Picha za Facebook Zasababisha Anyimwe Pasipoti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha za Facebook Zasababisha Anyimwe Pasipoti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 12, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwanaume mmoja toka nchini India ambaye alijifanya yeye ni mkimbizi toka Tibet ili aweze kupata 'makaratasi' ya nchini Australia, amefikishwa mahakamani baada ya picha zake alizoziweka kwenye Facebook kuonyesha kuwa yeye ni raia wa India.
  Mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa kwa sababu za kisheria, aliingia nchini Australia mwaka 2009 kwa kutumia pasipoti ya India na kisha kwenda kujilipua kwa kujifanya yeye ni mkimbizi toka Tibet.

  Mwanaume huyo alidai kuwa yeye ni mtoto wa mwanaharakati wa kutetea haki za watu wa Tibet ambaye alikimbia toka Tibet mwaka 1991 kuukimbia ukatili wa utawala wa China nchini Tibet.

  Aliendelea kusema kuwa alilelewa katika kambi ya wakimbizi nchini Nepal ambako pia alimaliza elimu yake ya msingi.

  "Kama nikirudi Nepal, serikali ya Nepal itauruhusu utawala wa China nchini Tibet unichukue hivyo watanitesa na hatimaye kuniua", alisema mwanaume huyo wakati wa kujilipua kabla ya siri zake kufichuka hivi karibuni.

  Hata hivyo picha zake kwenye mtandao wa Facebook zikimuonyesha akiwa na wanafunzi wenzake nchini India zimepelekea maombi yake ya kupewa uhalali wa kuishi Australia kukataliwa.

  Mwanaume huyo alifikishwa mahakamani ambapo mahakama ilionyeshwa picha zake kwenye Facebook zikimuonyesha akiwa amevaa unifomu za shule moja iliyopo katika mji wa Bengal nchini India.

  Katika profile yake ya Facebook mwanaume huyo alijitambulisha kuwa amemaliza masomo yake nchini India.

  Mojawapo ya picha zake kwenye facebook ilimuonyesha mwanaume huyo akiwa pamoja na dada yake wakiwa wamevaa unifomu za shule wakiwa kwenye bustani ambayo nyuma yake kulikuwa na bango lenye maandishi ya Kihindi.

  Picha zake zingine kwenye mtandao wa Hi5 zilimuonyesha akiwa amevaa unifomu za shule akiwa amepozi pamoja na wanafunzi wenzake wa nchini India.

  Mahakama iliambiwa kuwa uchunguzi wa polisi umeonyesha kuwa mwanaume huyo ni raia wa India na anamiliki pasipoti ya India na wala si mkimbizi wa Tibet kama alivyodai baada ya kuwasili nchini humo.

  Madai yake ya ukimbizi yamekataliwa huku mwanaume huyo akikabiliwa na kesi nyingine ya udanganyifu.
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  ukitaka kudanganya, haribu asili yako yote.
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  asili haipotei kuna siku utadakwa tu Nazjaz
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ukiwa muongo usiwe msahaulifu. Hakujipanga vizuri katika kudanganya!
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hii teknolojia ya internet inafichua mambo mengi sana hasa hizi social networks katavi we subiri tu tutajua mengi sana sema kwa nchi kama bongo wenye access ya net ni wachache sana!so informations za watu wengi hazijulikani
   
 6. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
Loading...