 months old baby after she met a rich man who promised to marry her.

She did not tell the rich man that she already had a child from a married man. In order to save her new relationship with the rich young man.. she decided to play single by getting rid of the child.

Sadly she buried her the child alive while the child was asleep. This is sad brothers and sisters.

Share ili kupinga na kukomesha vitendo viovu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom